Home
Unlabelled
mji kasoro bahari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hii picha inanikumbusha sana home.Stand imapendeza ila inabidi tuwe wastaarabu huto tuvibanda katikati na pembeni tunaharibu madhari inabidi vibanda viwe na mpangilio.Vinakuwepo katikakti na madhari unaonyesha kama hakuna master plan iliyotengenezwa na kufuatwa
ReplyDeleteSafu za milima mmmmmm mwayego vinavutiaga mmm kina Mloka big up
Kaka Michuzi umenikumbusha mbali we acha tuu. Nakumbuka wakati nikisafiri kutoka Dar kuelekea Turiani, nikiunganishia basi au costa hapo msamvu, wale wapiga debe walikuwa wakidaka watu na mizigo yao wakiwa wanashuka toka kwenye mabasi. usipokuwa mkali na makini mizigo hutaipata. Nilikuwa kabla sijashuka kwenye gari nakunja sura kwanza halafu ndo nashuka taratibu, wanasogea pembeni wenyewe, utasikia kwa mbali; mvomero.kilakala, taxi,turiani short cut. Kuna vijimambozi usafiri wa Tanzania.
ReplyDeletenyumbaniiii...i looove morogoro!!!
ReplyDeleteMwanangu Michuzi hapo umenigusa, hiyo ndiyo Mji kasoro bahari tu!Miaka kadhaa sijaitia macho MG naona Mlima Uluguru jani limekubali kwelikweli tena la asili.
ReplyDeleteNyie kina michuzi kwa kulalamika ni kiboko yao. Utawasikia "Morogoro mji kasoro bahari,Nyerere alikataa kutuletea bahari Morogoro".
ReplyDeleteMorogoro zama za miaka ya 70 na 80 ilikuwa babu kubwa nakumbuka wakati huo niko teenage watu walikuwa wanatoka DAR kuja week-end kwenye mara MORO, dansi, sinema na mpira, ukiwa DAR kila mtu utasikia naenda MORO week-end kwenye dansi, au sinema, au mpira, au hata kutembea tu, vi-coaster vilikuwa kibao. zama hizo hali ilikuwa mswano.
ReplyDeleteMkubwa wa naniii hapo hata mimi nimekubali hii taswira maana imetulia sema hizo camera ndio zinahitaji nyongeza! Mdau B20 (Bham)
ReplyDeletekaka michude wee acha tu umenikumbusha mbali sana wangu. Yaani hapo kwa pembeni kuna hoteli inaitwa Makuti hapo nilikuwa najirusha kwa kwenda mbele mziki wa zamani mambo ya Mbaraka Mwinshehe! Sina hata la kusema kaka michuzi. Nakubaliana na anony hapo juu kuwa enzi hizo starehe Morogoro lakini mpaka sasa starehe zipo wangu. Michude umenihamasisha ngoja nirudi Moro wangu! Unamenikumbusha wimbo mmoja wa Mbaraka unasema hivi: "Jamani Morogoro mje mjionee Moro, maji yatiririka milimani Moro,si mchezo!!Nyumbani kuzuri jamani. Asante sana kaka michuzi.
ReplyDeleteMdau - Surrey