Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impack wakiwajibika wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani mjini Morogoro Jumapili chini ya udhamini wa Zain ambayo ilichangia zaidi ya sh. milioni 30 kwa Wiki ya Usalama Barabarani na kupewa tuzo na kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani.

Waimbaji wa bendi ya Akudo Impack wakicheza wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani mji kasoro bahari.
ZAIN Tanzania, kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayoongoza kwa huduma bora nchini imetoa zaidi ya sh. milioni 30 kuchangia usalama barabarani, hivyo kupewa tuzo na kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani.
Zain ilichangia stika za usalama barabarani zenye thamani ya sh. milioni 30 kwa ajili ya Polisi wa usalama barabarani ili kuwasaidia kuhakikisha Usalama Barabarani na kuadhimisha Wiki ya Usalama Barabarani iliyozinduliwa Jumapili mjini Morogoro na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, James Kombe aliishukuru Zain kwa kujali na kutambua umuhimu wa Wiki ya Usalama Barabarani na kutambua juhudi zinazofanywa na Polisi wa Usalama Barabarani.
“Tumeunga mkono kampeni hii kwa miaka sita iliyopita na tunaona fahari kujumuika tena na Polisi wa Usalama Barabarani katika mradi huu wa kuhakikisha usalama barabarani,’’ alisema Meneja wa Zain Tanzania Kanda ya Kati, Samson Majwala.
Mchango huo pia umedhihirisha uwajibikaji wa Zain kwa kuunga mkono shughuli za jamii wanayoihudumia. "Tunaamini mchango wetu utasaidia juhudi za polisi wa usalama barabarani na kuhakikisha usalama katika barabara zetu. Zain inaahidi kuendelea kuiunga mkono polisi katika kipindi cha miaka mitano ijayo," alisema Majwala.
Mbali ya kutoa stika zilizosambazwa nchini kote, Zain pia ilichangia makoti 1,500 ya kujikinga mvua yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 34.
Majwala alisema Zain inaahidi kuendelea kutoa huduma kwa jamii na itaendelea kujihusisha katika shughuli mbalimbali kwa kutoa michango ya hali na mali ili kusaidia kuinua uchumi na maendeleo ya jamii ya Tanzania kwa ujumla kwa kutekeleza kauli mbiu ya kutoka ‘Making life better’ (Boresha Maisha) hadi kuwa ‘A Wonderful World’ (Ulimwengu Maridhawa).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kak michuzi kama mambo yenyewe ndio hivyo usalama hupo kweli barabarani hapo juu.

    ReplyDelete
  2. Haya tena waongeaji kwa picha, hao wanenguaji wa akudo wanatupa msg gani. ni pweeee? au puuuu? au fyuuuu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...