Toka shoto ni mjane wa marehemu Millinga bibi Conrada Millinga, mwalimu mkuu wa shule ya RDA, iliyoasisiwa na kuendeshwa kijamaa bw. Suleman Toroka. Kati ni naibu balozi wa Tanzania nchini uingereza Mh. Chabaka Kilumanga akifuatiwa na mwanaharakati Selma James na Apollo Temu
Hii ni katika hafla ya kumuenzi muasisi wa Ruvuma Development Association (RDA) ndugu Ntimbanjayo Millinga. kwenye miaka ya 1960 RDA ilijaribu na kufanikiwa kuyaweka katika vitendo mawazo ya Ujamaa ya baba wa Taifa julius Nyerere.

Hadhara hiyo ilifanyika ukumbi wa Boliva wa ubalozi wa Venezuela nchini Uingereza, Grafton way, London. iliandaliwa na Global women strike.

Conrada millinga (kulia) ambaye alitoa mada kuhusu nafasi ya wanawake kwenye RDA katika hadhara hiyo akiwa na mwanaharakati bibi selma James pamoja na wanaharakati wengine waliohudhuria.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ooh my uncle John Ntimbanjoyo Millinga, I am missing you, I am missing, so badly. I am glad to see you're still honored. Aunt Conrada I am proud of you, stay focus and be blessed always. Mpwao from Arkansas Feyettiville, US.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...