march 20, 2008: waziri wa afya profesa david mwakyusa akisalimiana na mh. richard nyaulawa alipomtembelea katika hospitali ya apollo huko india ambako mbunge huyo wa mbeya vijijini alikuwa kalazwa kwa kansa ya tumbo. usiku wa kuamkia jana mh. nyaulawa alitutoka.
Mheshimiwa Samuel Sitta (Mb.),
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,
DODOMA.

Yah: SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHESHIMIWA RICHARD NYAULAWA (MB)
Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Richard Nyaulawa, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kutoka Chama cha Mapinduzi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Kwa niaba yangu binafsi, familia yangu, Serikali na kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi, nachukua nafasi hii kukutumia salamu zangu za rambirambi kwako wewe Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na, kupitia kwako, kwa familia ya Marehemu Nyaulawa na Wabunge wote.
Kifo cha Mheshimiwa Nyaulawa kimetokea wakati ambapo alikuwa anahitajika sana na watu wote.
Kifo chake kimewagusa na kuwasikitisha watu wengi nchini. Wabunge wamepoteza Mbunge mwenzao wa kutumainiwa kwa mambo mengi. Marehemu alikuwa mtu mtaratibu lakini makini sana na muungwana, mambo ambayo yalimfanya awe kipenzi cha wengi. Chama cha Mapinduzi kimepoteza kiongozi na kada wake mahiri. Familia yake imepoteza baba mpenzi, mlezi na nguzo ya kutegemewa.
Wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini wamepoteza mwakilishi na mtumishi wao wa kutumainiwa. Jamii ya Watanzania nayo imempoteza kiongozi na mwanajamii mwema mwenye ukarimu na moyo wa huruma.

Wengi wetu tutamkumbuka Mheshimiwa Nyaulawa kwa mchango wake muhimu Bungeni na katika jamii. Alikuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananchi wa Jimbo lake na Watanzania kwa ujumla.

Kwa dhati ya moyo wangu, naungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Naelewa machungu waliyonayo wanafamilia, lakini napenda kuwahakikishia kwamba machungu hayo sio yao peke yao bali ni yangu pia na Watanzania wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na kuwafariji.
Ni maamuzi yake Mola, na kazi yake daima haina makosa.
Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aiweke roho yake mahali pema peponi.
Amin.
Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. innaalillahi wainnaa ilayhi raajiuna.
    Jamani lakini haii barua si kopi and paste?

    ReplyDelete
  2. poleni wafiwa mungu atawapa subira.

    yaani watanzania inasikitisha sana hata kuwapa pole wafiwa mnashindwa kazi kuzozana tu na matusi,madongo na umbea ndo kazi yenu mnashindwa hata kutoa comments za pole na masikitiko kweli bado tupo nyuma sana katika ustaarabu.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana watu wa Mbeya hasa jimbo la Mbeya vijijini, poleni pia familia na Ndugu na jamaa. Mungu aiweke mahali pema peponi. Ameni

    ReplyDelete
  4. michu umeibania meseji yangu,,poa tuuu lakini
    wewe ni walewale tu sii uko sirikalini??EPA mdogo nini wewe??
    poleni wafiwa na ndugu zangu wa Mbeya
    ILA KUFA WATAKUFA TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...