Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akimvalisha tunzo ya ushindi wa mwananchi bora wa Wilaya ya Mwanga Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh. David Cleopa Msuya wakati wa sherehe za baraza la Eid El Fitry zilizofanyika kitaifa katika msikiti wa AL-MASJID MUNAWARA katika kitongoji cha Mororo Wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. suprise, suprise!!

    ReplyDelete
  2. kuna mwanakijiji mwingine afahamikae huko?...hehehe
    CCM bwana...never seize to amaze me.
    Mbona wanaendeleza haya mambo ya kiujamaa mpaka leo? Si wachague moja...ujamaa au ubepari.
    Kumetumika criteria gani kuchagua mwananchi bora?

    ReplyDelete
  3. EAC ilipovunjika Cleopa Msuya alipewa jukumu la kusimamia zoezi la kuanzisha viwanda Tanzania ktk kutekeleza azma yetu ya kujitegemea.

    zoezi hilo alilisimamia kwa ufanisi mkubwa.

    awamu ya kwanza ya utawala wa Raisi Mwinyi, Msuya alipewa jukumu la kusimamia marekebisho ya uchumi, kupambana na mfumuko wa bei, uhaba wa bidhaa, na kurejesha mahusiano mema na wafadhili na vyombo vya fedha vya kimataifa.

    john malecela alipolazimishwa kujiuzulu taifa lilimgeukia Cleopa Msuya kurudisha heshima ya serikali iliyokwenda likizo ktk kukusanya kodi, na kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu 95 unafanyika kwa kutumia fedha zetu za ndani.

    Cleopa Msuya siku zote ulitekeleza majukumu yako bila majungu na kutafuta kujikweza.

    ReplyDelete
  4. wanakijiji wengine wa Mwanga ni Dr.Asha-Rose Migiro, Prof.Jummanne Maghembe, Lt.Gen.Abdulrahman Shimbo,Prof.Jummanne Maghembe,Prof.Yunus Mgaya,Prof.Iddi Mwindadi Mmbaga,Prof.Abdulrahmani Msangi, Khatibu Kihiri Senkoro,Balozi Fadhili Mmbaga,Balozi Radhia Mtengeti Msuya, VC Mwantumu Malale......

    ReplyDelete
  5. mwananchi bora kwa category gani? Mimi naona hii ingeenda kwa mwananchi amabte anaishi normal life na anajitahidi kukabiliana na ugumu wa maisha na bado anakuwa na moyo wa kujitolea kusaidia jamii


    Hii hapa wala hainogi kwa vile tunajua uwananchi wake bora ni kwa ajili kazi alizowahi kushika na wala sio jingine

    ReplyDelete
  6. Na yeye ndiye aliyeteuliwa na Mwalimu aongoze Timu ya Watanzania kwenda kujadiliana na IMF na BENKI YA DUNIA kuhusu Ubinafsishaji wa Uchumi wa Tanzania,na kilichofuata kila mtu amekiona!This Photograph tells it all,the smiles!Abracadbra!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...