Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hiyo ni kweli KP ila mipira yote ilitokea kwa "wataalamu wa move" wachezaji wa S maana kila mchezaji ana jukumu lake uwanjani!!!

    ReplyDelete
  2. When we stand as a nation we have to forget all our differences, sasa hii ya nini tena!

    ReplyDelete
  3. Na Krosi zote za Taifa Stars Zimepigwa na wachezaji wa Simba! hapo mana yake kwamba Taifa stars wachezaji wengi ni Yanga Au YAnga na Simba lazima kuwepo na mchanganyiko ila wachezaji wawe wakali. Amir

    ReplyDelete
  4. alivyosema mhenga wa kizungu...'divided we fall united we stand'acheni ushenzi wa kusengenya uyanga na usimba...jukumu bado halijakamilika!!!JK BOYS OYEEEE!
    mabeba boksi wala hatuwataki!

    ReplyDelete
  5. Usimba na Uyangta hautusaidii chochote. Magoli yamefungwa na wachezaji wa Taifa Stars, na krosi zipepigwa na wachezaji wa Taifa Stars pia, ushindi ni wa Watanzania wote, umeletwa na wachezaji wa Taifa Stars wote (waliocheza na waliokuwa bench), waalimu,na wadau wengine wote.

    Acheni ubinafsi usiosaidia timu zaidi ya kuwagawa wachezaji. Tulipofungwa 4-0 na Senego mbona sikusikia mtu akisema tumefungwa 'sisi yanga' au sisi simba'?

    Nawaomba wachezaji wayapuuze maneno kama haya yasiyojenga.

    Mdawa.

    ReplyDelete
  6. KP huwa nakuamini sanaaa kwa ideas na mawazo yako. Lakini hapa umechemka!!! Mtazamo wa kishamba na kizamani huu. Unapodai magoli yote yamefungwa na Yanga basi Simba hatutakiwi kushangilia ushindi wa inchi yetu? Acha ushamba wa kizamani huo.. Hapa cha kujivunia ni Taifa letu siyo usimba na uyanga.

    Tatizo la ufisadi na wizi wa inchi hii ni ubinafsi ambao KP unauonyesha hapa.. Sisi, mimi... wao!!! huo ni ubinafsi haswa yanapokuja masuala ya kitaifa unaturudisha nyuma!!

    KP usitake kututenga!! Tena ushindwe na ideas zako za kishamba hizo. Team ikifungwa Sudan utasema imefungwa Yanga au Tanzania?

    ReplyDelete
  7. Nadhani nyie mnaemlaumu KP mna mawazo finyu sana na hamna exposure kwenye kwenye modern football. Wachezaji wa YANGA kufunga wanastahili credits as YANGA players. Theo Wallcot alipofunga mabao 3 England Vs Croatia, Wenger alitoa comments kwenye press za kusifia as Arsenal Player, hakuna aliyelalamika kwamba analeta U-Arsenal…Nyie mnealalamika ndo mna U-Simba na U-Yanga. Ni wazi kuwa first eleven ya STARS 80% ni YANGA, wao kufunga 3 si cha ajabu. Mapunda alipofungwa 4 na Senagal mlilalamika kuwa kipa wa Yanga hafai na kwanini kocha hakumtimia Kaseja..Acheni mambo ya ajabu..TAIFA STARS HUREY!!
    Mdau,BABATI.

    ReplyDelete
  8. Watu wana chuki na "wabeba boksi"!!
    Sasa hapa issue ya wabeba boksi imeingiaje?
    Pole sana ndugu yangu,utaendelea kulia kama sugura "sizitaki mbichi hizi"......

    ReplyDelete
  9. Anony 02 December, 9.06 hapo juu nakuunga mkono 100%. Hizi ni fikra potofu sana na zinaua uzalendo katika michezo. Mawazo kama haya yanaweza kuleta mgawanyiko mkubwa kiasi kwamba wachezaji wanaweza kupeana pasi kwa kuzingatia timu zao wanazotoka au kuamua kubutua tu mpira kwa mawazo kuwa mwanasimba au mwanayanga mwenzangu hayupo karibu kupewa pasi. Mawazo mengine ya mitaani hayafai kuwekwa kwenye hadhara na hayafai kuletwa na mtu kama KP ambaye anajua kuwa katuni zake zinasomwa na watu lukuki.Ningefurahi kama katuni yake hii ingekemea ubaguzi. Hata kama KP ni mpenzi wa Yanga yeye kama muelimisha jamii alitakiwa adumishe uzalendo.Hii idea ya ubaguzi siifagilii kabisa. Bradha KP kwa hili "umechemka".

    ReplyDelete
  10. Kwani ilikuwaje yeye na Fina kutimuliwa kwenye Clouds FM?

    ReplyDelete
  11. heeeeeeeeee kumbe????!!!!!

    ReplyDelete
  12. Mimi ni mpenzi Mkubwa sana wa YANGA na nafurahi wachezaji wa timu yangu wanapofanya vizuri hata timu ya Taifa ni jambo la kufurahia mchango wa timu yako ktk timu ya Taifa..., Ila tunapoanza kuwatambia watani wetu si jambo la busara kwani hilo halikuzi kiwango chetu cha mpira kama Nchi, na kama tukiendelea hivi maendeleo ya soka hayatatokea mapema kama tulinavyofikiria kwani hii italeta ubaguzi ndani ya timu na matokeo yake wajezaji watakuwa wanfuata maelekezo ya Viongozi wao wa vilabu na sio waalimu wao timu ya Taifa ..., Utanzania kwanza U simba na Yanga baadaye ... Mungu ibariki Taifa Stars, Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...