Habari balozi Michuzi,
Nafurahi kwa jinsi unavyotuhabarisha, kutuelimisha na hasakutuburudisha. Mimi huwa nikiingia humu lazima nipate chakunifurahisha.
Nasikitika sana baadhi ya wanaume wanapoachana na wenziwao huanza kusambaza picha za uchi walizowapiga kupitia kamera za simuzao kwenye mitandao ya picha za utupu, kwenye magazeti na pia katikasimu za watu wengine kwa nia ya kumchafua kumdhalilisha na kumnyimauhuru wa maisha yake.
Hali hii husababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi,wanawake kukimbia miji, kudharaulika mbele ya jamii inayomzunguka nawakati mwingine husababisha maafa. Ushauri wangu kwa wanawake, kamweusikubali kupigwa picha zinazoonyesha utupu wako hata kama mpenziuliyenaye anakupenda kiasi gani au hata kama tayari ni mchumba aumumeo kwani huwezi kujua ya kesho.
Pia inaweza kutokea bahati mbayasimu hiyo kupotea au kuibwa na kuangukia mikononi mwa adui yako. Pichahizo zinamgharimu zaidi msichana pale anapokuja kuwa kiongozi fulaniau mtu maarufu.
Kuna mtangazaji mmoja nchi jirani alikuwa anazinunuapicha alizopigwa na mpenzi wake waliyeachana naye kabla hajawa maafurulakini alishindwa baada ya kugundua anatumia pesa nyingi sana bilamafanikio kwani picha hizo zilikwisha sambaa kila sehemu.
Sijui mwishowake ulikuwaje ila chonde chonde dada zangu na kamera za simu za wapenzi wenu.
Mdau Pretlue.
Mdau Pretlue.
Tarime.


Wadau hii inaboa sana, kuna bwana mmoja alimwacha mke wake kwa sababu kama hizi. Hivi inakuaje we mwanaume ukiona hupendwi tena unaamua kumchafua mwenzako ili asipate mwanaume mwingine tena? Kuna baadhi ya wanaume mi wananikeraaa! Kuna wakati nafikiria sijui niishi peke yangu tu.
ReplyDeleteHusna Mpemba.