mama salma akipanda mti wake
JK akimwagilia maji mti alioupanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kila mwaka ya upandaji miti iliyofanyka kitaifa eneo la Bendera Tatu,Temeke jijini Dar leo. picha na mdau Freddy Maro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. TUJITAHIDI KUPANDA MITI NA KUITUNZA KUZUNGUNGA NYUMBA ZETU NA BARABARANI ILI KUPATA HEWA SAFI, KUFUTA MVUA, VIVULI NA KUPENDEZESHA MANDHARI KAMA VILE KWA WENZETU WALIVYO HUWA INAPENDEZA. TUSIKATE MITI WALA VICHAKA TUVIACHE VILIVYO TUVITUNZE TU.

    ReplyDelete
  2. kama ni kampeni ni kupanda miti, mbona rais Huo anaopanda siyo mti. LABDA TUSEME NI KAMPENI YA KUPANDA MIMEA

    ReplyDelete
  3. Huu sio msimu wa upandaji miti, kwa kawaida msimu huu huanzia katikati ya mwezi wa 3 au mwezi wa 11 hiki ndio kipindi ambacho kina mvua za kutosha, hiyo iliyopandwa utakaopona ni mmoja tu alioupanda mheshimiwa kwa sababu wataumwagilia na boza la maji hadi ushike, hiyo mingine itakufa yote

    ReplyDelete
  4. naunga mkono kampeni ya kupanda miti. wananchi haswa wa vijijini wahamasishwe kupanda miti ili kuzuia kuenea kwa jangwa.

    ReplyDelete
  5. ninashukuru kumuona rais wetu anapanda miti. hili ni jambo zuri sana. watanzania ni lazima tupande miti. kwanini miji yetu hatutengi sehemu za parks. wazee wa miji kazi yao ni kugawa viwanja vya kujenga nyumba peke yake lakini hawaweki aside sehemu za parks. baba yangu ananiambia wakati wa ukoloni kulikua na miti mbele ya karibu kila nymba lakini ikakatwa yote. pengine tungepanda mingine. tafadhali serikali angalieni ile sehemu kati ya longido na oldonyo sambu mkoani arusha kunageuka jangwa.

    ReplyDelete
  6. weee annon wasema longido tu??yan nilipoenda iringa km miaka mitano ilopita nilikataa kbs sio iringa,yan jangwaaaa no miti kabisa kule miliman yan kukame adi balaa,jaman izi ngozi zingine na akili finyu??
    yan hakufai mchana ilo joto na jua,no upepo at all,dar ndo usiseme yan mtu anapojenga anakata miti yooote around asafisha kama barazan wee wafikilia nini??dar hakufai kwa mvuke la joto na jua adi niliugua,hutembei mchana,asa pale mliman city ndo walinshangaza kabisaaa yan na "uzungu" wote ule wa malls hakuna kivuli hata kidgo nje no miti zaidi ya vile vimtende sijui!!!aaggh so stupid yan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...