Ndugu wanachama wote wa CCM na Watanzania wote Manchester mnaalikwa kwenye sherehe ya kuzaliwa CCM tarehe 5 mwezi wa 2, ambayo itafanyika tarehe 07.02.09 kuanzia saa 12 jioni kwenye ukumbi wa
115 Hertford Rd,
Edmonton,
London,
N 9 7EN.
Kiingilio bure,
vinywaji na chakula vitatolewa bure pia.
Karibuni sana.
Uongozi CCM Manchester

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Makachero SFO wabaini maovu mapya ya Chenge

    2009-02-03 10:26:30
    Na Mwandshi Wetu


    Matata mapya yamemkuta Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, baada ya uchunguzi wa makachero wa Uingereza wa Kitengo cha Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) kugundua kwamba mwanasiasa huyo, hakuwahi kutaja katika fomu zake za kutangaza mali kwa Kamishna wa Maadili, kiasi cha Dola za Marekani milioni 1.5 alizokuwa ameweka kwenye akaunti yake kisiwani New Jersey.

    Taarifa za uhakika ambazo Nipashe imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika, SFO wanaochunguza rushwa katika ununuzi wa rada ya Tanzania iliyonunuliwa kwa bei ya Dola za Marekani milioni 40 na kiasi cha Dola milioni 12 (zaidi ya Sh bilioni 15) kutolewa kama rushwa ili kufanikisha ununuzi huo, wanashauri Chenge ashitakiwe.

    Vyanzo vya uhakika vya habari kutoka SFO vinasema kwamba hakuna wakati wowote ambao Chenge, wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alitangaza kumiliki fedha hizo katika akaunti hiyo ughaibuni.

    Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

    Kwa taarifa hizi mpya, SFO wamependekeza kwamba Chenge anaweza kufunguliwa mashitaka ya jinai kwa sababu ya kudanganya chini ya kiapo.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi, kila mwaka kiongozi anayekalia ofisi ya umma anawajibika kujaza fomu maalum ya kueleza mali zake na mkewe pamoja na za watoto walio chini ya miaka 18, pia anawajibika kutangaza madeni yake kwenye fomu hiyo.

    Akizungumzia utaratibu wa kujaza fomu ya kutangaza mali, Wakili wa kujitegemea, Mabere Marando, alisema kwamba kama mtu akithibitika amesema uongo chini ya kiapo ni kosa la jinai ambapo adhabu yake ni kufungwa na faini.

    ``Kwa sasa sina uhakika ni kifungo cha miaka mingapi, lakini hilo ni kosa la jinai, hivyo adhabu yake ni kufungwa,`` alisema Marando

    Naye wakili wa kujitegemea wa Mahakama Kuu, Juvenalis Ngowi, alisema kwamba ni kosa la jinai kusema uongo chini ya kiapo.

    ``Jambo lolote ambalo unafanya chini ya kiapo, lazima useme ukweli. Usipofanya hivyo unakuwa umetenda kosa la jinai ambapo ni kufungwa,`` alisema Ngowi.

    Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, kiongozi wa umma ambaye chini ya kifungu cha 22 na 23 akijua kwamba anatoa taarifa za uongo atakuwa anatenda kosa baada ya kuthibitika ambalo adhabu yake si chini ya Sh 200,000 na kiasi kisichozidi Sh milioni moja au kufungwa jela kwa kipindi kisichozidi miaka miwili.

    Uchunguzi wa SFO unaonyesha kwamba Chenge akiwa kiongozi wa umma hakuwahi kusema anamiliki kiasi hicho cha fedha katika akaunti yake, na hata alipohojiwa juu ya fedha hizo alitoa majibu ya kukinzana.

    Awali alisema fedha hizo ni malipo kwa ajili ya huduma ya kisheria aliyokuwa anatoa, lakini mara ya pili alibadili maneno na kusema kwamba zilitokana na akiba ya familia yake pamoja na urithi, pia alieleza kwamba asilimia 25 ya fedha hizo ni mali ya mkewe.

    Chenge andaiwa na SFO kuwa mtu muhimu wakati wa mchakato wa ununuzi wa rada ya Tanzania, kwa sababu alitakiwa atoe ushauri wake wa kisheria kwa serikali.

    Bila yeye mpango mzima wa ununuzi usingefanikiwa.

    Kulingana na vyanzo vya habari, hata kama Chenge ataweza kuthibitisha vyanzo halali vya fedha alizochimbia New Jersey kwenye akaunti ya benki ya Barclays, bado atakuwa na kesi ya kujibu kwa kudanganya chini ya kiapo.

    Chenge alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Miundombinu Aprili mwaka jana, kutokana na kuwa chini ya uchunguzi wa SFO, akituhumiwa kwamba fedha alizojiwekea New Jersey zilitokana na mgawo wa rushwa ya ununuzi wa rada. Chenge amekanusha kuchukua rushwa.

    Ununuzi wa rada hiyo ulisababisha mvutano mkubwa baina ya mawaziri wa serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, hali iliyomlazimu aliyekuwa Waziri wa Misaada ya Maendeleo, Claire Short, kuhitilafiana na serikali na mwishowe alijiuzu.

    Short alisema ingawa hakuwa na ushahidi mahususi, ununuzi wa rada ya Tanzania kutoka kampuni ya kuuza vifaa vya kijeshi ya Uingereza, BAE System, ulikuwa umegubikwa na rushwa.

    Kabla ya rada hiyo kununuliwa, kuliibuka mjadala mkali nchini, wengi wakipinga kwa sababu ilikuwa ina gharimu pesa nyingi wakati Tanzania ingeweza kupata rada mbadala kwingineko kwa gharama chini ya nusu ya hiyo.

    Hata hivyo, serikali ya awamu ya Tatu ya Rais Benjamini Mkapa ilisisitiza kununuliwa kwa rada hiyo.

    Hii ni mara ya kwanza taarifa za Chenge kudanganya chini ya kiapo zinafichuliwa, zikifuatia habari za kina zilizoandikwa na gazeti dada la The Guardian on Sunday wiki iliyopita jinsi Chenge alivyolipwa mabilioni kwenye akaunti yake namba 59662999 inayomilikiwa na kampuni ya Franton Investment Limited.

    SOURCE: nipashe


    sasa wadau hapo mnasemaje? kwanza tusifocus sana kwenye kosa la kudanganya chini ya kiapo manake nishaona hapo juu ni kifungo cha miaka miwili tu.kosa kubwa la rushwa aliokula hio na uthibitisho ndio huo sasa je CHENGE ATAFUNGWA AU HAPANA?
    mdau "cha mtu mavi"

    ReplyDelete
  2. INAKAAJE HII! WATU WA MANCHESTER WAKALE SHEREHE ZA CCM LONDON? KWA NINI MSIFANYIE HUKO HUKO MANCHESTER

    ReplyDelete
  3. Tawi tufungue Manchester sherehe London. VP nyie?

    ReplyDelete
  4. Ufanunuzi ni kwamba imechaguliwa sehemu moja kuwa mwenyeji wa sherehe hiyo. kwa hiyo watu wote kwa mfano Birmngham, Reading na kote UK watakuwepo siku hiyo. Nafikiri nimejibu maswali yenu ngdu Zangu

    ReplyDelete
  5. Sherehe ni London, kusheherekea Birthday nyingine ya Chama cha Mapinduzi Taifa.

    Hii ni sherehe ya wana CCM na Watanzania wote walishio Uingereza, siyo sherehe ya Shina.

    Wote Mnakaribishwa

    ReplyDelete
  6. annon wa kwanza,,,mpe michu apost apo barazani hii newz,,,
    ccm ndo kituko gani???

    ReplyDelete
  7. michuzi muoga hawezi kupost kitu kama hicho juu anajua hoja nzito hio japokuwa ina source tayari.wewe si unaona makada wa ccm walivyoiruka wanafanya kama hawaioni wame focus kwenye party ya london lool.

    ReplyDelete
  8. MTOWA RUSHWA NA MPOKEAJI WOTE WANA MAKOSA. NI MCEZO WA MAKAMPUNI MENGI A NCHI ZA MAGHARIBI KUTOWA RUSHWA HASA UK NA USA NI HODARI WA RUSHWA HASA HI BAE NI YENYEWE KWA RUSHWA ILITOWA RUSHWA KUUZA NDEGE ZA KIVITA SAUDI ARABIA HAO HAO SFO WALIJARIBU KUFUATILIA NA WABUNGE KUPIGA KALELE WASAUDI WAKAWAWEKEA MKWARA KAMA MTAENDELEA KUPIGA KELELE BASI TUTAACHA USHIRIKIANO NANYI KWENYE VITA YA MAGAIDI UK WAKAFYATA MKIA. TANZANIA NCHI MASIKINI BASI NDO HAYO TENA, HAWA WATU NI WABAYE NA NDUMILA KUWILI.

    ReplyDelete
  9. Manchester mpaka London kisa sherehe ya CCM! mna kazi wanachama wa CCM... umewachukulia B&B? Poleni wana CCM wa Manchester...

    ReplyDelete
  10. yani ntajiunga tu CCM naona nna vision kuwa kiongozi,,,sii mchezo mnavojilusha adi London??????????
    chama letu lidumuuuuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...