"Kaka naomba uiwakilishe hii picha ya askari wananihii aliyemuogeshadereva wa school bus pale kawe darajani kwa komba asubuhi ya leo baada ya kumwagia maji viatu vyake ambavyo anadai alivipiga kiwi leo asubuhi.
Haya sio ya kusikia nimeyaona kwa macho na watu wadau wengine pia walishuhudia.
Nawakilisha
Regards
Regards
Mdau Kawe kwa Komba
Inasikitisha sana kuona vitu kama hivi bado vipo, hapo wa kulaumiwa nani dereva, askari wa jeshi au serikali kwa kutotengeneza barabara. Kwa ufupi huyo askari anatakiwa kufikishwa mahakamani kwa kuchukua sheria mkononi kama leo anafanya hivi kesho itakuwaje? muda si mrefu niliona kwenye tovuti askari walifanya kitu mbaya sikumbuki kam ilikuwa pugu au mbagala.
ReplyDeletemkiambiwa bongo hakuna serikali wala sheria mnakuja juu dhidi ya watu walio nje ya bongo.Sasa hapa haki ipo wapi?
ReplyDeleteHaikuwa sahihi kumuazibu dereva,ukizingatia leo hali ya hewa niyamvua na hali ya njia zetu inaeleweka. Wote inapaswa kuchukua tahadhari na sio kutumia uafande hapa.
ReplyDeletehahahahaha...heheheheh...kwakwakwakwakwa....
ReplyDeleteDuuuh hii ni noma sana hii...!!nakumbuka enzi zile nikiwa bongo nasoma mzizima nikawa natokea home mitaa mbezi beach kufika maeneo ya makongo nikapita chobiz kukwepa foleni pale makongo sekondari ilikuwa siku ya mvua kwa makusudi nikakanyaga dimbwi la maji nikamwagia meja kagisa akiwa amevaa nguo za jeshi akiwa na afande miraji ambaye kwa sasa ni marehemu...ebwana eeh sitasahau hii siku walipanda gari tukaenda sehemu moja maeneo ya hapo wakanipa nguo nifue na zikauke kuda huo nikasema siwezi nikaomba msamaha wakanipa adhabu ya kukausha madimbwi ya maji duuhhhh nom sana...!!
mdau
Ukerewe
JAMANI HIVI HAWA WANAJESHI WAO MBONA HUCHUKUA SHERIA MIKONONI, MWENZENU SIFAHAMU NI KWANINI MAANA HATA UNAPOPITA MAENEO YA JESHI MARA UTAKUTA MTU ANAADHIBIWA KISA KAKATIZA ENEO LA JESHI. NA KUNA SIKU NILIPITA MAENEO YA LUGARO USIKU WA SAA SABA NA ROBO NIKITOKEA SAFARI MKOANI MBEYA NIKIRUDI NYUMBANI KWANGU BOKO NILISIMAMA ENEO LAO KUANGALIA KITU KILICHOKUWA KIKIPIGA KELELE CHINI YA GARI GHAFLA WAKANIVAA WANAJESHI NA WAKAANZA KUNIPIGISHA KICHURACHURA MBELE YA MKE WANGU NA HATA WALIPOMALIZA HAWAKUNIRUHUSU KUTOA KIBATI CHA GARI YANGU KILICHOFUNGUKA NA KUGUSA BARABARA HIVI KWANINI HAWA WATU HAWACHUKILIWI HATUA KWA VITENDO VYAO VYA KIDHALILISHAJI NA VISIVYOFUATA HAKI ZA BINADAMU?
ReplyDeleteNI MIMI MUATHIRIKA WA VITENDO VYA WANAJESHI
Unategemea tutamwonea huruma !. Mwache aogeshwe fara huyo....last week tuliikuta school bus kwenye mtaro tukabaki kujiuliza kama watoto waliokuwemo walisalimika vipi.......ngoja aogeshwe tena ukichukulia ni wachafu sana
ReplyDeleteHili ndilo linalojulikana kama Jeshi la WANANCHI. Na majeshi hawa ndio wanaotaka wapande daladala bure.
ReplyDeleteUdhalilishaji kama huu nilifikiri uko kule Zanzibar tu ambako ndio hakuna utawala wa sheria kumbe hadi huko bongo Jeshi la WANANCHI nalo huwafanyia wananchi udhalilishaji kiasi hiki? Lakini sishangai kwani Jeshi liitwalo la WANANCHI limewahi hata kutia mkong'oto kwa WANANCHI na hakuna lolote lililokuwa. Kwa ufupi ni kuwa Jeshi la WANANCHI linaogopwa na kila mwananchi.
Antway lakini tuseme mawilimawili, ivi huyu dereva kama angekimbia au kukataa kugaragarizwa ingekuwaje? Jamaa angempiga risasi? au kwa mfano wakati anagaragarizwa angemrushia huyu afande hayo maji machafi (teh teh teh) ingekuwaje?. Nahisi huyu jamaa alikuwa boza. Kama mie huyu afande angerusi nyumbani kwenda kubadilisha nguo. Mnasemaje wadau?
dah afande kamuonea sana dereva siangeweza kubrush tu tena kuliko kumchelewesha dereva wa bus la wanafunzi huo ni ukatili jamani, kaka michu nipo ufini aisee hapa chuoni wanafunzi wanafagilia sana web yako kaka endelea kuwapagawisha.
ReplyDeleteHuyu askari lazima sheria ichukue mkondo wake. hatuwezi tukaendelea kulea wanajeshi wasiojua majukumu yao na mipaka yao. Mkuu wa jeshi hivi yupo awe na yeye anafagilia tabia hizi?
ReplyDeletewananchi wanatakiwa kulaumiwa kwanza. wanawafagilia sana. jaani wanawaunga mkono kila wakifanya hivi. jambo hili likifanywa na askari wa jeshi lingine wananchi watapiga kelele sana lakini kwa askari wa jeshi la wananchi watu huona ni haki yao kufanya hivyo. hawa hata wakiua utasikia duh niliingia anga zao. tubadilike.
ReplyDeleteWadau huyo askari inaelekea hajui sheria, serikali na kambi ya jeshi hapo tupieni jicho
ReplyDeletedah!
ReplyDeleteafande nuksi sana huyo. Je angepigwa pasi ingekuweje? Hiyo haina tofauti na alichokifanya brother Dittopile.
Asubiri atakiona, machozi ya watu na masikitiko ya wadau na lawama zote za wananchi walioshuhudiwa ni kama laana kwa huyo askari.
jshi la wananchi wa tanzania, nchi yenye utulivu kama maji mtungini, amani tele na maisha bora. ndo maana nikirudi bongo naenda zangu kijijini, huko serikali ni mtendaji,hayo manyanyaso huko hakuna,watu watakuwa walipita ,wenye nyazifa zao, nani aseme wakati nchi imejaa wabinafsi, chukua chako mapema, kama hakikuhusu achana nacho.
ReplyDeleteKwa hilo hata sishangai, kwani yalikwishanikuta enzi hizo Mheshimiwa Mrema Waziri wa Mambo ya Ndani, wala sitaki kuhadithia, but ninachoteka kusema ni kwamba, kiburi hiki cha kijuba wanakipata kutokana na ufala na ubazazi wa watanzania wenyewe, ujinga, kuabudu vyombo vya dola na kutokuwa na fikra ya kutokubali kunyanyaswa, kunyongeshwa na kudunishwa. Lazima miafande hiyo ipate kiburi aroo kwani inaogopewa hairipi nauri. Tena cha ajabu hiyo miafande yenyewe mingine hata kusoma haijui. Siku moja jamaa mmoja aliulizwa na riafande rimoja unafanya wapi kazi, akajibu Uwanja wa Taifa, toa kitamburisho. alipotoa akikitazama kilikuwa kiamdikwa kwa kiingereza, akamwambia mwenzake, angaria hili nimeriuliza rinafanya wapi kazi rikasema uwanja wa taifa, rakini nimesoma kitamburisho chake kimeandikwa National Stadium (NESHINO SITADIUM kwa lahaja yake)
ReplyDeletehao ni wenyewe kwa kunyanyasa.
hamna afande hana kosa hata kidogo awamadereva nao wamezidi kutulowesha siku za mvua bwana acha amuogeshe sawa kabisa afandemtu anapitisha mgari wake resi wakati kuna mimaji
ReplyDeleteTanzania mnyonge hana haki. Ikiwa kila mtu atachukuwa sheria mkononi mwake itakuwaje tanzania? huyo jamaa wa jeshi imetumia nguvu za sare yake kinyume cha sheria, hakuna mtu anaeruhusiwa kuchukuwa sheria mkononi mwake. kwa ufupi huyo askari ameidhalilisha sare alovaa, amelidhalilisha jeshi na kulitia aibu, anafaa kuadhibiwa kabisa. ah nimesahu haya yametokea tanzania, jeshi na polisi wao wanaona nchi ni yao na wanafanya watakavyo na hakuna wa kuwaadhibu. atapongezwa na wengi. waandishi wa habari hebu itambazeni hii stori kwenye vyombo vyenu na mtasikia ya kawaida. "uchunguzwi unafanywa na adhanbu kali itachukuliwa endapo akigundulikana ni mkosa" baada ya hapo kesi ni mkobani.!!!!
ReplyDeleteHi si haki kabisaaaaaaaaa nyie wanajeshi hebu kuweni na ubinadamu
ReplyDeletewhaaaaaaaaaaaaaaaaaaat?
ReplyDeleteati anamwogesha raia katika dimbwi?
who the hell is that mjeshi?
wee ngoja,me ndo mana siipendi iyo taaluma sijui kazi,,,ata kama mnafundishwa kumuua adui sio raia ati kiatu chake
Eti ni askari wa ulinzi wa wananchi!
ReplyDeleteJamani,kupiga kwata isiwe sababu ya kuonea watu wa sekta nyingine. Nishashuhudia kondakta akichapwa bakora na Afande,Makongo, saa 8 mchana. Kama vp itabidi wote tujiunge na jeshi.
ReplyDeleteJAMNI MADEREVA HUSUSANI NJIA YA KAWE TUWE MAKINI ASUBUHI WAJOMBA WANA HASIRA WENGINE HAWAJAPEWA UNYUMBA VIZURI AU BASI WAMEGOMBANA NA WAO WA UBANI BASI KIATU KINAFANYWA ISSUE WANADAMU WABAYA SOME TIME POLE NDUGU,TEH TEH SHUKURU MUNGU ILA USIMIND,KUNA SIKU NILIKUTA WANAMGALAGAZA MSHKAJI KWA STAILI YA KUMBILINGISHA KWENYE MAVUMBI NA HUKU AKIWA AMESHIKA NYETI ZAKE ,ILA HUU UONEVU HAUKUBALIKI SASA HAPO CHUKUA DEMU WAO UONE MOTO WAKE ,MKIWA BAR UTASIKIA AISEE KIRA DEMU NI MWANAJESHI MARWA ANGARIA RAIA WASITONGOZE WANAWAKE WETU TUTWABIRINGISHA KAMA PIPA WAIONE NCHI CHUNGU KMA KICHURI, TEH TEH
ReplyDeleteKISIJU UTAJIJU,
LAMU KUTAMU,
wanajeshi wetu hawajui kwamba yeye pia ni raia kama raia ,wengine na jeshi ni kibarua tu, cha kumpatia riziki yeye na familia yake halafu wengi ni ngumbaru yaani shule hamna hawajui haki za binadamu,na utawala wa sheria kama aliona hilo ni kosa kwa nini aisende polisi,kweli nachukua uraia huku nilipo bongo balaa.
ReplyDeleteMasikini dereva hakujua haki zake alichotakiwa kufanya ni kumuomba tu msamaha and that is it. Afande asingeweza kumfanya chochote zaidi ya hapo. Hata polisi hawaruhusiwi kufanya vitendo kama hivi. Mambo yote yanatakiwa kuishia mahakamani ambapo hukumu ndio inatolewa. Hii ni aina ya kesi ambapo dereva angeweza kulipwa mamilioni ya fidia anachotakiwa kufanya ni kusue hilo jeshi. Kama kweli sheria za TZ zinafanya kazi vizuri tafuta mwanasheria mzuri mnakubaliana malipo utakayopata naye atalipwa gharama zake halafu sue Jeshi.
ReplyDeleteMichuzi unapendelea sana comment ukiona comment zinamponda mwanajeshi huweki kabisa narudia tena huyu mjeshi AWEKWE KWENYE MAGAZETI AULIZWE NI NANI? anaye mjuwa aseme sababu kajichukulia hatuwa ASHITAKIWE AU AFUKUZWE KAZI YAKE jeshi la wananchi ni lakutizama wananchi sio kupiga wananchi. Dereva kweli anakosa ila wewe mwanajeshi mzima sheria unajuwa unakuwa kama hukusoma au ndio unampima kama mwenzako anajuwak uogelea Ili aende mito ya IRaqi?
ReplyDeleteHalafu hili si ndiyo lile eneo waliloandika "USIPIGE PICHA ENEO LA JESHI" Kumbe wanazuia mambo kama haya, na wewe mdau aliechukua hii inaoneka ulikuwa na woga ndiyo maana image imekuwa blured, angekuona na wewe ungeogelea kwenye dimbwi.
ReplyDeleteKweli sheria hakuna Bongo, Huyu anatoa amri wananchi wajichukulie sheria mikononi kwa kuuwa watuhumiwa wa Albino na huyu ajimuogesha mtu kwenye maji machafu akiwa infected hopsital hakuna dawa.
Yaani bongo ni "LAW OF THE JUNGLE, STRUGGLE FOR EXISTANCE SURVIVAL FOR THE FITTEST" Mkubwa kumla mdogo ndiyo mwendo
CHA AJABU NI NINI HAPO? ANAMWADHIBU MKOSAJI KWA MUJIBU WA SHERIA ZA JESHI, UKIWA KWENYE HIMAYA YA KIJESHI UKIFANYA KOSA DOGO UNAADHIBIWA KIJESHI FASTA AND LIFE GOES ON! MNASHANGAA NINI SASA KAMA SI UNAFIKI WENU TU.OOH JESHI VILE MARA JESHI HIVI
ReplyDeletekWENYE JESHI KUNA SHERIA MBILI TU UNAZOTAKIWA KUZIFUATA
1. MKUBWA HAKOSEI
2. ENDAPO UTAONA MKUBWA WAKO KAKOSEA REJEA NAMBA 1 HAPO JUU.
HABARI NDIYO HIYO
Imagine hilo jambo lingetokea hapa Europe ama USA,aliye garagazwa chini ni mweusi nawaapia all hell broke loose.Kwa kuwa mmatumbi kwa mmatumbi story inaishia hapo hapo.
ReplyDeletePoleni sana.
Ex TZ
Mh Michuzi, lelooooooo! unahabari kwamba Baba wa huyo mjeshi kaona picha yake kwenye blog yako kasema akikukamata utaogea Sabuni"MBUNI" mche mzima, Mjeshi pia kasema Kisoda Ndio itakuwa kuchotea maji na kikombe kimoja ndio ndoo yako, ila Mche wa sabuni uishe na utakate maji yasiishe kasema hii picha itowe haraka sana kabla azabu juu ya hiyo nyengine isikukute kakupa Siku 1 tu. nimekumbuka kengine kasema au Atakuvalisha Jezi ya Manchester United juu mpaka chini Sox kwa muda wa week uzunguke nayo Mji mzima huku unaimba mie man u fan. hahaha Habari ndio hiyo.From Mgambo
ReplyDeleteMichuzi we si unafanya daily news? Mfatilieni huyu mjeshi asimamishwe kazi halafu akajibu kesi mahakamani
ReplyDeletehawezi kuwa judge, jury and prosecutor at the same time, that is totally against the law! where is WAZIRI WA ULINZI? Is this the mission you assigned your troops to the citizens? If not why are you quite? I have seen this same picture on different blogs now which means kuna mtu mwenye power kuliko huyu mwanajeshi anayemnyanyasa raia kishaziona
Hii sio aibu kwa jeshi kweli? kwa watu wanaojua haki zao this is illegal and should not be left unpunished!!!!
//// Utawala wa sheria haupo ////
ReplyDeleteHili ni mafano mmoja. Kuna stori za wanajeshi kuwapiga wananchi kitingoji kizima mikanda na mabuti.
Habari za wanajeshi kuwapiga wafanyakazi wa DAWASCO baada ya kukata maji pale JWTZ ilipokuwa hijalipa ankara zake kwa muda mrefu.
Hapa Dar kwa wananchi wa KAWE(calico), Kunduchi, Kigamboni (maji) , kwa Azizi Ally (twalipo) na Minazi Mirefu (Ea-wingi) hula vipigo kila mwezi kwa sababu mbali mbali.
Sasa uje visa vya mgambo kuwakandamiza 'mama ntilie' na chingaz .. utalia hata utakaukiwa na michozi kwa huruma.
Watumishi wengine kama wa TPS hufanya ubabe dhidi ya wenye magari kwakandamiza ile mbaya. Trafic nao huwafanya madereva kuwa ni mashamba yao.
Nchi hii hata wapiga debe wa daladala wanajifanyai jeuri ya kulazimisha wenye dala dala kuwalipa fedha kila kituo.
Nchi isio na mfumo wa utawala wa sheria huwa mdhulumiwa huonekana mkosaji.
Sasa hata mahakama huhitaji mabilioni kama dhamana. Ikiwa mafisadi weney utajiri wanashindwa kupata haki ya dhamana itakuwaje mimi na wewe?
miningemwendea kwa babu maana hamna pakushtaki,dawa kuwaroga tu ningempa ugonjwa usioeleweka.Ndo wajue watu wengine hawaonewi bure.
ReplyDeleteHii imenikumbusha nilipokuwa JKT, mwaka 1973. Ukimkorofisha afande namna hii, lazima ushikishwe adabu, Hakuna kitu cha ajabu hapo. Huyu jamaa kwenye bwawa hatakufa, na afande anajua hivyo, ila huenda akajifunza nidhamu. Mambo ya kiraia ndio yanayotuharibia nchi yetu. Nafurahi kuona sasa tunaye rais ambaye ni afande na ameanza kidogo kidogo kuwatia nidhamu hao mafisadi. Kumbukeni, mambo ya uraia huko huko uraiani. Mkiwachokoza maafande, mtaogelea kwenye bwawa kama huyu njemba hapo juu.
ReplyDeleteHalafu, sana sana sisi tunaona tu hiyo picha hapo juu. Hatujui, pengine huyu jamaa alimpa askari maneno ya jeuri? Madereva wetu tunawafahamu sana. Mwacheni aogelee.
Madereva wa Bongo wahuni wanasitahili kuadhibiwa. Watu wanasema eti oh ingekuwa Ulaya, USA....! Hata sisi Ulaya tumekaa, na maboksi tukabeba. Tulipopata mtaji tukarudi Bongo. Dereva gani USA, Europe....ataona dimbwi la maji na kuna wenda kwa miguu pembeni halafu analiingia kwa fujo? Ukiona kuna watu na madimbwi wakati unaendesha, unapunguza mwendo. Sasa madereva wetu hapo ndo kwanza wanakanyaga mafuta. Wametufanya kama wanyama mjini, tukiwaona wanakuja inabidi tuwakimbie! Udereva gani huo? Mimi ningekuwa mwanajeshi pia ningewa-Ditopile tu hawa wahuni.
ReplyDeleteHIYO PICHA NI USHAHIDI TOSHA WA KUMFUKUZISHA KAZI NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI, DEREVE AENDE POLISI NA KWA MBUNGE WAKE HUYU MJESHI NI MJINGA NA MBUMBUMBU, HIYO KITU IPELEKWE BUNGENI, NDIYO KAZI YA BUNGE HIYO.
ReplyDeletehapo sina comment kwani haya mambo si leo wala jana ni mambo ambayo yapo kila siku katika maeneo ya majeshi yetu,nadhani mifumo yetu ya utawala in mapungufu toka uhuru.kwa tanzania ukiwa mkubwa tu basi uko juu ya sheria,nampa pole sana driver tena ashukuru hata anaogeshwa maji,angepelekwa kunako kambi ndo angejua mwita ni nani na baba yake marwa ni nani
ReplyDeleteMadereva hawa mnawatetea bure tu,mara nyingi wanawamwagia maji watu kwa makusudi hasimami na anajua hutampata-msitetee ujinga!
ReplyDeleteHilo ni eneo la jeshi na meengi yana mabango ila wabongo viburi,waache watupe mkong'oto tu
Duu!!! Madereva wa Dala dala muwe waangalifu maana ni maeneo hayo hayo marehemu Uncle Nanihii 'alimrestisha in pisi' dereva mwenzenu!!
ReplyDeleteTatizo kesi kama hizo wanasheria wa bongo hawazitaki wote wamekimbilia kesi za EPAAAAAAAAAA!!
ReplyDeleteHUO MFANO NDIO TUNAITA "MODERN SLAVERY" watanzania wengi tunaishi kama modern slaves sema watu hawakubali hali halisi tu.
ReplyDeletemdau msema kweli.
Ni kitu cha kusikitisha sana hawa wanajeshi wetu kujiona wao wako juu ya sheria (zaidi) Huyu mjeshi achukuliwe hatua za kisheria, huyo aliyemgaragaza kwenye maji machafu ni binadamu kama yeye thamani ya huyo dereva haiwezi kulinganishwa na hicho kiatu chake kinachokanyaga kinyesi kila wakati. Basi atoe adhabu kwa Mungu aliyeleta mvua, serikali ambayo haijatengeneza hiyo barabara, na aliyemnyima pesa ya kununulia gari. Huo si ubinadamu wala uungwana, Mjeshi anatakiwa apewe adhabu kwa kumdhalilisha dereva huyo. We mjeshi usifikiri ni sifa kuwanyanyasa raia unatakiwa uwe umstari wa mbele kulinda raia na siyo kuwanyanyasa!!!!!!
ReplyDeleteAfrika ni Afrika tu, kuoneana ni kitu cha kawaida. Nilipokuwa Ubalozi wa Marekani, alikuja Mwanajeshi na uniform yake kubwa tu na kila aina ya nyota begani. Jamaa alifikiri atamtisha mtu pale, mwanae kanyimwa viza mbele yangu, kabaki kuduwaa na uchozi. Nilicheka sana, wamezoea kuwanyanyasa wananchi na vyeo vyao, wanafikiri wako juu ya sheria. nashukuru siwaoni tena wadudu hawa ughaibuni.
ReplyDelete