
Mheshimiwa Samuel Sitta (Mb.),
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,
DODOMA.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,
DODOMA.
Yah: SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHESHIMIWA RICHARD NYAULAWA (MB)
Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Richard Nyaulawa, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kutoka Chama cha Mapinduzi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Kwa niaba yangu binafsi, familia yangu, Serikali na kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi, nachukua nafasi hii kukutumia salamu zangu za rambirambi kwako wewe Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na, kupitia kwako, kwa familia ya Marehemu Nyaulawa na Wabunge wote.
Kifo cha Mheshimiwa Nyaulawa kimetokea wakati ambapo alikuwa anahitajika sana na watu wote.
Kifo cha Mheshimiwa Nyaulawa kimetokea wakati ambapo alikuwa anahitajika sana na watu wote.
Kifo chake kimewagusa na kuwasikitisha watu wengi nchini. Wabunge wamepoteza Mbunge mwenzao wa kutumainiwa kwa mambo mengi. Marehemu alikuwa mtu mtaratibu lakini makini sana na muungwana, mambo ambayo yalimfanya awe kipenzi cha wengi. Chama cha Mapinduzi kimepoteza kiongozi na kada wake mahiri. Familia yake imepoteza baba mpenzi, mlezi na nguzo ya kutegemewa.
Wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini wamepoteza mwakilishi na mtumishi wao wa kutumainiwa. Jamii ya Watanzania nayo imempoteza kiongozi na mwanajamii mwema mwenye ukarimu na moyo wa huruma.
Wengi wetu tutamkumbuka Mheshimiwa Nyaulawa kwa mchango wake muhimu Bungeni na katika jamii. Alikuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi wa Jimbo lake na Watanzania kwa ujumla.
Kwa dhati ya moyo wangu, naungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Naelewa machungu waliyonayo wanafamilia, lakini napenda kuwahakikishia kwamba machungu hayo sio yao peke yao bali ni yangu pia na Watanzania wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na kuwafariji.
Ni maamuzi yake Mola, na kazi yake daima haina makosa.
Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aiweke roho yake mahali pema peponi.
Amin.
Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
innaalillahi wainnaa ilayhi raajiuna.
ReplyDeleteJamani lakini haii barua si kopi and paste?
poleni wafiwa mungu atawapa subira.
ReplyDeleteyaani watanzania inasikitisha sana hata kuwapa pole wafiwa mnashindwa kazi kuzozana tu na matusi,madongo na umbea ndo kazi yenu mnashindwa hata kutoa comments za pole na masikitiko kweli bado tupo nyuma sana katika ustaarabu.
Poleni sana watu wa Mbeya hasa jimbo la Mbeya vijijini, poleni pia familia na Ndugu na jamaa. Mungu aiweke mahali pema peponi. Ameni
ReplyDeletemichu umeibania meseji yangu,,poa tuuu lakini
ReplyDeletewewe ni walewale tu sii uko sirikalini??EPA mdogo nini wewe??
poleni wafiwa na ndugu zangu wa Mbeya
ILA KUFA WATAKUFA TU