salamaleko!
mie bwana napenda kwanza kuwasifu kinamama na kinadada kwa unadhifu wa kupiga pamba pamoja na kubeba mabegi yanayopendeza.
sasa swali langu ni je kinamama na kinadada huwa wanaweka nini kwenye mabegi hayo ambayo mengine huonekana makubwa na yamesheheni?
samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu, kwani kuuliza si ujinga...
Mdau Mikindani


Khanga ni muhimu mno ktk pochi/mkoba wa mwanamke. Maana zipu yaweza kutatuka au kuharibika wakati wowote. Pia ni uamuzi wa mtu kubeba apendacho ktk pochi/mkoba wake. Wengine wanabeba vipodozi pia.
ReplyDeletehandbags ni urembo tu kakayetu,ukivaa ukipendeza handbag na yenyewe inaongeza nakshi kama mwanamke,ndani hakuna cha maana zaidi ya walet na poda kidogo,na kina mama wenye watoto basi huweka kama chupa za maziwa na diapers na wipes na vitu kama hivyo,ila iwe kubwa au ndogo zote ni kuongeza nakshi ya udada tu
ReplyDelete1) Always (Kama yuko kwenye nanihii)
ReplyDelete2) Kibanio Cha Nywele
3) Make Up
4) Wanja
5) Kioo Cha Kujiangalia
6) Kitana
7) Mtandio
8) Lip Stick
9) Ndomu (Kama wa Kujirusha)
10) Pesa
11) Wigi
12) Wallet (hata kama haina kitu)
13) N. k
Swali zuri sana...nakushauri ukamuulize mamako mzazi
ReplyDeleteKAMA SEHEMU ULOTOKA "mikindani"
ReplyDeleteso yanakuhusu nini wewe na mipochi yetu ndani?huna mke/girlfriend etc?
anyway uwa tunabeba condoms na pills na vyupi vya kubadilisha
unauliza ili iweje? chungulia ya mkeo ndo ujue
ReplyDeleteSwali zuri sana mdau, humo huwa tunabeba vitu kama mafuta ya kupka labda baada ya kazi na poda, mda mwingine naweza kupita madukani nkanunua hata nguo nikaweka humo, au naweza kubeba viatu vya kubadilisha kama nimechoka kuvaa vyenye kisigino, hopefull umeelewa.
ReplyDeletespea nmtu wangu ukipenda zana siunajua ziletarehe zao some times zinakuja ghafla sa ikiwa hivyo anakula kona sehemu anrekebisha mwendo mdundo pia na vipodozi wengine viwalo vya kubadili kwenda kuwaibia watu
ReplyDeleteHumu tunaweka kila kitu kuanzia vipodozi, perfume, pesa, cm, na vingine vya sirini!
ReplyDeletevitu vya kujisafisha chini, perfume, deodorant kama ikihitajika, mipira ili tusipatwe magonjwa tukinaniii. unajua tena hasa sie tulio na vijiboyfriend hatuishi nao nyumba moja hatuwaamini,diary, peni etc
ReplyDeleteulishaga uliza ndugu zako wa kike wanaweka nini?
mara nyingi ni vipodozi.na wengine wanabeba tu km "fasheni"coz mwanamke handbag kaka..
ReplyDeletesome keep confidentials coz anythin can happen..
We mdau sijui mtumbwi, kwani huna dada au shangazi, siwende ukawaulize wanaweka nini kwenye mabegi yao...!
ReplyDeleteUwe unakuwa mwili na akili, acha utoto....!
swali zuri kakangu, si akina mama tuna mambo mengi wakati mwingine. humo usishangae ukakuta vipodozi, nguo za emergency kwani wakati mwingine mambo uharibikia njiani. ndo vinavyojaza mikoba yetu.
ReplyDeleteMambo kibao. Karatasi za usafi, kalamu, pochi, funguo, nguo za ndani, condoms, etc. Wanawake wako tayari kwa libeneke wakati wowote. Huwezi kutabiri mtanange utaibukia wapi. Ni bora kuwa tayari kwa lolote....lol!
ReplyDeleteMzee wa maishuz
mimi ni mdada mimi nina hand bag ndogo naweka
ReplyDelete1 .wallet
2 .simu
3 .ch**i
4 .P**i
5 .pen
6 note book
7kama kuna joto chupa ndogo ya maji
8 dawa mfano "panadol"
9 bibilia ndogo
Kama una rafiki wa kike au dada watakupa jibu sahihi ila hapa unatafuta lawama tu mshikaji wangu. lol
ReplyDeleteMdau mikindani mimi kama mwanamke nakujibu kuwa mabegi ya akina mama yanabeba mambo mengi sana mengine ya siri sana unavyojua mwanamke any time mambo yanaweza kumribikia halafu cha kujisitili kikawa kiko mbali lakini anapokuwa na hand bag yake mkononi ni kama mwanajeshi au polisi hasau silaha yake anapokwenda vitani na lapili huenda tunaweka khanga kwa ajili ya kwenda msibani ukisikia tu taarifa za msiba upo tayari kwenda kama una kuhusu kwa vile huna haja tena ya kurudi nyumbani kama utakuwa ofisi au sehemi nyingine,na latatu mdau tunaweka vitu kama lipstic,make up set unajua tena mwanamke kupendeza muda wote uso unatakiwa ung'ale pia perfumu lazima iwepo ndani ya hand bag kwani mwanamke mazingira si kunuka kikwapa,powder na pesa na mambo mengine mengi yahusiyo kuwekw ndani ya handbag kubwa kama hiyo
ReplyDeleteswali lako zuri sana, ila nafikili ungeanzia kwenu kuuliza swali hilo kama una mama au dada.
ReplyDeletemimi huwa naweka salama,mafuta uzuri,mswaki,chupi ya spea,n.k sijuwi dada zako wanabeba nini waulize utapata jibu.
Inaonekana wewe mdau hujaoa au huna hata girl friend. Akina dada na akina mama wana mambo mengi sana. Kwanza anatakiwa awe na vitambaa vya kujifutia jasho zaidi ya kimoja, awe walau na toilet paper, awe na pedi ya dharula, awe na perfume, awe na mafuta na kioo kidogo, awe na lipstick, awe pia na kipochi kama wallet hivi kinachokuwa kimewekewa nyaraka zake kama kadi ya benki, kitambulisho, n.k. kwenye hiyo wallet ndiyo anaweka hata simu yake ya mkononi. Pia akina mama wanajipenda sana unaweza kumkuta mwingine ameweka huko hata juice chupa ndogo, biscuits, big G na vitu vingine vidogovidogo. Hivi vyote kwa wewe mwanaume havihitajiki. Nadhani umepata tafsiri ya kwa nini wanakuwa na mabegi saa zote kama anavyoonekana mama huyo kwenye picha.
ReplyDeleteMdau
hahaa swali limenifurahisha sana, mi najua watu ambao huweka vitu kama khanga just in case ikhitajika mahali, lakini wengine wana hobby tu ya pochi kubwa zinawafurahisha hivyo lazima kutafuta kitu cha kuweka ili shape ikae vizuri, kama wanaume wengine wanaovaa viatu vikuuubwa, just a hobby
ReplyDeletema alwayz!!!!
ReplyDeletemmh kweli swali la kizushi, tuna weka mapampazi, loh mmbeya wewe,,,
ReplyDeleteahahaha acha maswali ya kizushi watu wapo kazini..Nondoz zote mhimu zinakuwa humo
ReplyDeleteinategemea kwa wakati huo anakwenda wapi, lakini vipondozi (wanja, rotion, lipgrow/stiki, kioo nk) chanuo, khanga/kitenge/mtandio, notebook, peni, walet hivi ni muhimu kwenye pochi kubwa kama hiyo!
ReplyDeletekuna wengine wanakuwa mpaka na huduma ya kwanza (panadol,plasta) hizo pochi zinabeba vitu vingi sana hapo yupo full!!
jasmin
WANAWEKA VITU VINAVYOHUSIANA NA AKINA MAMA, WEWE KAMA YOU ARE OVER AGE UTANIELEWA NINA MAANA GANI. AKINA MAMA NI WATU WANAOPENDA KUJIHESHIMU NA KUJIHIFADHI VIZURI, HUWEZI JUWA INAWEZA TOKEA AJALI YA AINA YOYOTE ILE THEN WAKAPATA NAMNA AU KITU CHA KUJIHIFADHIA. I HOPE YOU GONNA UNDERSTAND ME.
ReplyDeletekuuliza si ujinga. jibu ni kwamba, mara nyingi unaweza ukaona wameweka vitu kama vile vya kuwasaidia kama wako mwezini, funguo, vipochi vya pesa, leso, kitana wakati mwingine kioo kidogo mafuta madogo nk.
ReplyDeleteakina dada naona leo wagumu kujibu huu uzishi, sasa kwavile mimi nawajuilia vizuri,wengi wa akina dada ni watulivu,lakini ni wepesi wa kukasirika,sasa mimi nawakasirisha kwa kuongeza uzushi ili tupate jibu la haya mabegi ya kwapa yaliyokuwa hayaishi hata kama munakwenda nymba ya pili ya jirani inakuwa manake ni nini,na kama mdau hapo juu anauliza mengine yanakuwa yamesheni ile mbaya yaani,ni nini hasa munaweka ndani yake
ReplyDeletethanks,kubwa la uzushi
Waaalykum msaalam shekhe.......Yaani leo nimecheka sana......Yaani hilo swali lako utani kama unajuwa na mimi kama nilikuwa nalifikiria.
ReplyDeleteNi kweli mkuuu swali lako zuri sana tena sana....Hao wakina dada humo ndani huwa hawaweki kitu kabisa zaidi wanajaza vipodozi na mavitabu ili begi lionekane kubwa wanasema etii wanakwenda na wakati sasa sijui wenzangu wana mawazo gani....Maana sidhani kama vitu alivyoweka humo vinatumika!!
angalia la mkeo utajua kinachowekwa, kama huna muulize mama, dada au jrani yeyote mwanamke atakufahamisha. acha uzushi.
ReplyDeleteKwenye hayo mapochi makubwa wakina dada tunaweka vitu kama hand lotion,money, note book, lipgloss,bottle of water,a book, upande wa kanga, deodorant, manukato etc. kwa hiyo unaona ndugu yangu hiyo tosha kujaza pochi.
ReplyDeleteWhatever! Who is bothered? You?
ReplyDeletehujakosea kabisa,hata mimi nashangaa wanake wenzangu,na mabegi makubwa kama ya dipper.tena sometimes wanakuwa na mabegi makubwa kwenye dance floor ha ha haaaa washamba sana ,utavaaje cocktail dress na begi kubwa kama la diper? kisa fake gucci basi hao wana yabeba kwenye mduwara.
ReplyDeleteangalia la mkeo, kama huna dada yako, kama huna mama yako, kama huna tafuta gf.
ReplyDeletewewe kweli mzushi na unatafuta maneno na sisi wabeba mabegi makubwa kwa hiyo ungeishia hapo na hata sijui kam kuna mtu atakwambia ukweli humu. Ni kwamba hiyo ni siri ya mwenye begi tuu weye wayatakia ni ? mie hapa hata mume wangu huwa hajui naweka nini kwenye mabegi yangu kama anavyosema labda nabeba "vichwa vya watu" mana ukubwa na uzito umezidi .....utajijuuuuu!
ReplyDeleteSwali zuri-wacha nikupashe mdau mikindani. Inategemea na mwanamke anayebeba begi lenyewe. Normally lakini, mle ndani ya pochi kubwa kuna tena ka wallet/kapochi kadogo cha kubeba pesa, kuna various make up kama lip gloss na poda, snacks na labda changing clothes za kwenda kuworkout baadae? It just depends.
ReplyDeleteNi fashion tu. Kama zilivyokuwaga fashion za aina nyingine kama enzi zile suruali za bugaloo,za njiwa style n.k. Kinachobebwa ndani ya pochi nadhani kiwe ni siri ya mbebaji tu. Asante
ReplyDeleteNi fashion tu. Kama zilivyokuwaga fashion za aina nyingine kama enzi zile suruali za bugaloo,za njiwa style n.k. Kinachobebwa ndani ya pochi nadhani kiwe ni siri ya mbebaji tu. Asante
ReplyDeletewaTZ bwana, eti wanasema "Always" wakimaanisha "Visodo". Always ni "Brand Name" kwa Visodo kama vile Jassy, Tups nk.
ReplyDeletekhaaaaa
ReplyDeletemwanaume mmbeya wewe?heee are yu under 16 years au ushazeeka 70's?
iyo ni siri ya binti/mwanamke
dah jamaaa uyu?
hahahaaaaaaa
Kati ya wote binadamu mchafu ni mwanamke.
ReplyDeleteMwanamke ni mchafu sana asipo oga masaa tu unamkimbia,akikojoa asipo safisha nanihii utamkimbia.
Hawa watu wanabeba vichupi vyao vya kubadilisha mara kwa mara pamoja na vipodozi vya kupoteza harufu yao mbaya inayo nuka.
Kama anavuja au yupo angani atabeba vile vifyonza uchafu.
Mwanamke anaye jiheshimu hawezi akabeba condom kwenye bag ukiona kabeba basi huyo siku zote yupo katika bussiness kuwinda mabuzi. Lazima atakuwa hajatulia.
We unayesema wanawake wachafu kumbuka ulitoka tumboni kwa mmoja wao....rekebisha lugha yako maana inakushtaki kama hujaenda shule.
ReplyDeleteNICHOLAS SEMIONI
UK
mama mmoja yeye akiwa na mimba anabeba chupi za mumewe kila wakati ananusa hii akiwa na mimba.
ReplyDeleteTupunguze 'usenene' jamani. Jamaa kauliza tu (kwa niaba ya wengi)tupate fahamu. Sio kila jambo mtu anaweza kumuuliza mamake au dadake! Mawazo na matumizi pia yanatofautiana, kama tulivyoona! Mjukuu wangu aliwahi kuniambia "ni urembo tu babu."
ReplyDeleteDILDOZ.........CONDOMZ.......ALWAYZ..........
ReplyDeleteAkili ni nywele kila mtu ana zake hivyo mdau hakuna kushangaa!
ReplyDeleteLONDON (Reuters) - A milkman who admitted he delivered cannabis as well as pintas to elderly customers to ease their aches and pains, was spared jail on Friday.
Robert Holding, 72, from Burnley, told police he supplied the drug to 17 customers after detectives raided his home and found nearly 6oz (167g) of cannabis in an egg crate in the van he used for deliveries.
"He said he sold the cannabis to existing customers because they were old and had aches and pains," said prosecutor Sarah Statham.
"He said he sold a 9oz (255g) bar about every three weeks and sold it for a relatively cheap value. He said that customers left him notes saying, for example, 'Can I have an ounce this week or can I have an eighth.'
Holding, who admitted supplying and possession of the drug at a previous hearing, was given a 36-month prison sentence suspended for a year at Burnley Crown Court on Friday, the Press Association reported.
Judge Beverley Lunt told him the sentence was "an act of mercy" because he visited his wife, who has Alzheimer's disease, every day in a care home.
"You were not some philanthropist helping out the elderly out of the good of your heart. You dealt drugs for profit in a calculated way. It was a business," the judge told him.
His lawyer Philip Holden said his client "wasn't making much of a profit" and that his oldest client was 92.
"Word had got out that he was a man who could supply cannabis to those of a certain age with aches and pains and he misguidedly believed he was providing a public service," he said.
After the verdict Holding insisted he had not made money from his drug dealing.
"They (the customers) enjoyed it, they saved a lot of money while I was doing it and I only did it for a short time," he said.
However Neil Standage, area crown prosecutor for East Lancashire, said there was no evidence that he was only supplying elderly people with painful ailments.
"This might make it sound like what he was doing was harmless. It wasn't," he said.
Reuters
Sawa akina mama majibu yenu yote ni ya kisasa na mjini, vipi hawa akina mama wa vijijini mbona hawana mabegi makubwa kiasi hicho, sis watoto wa miaka ya 1960, 1970, 1980 hatukuona akina mama zet na dada zetu na mabegi makubwa kiasi hicho! ina maana wao hawakuwa na hali kama zenu? tunaomba jibu sahihi. Kama hawakuwa nazo basi tusingezaliwa, mimi nahisi walikuwanayo, sasa kwa nini hawakubeba mibegi? NAWAKILISHA.
ReplyDeletekakazetu msishangae,pochi iwe kubwa au ndogo zote ni urembo na kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama lipstick,peni,walet,lesso,kanga labda au nguo au viatu vya kubadilisha,kama umevaa high heels then upo ofisini unataka kupumzisha miguu unavaa sandals mpaka muda wa kutoka then unarudia high heels zako au unaenda kwenye party unaweza high heels ndani mpaka ufike ndio unabadilishia na vitu kama brush ya viatu au nywele,
ReplyDeletekina mama ndio tulivyo tunapenda kuwa tarari saa zote kama wanajeshi,pia na vitu kama walet zetu etc,
na kusema pochi kuubwa,hiyo ni style tu,kama style imeingia kubeba pochi kubwa basi unabeba kuvutia tu au kuwa na style yako unique,na pochi ndogo ndogo wanaita clutch ni za night parties unavaa unapendeza huna haja ya begi kubwa unabeba kadogo ndani ni few makeups basi,nadhani sasa mtatuelewa.
kukeep urembo is a big job na nyendo ndio hizo ndani ya mabegi yetu,waswahili wanasema msione vinaelea..ukitaka mkeo ang'ae na kuwa msafi saa zote basi shurti wanja,poda,pedi,kitambaa cha usafi,vya kubadilishia viwemo ndani ya begi hawezi kubeba mkononi ati
kwaheriii
heheheheeee
ReplyDeletewahaya wanasema ka nsheke!!!
humo kwenye mahendbeg yetu ukifanya search utakuta ndani yake kuna vipochi tena kama vi3 hivi.kimoja cha vipodozi vyote muhimu cha pili cha hela na cha tatu cha notebook,kalamu handkerchief na simu.pia na mtandio haukosi,na pedi inakaa kwenye kazipu ka pembeni.na simple shoes kwa ajili ya dharula au ukichoka kutembelea viatu virefu.
na mimi hapa pembeni koba ninalo na ndo hivyo nilivyobeba.
ila sometimez huwa nabeba na laptop kabisa humo.
mzee wa mikindani wa Pemba au? we unashangaa nini/ enzi za mwalimu kule pemba handbags ni mikoba ya ukili/ukindu, sasa leo mkoba wa ngozi unakupa maswali ya nini? sikulaumu kwa kuwa swali lako la kizushi.
ReplyDeleteMzushi wangu, kwanza elewa kuwa mazoea yana tabu , ukiwa unabeba huo mkoba kila siku inafikia mahali huwezi toka na kupunga mkono bila kubebe handbag, yaani unajihisi mwepesi sana, pia inategemea na kila mbebaji wa mkoba huo ana tabia gani au hupenda vitu gani kuwa navyo kila anapokuwa, wengi huwa lazima tuweke vipodozi na pochi ndogo ya kuweka pesa, zaidi ya hapo inategemea aidha simu,spika za masikioni za simu MD kwa wapenzi wa mziki, unakuwa huru kuweka chochote cha kwako unachohitaji iwe contaner ya vitafunwa au kama umepita dukani hapo ndo sisemi huo mrundo wa kila unachopata kinachoweza kuingia humo kinachomekwa. Narudia tunauhuru wa kuweka chochote kutokana na maumbile yetu wanawake na mabadiliko ya hali ya hewa tunakuwa tunajiandaa na kujistiri endapo utapita mda mwingi bila kurudi kujihifadhi nyumbani, hivyo kaka zetu nawasihi msipende sana kufungua au kuchungulia mikoba ya dada zenu mnaweza kumuaibisha bila kukusudia, au unaweza ukakarahika wewe mwenyewe pia.
Hili swali lilikuwa la kizushi lakini la maana,ila kama kawaida ya watoto wa JK imekuwa issue.
ReplyDeleteNimesikitika kuwa katika wote walioyatetea hayo ma begi,hamna aliyesema kuna angalau kitabu au gazeti.Lingine naomba wenye dada wa kizungu au mataifa mengine nao watupe mchango wao,nasikia mle wao hubeba mambo ya ajabu?*?
MIMI MWANAMKE. NA KILA MMOJA WETU TUNATOFAUTIANA. SIO WOTE WANAOBEBA HANDBAGS KUBWA, AU WANAOJAZA VITU. WAPO WANAOBEBA NDOGO NA HAZINA VITU VINGI.NA WAKO WANAOBEBA ZAIDI YA MOJA. MIMI NINAYO MATATU NATEMBEA NAYO KILA SIKU. SIO MAKUBWA NI SAIZI YA KATI.
ReplyDeleteMOJA NABEBA VITU VYOTE MUHIMU, WALLET YA PESA INA KADI ZA BENKI, KITAMBULISHO, BUSINESS CARD, LESENI N.K. PIA INA SIMU, NOTE BOOKS, DIARY, KALAMU,FUNGUO ZA NYUMBANI (CHUMBA CHA KULALA), ZA POSTA, ZA GARI NA ZA OFISINI. LESO, KITANA, KARATASI LAINI, MWAMVULI MDOGO, LIP BALM NA MFUKO WA KUBEBEA VITU VYA DHARURA HASA MBOGAMBOGA NA MATUNDA, NAUKUNJA VIZURI NDANI YA HANDBAG.
JINGINE NABEBEA VITAFUNWA NA CHAKULA KUTOKA NYUMBANI.
MFUKO MWINGINE WA MANUNUZI YA MAHITAJI YA NYUMBANI. HUU HAUTOKI NDANI YA HANDBAG MPAKA NINAPONUNUA VITU HIVYO.
TENA NIKIBEBA HANDBAG PEKE YAKE NAJISIKIA KAMA NIMESAHAU KITU. NIKIWA NIMEBEBA NA FAILI AU LAPTOP NAJISIKIA BURUDANI NA NIKO KAMILI.
mimi hapa ninalo bonge ya handbag swali lako imenifanya nifungue nikuelezee kuna nini labda itakusaidia,
ReplyDeleteEVERYDAY LIFE BIBBLE by JOYCE MEYER
MWAVULI MDOGO
BIG G kama tano hivi
KIPOCHI CHA MAKE UP ZOTE
KIPOCHI CHA PAD
FUNGUO ZA NYUMBA NA GARI
IPOD
CHARGER ZA IPOD,SIMU
FLASH DISK
KIPOCHI KIDOGO CHA INSURANCE CARD NA IDENTITY
SUNGLASSESS
NOTE BOOK NA DIARY
SHAJARA YA KIFRANSISKO 2009
nadhani umepata picha kidogo
Wewe unayesema wanawake wachafu basi temea mate chini maana kila siku nazalisha watoto wakike na wakiume na wote wanapitia kwenye njia moja na kutoka nje.
ReplyDeleteMie naongezea. Nabeba kitambulisho changu na hand sanitizer. Naweza nikapita mahali hakuna maji na nahitaji kunawa mikono ili nile kipande cha kuku.
ReplyDeleteISIWE TABU YAWEZEKANA MDAU UNATAKA KUNUNULIA UMPENDAYE HAYA MWAMBIE AWEKE VIFUATAVYO
ReplyDelete1. Kitabu cha neno la Mungu mfano Biblia. Pia Rosali
2. First Aid ndogo kama panadol, maginizium, plasta nk.
3. Vipodozi mbalimbali vikiambatana na chana za nywele na vibanio, nail cutter,mswaki na dawa ya meno ndogo, pair ya hereni mara nyingi zinaanguka hivyo uwe na ya kubadili nk
4. Pochi ndogo ya pesa na id mbalimbali
5. Kanga, Mtandio au Kitenge
6. Kila siku awe anatembea na always yaan pad tatu au nne ili kama sio yeye atamsaidie na mwingine. Hata one pair ya chupi kama upo kwenye siku zako sio mbaya ina tegemea na matatizo yako.
7. diary, pen, nk stationaries
8. Funguo za nyumba au gari
9. chaja ya simu
10. Mimi natembea na radio ndogo
11. Novel ambayo unaendelea kuisoma au magazine kama wewe ni mpenzi wa hayo
12.Freshiner ya mdogo au Pik au Big G, JOJO
13.Simu za mkoni
14. Kitambaa cha mafua hata viwili
15. Miwani ya jua na ya kusomea
Nichoka leo nitakwambia kesho tena
ww unayetukana wanawake ww inawezekana ukawa huna dada..mama wala penzi!!na kama unao...aibu yako....unawakosea heshima!!
ReplyDeletenewayzzz mm kwenye koba langu hua naweka....
a)Lotion
b)Perfume
c)Deodorant
d)Tissue
e)Handkarchief
f)Novel lazima..gazeti na Bible sumtymz
g)Pads
h)Kibanio cha nywele
i)Underpants
j)Kanga na kamtandio
k)Note book na kalamu
l)Make up na kioo
m)Walet muhimu
n)Viatu inategemea na ratiba
o)Mfuko mdogo wa plastic
funguo...simu na earphones!
Kwa mtaji huo lazima nikitoka nionekane kama nahama!ila ndo comfort yenyewe...bila mzigo wangu nakua sina amani!!
Lily
Hakuna kitu kinanifurahisha kama mautundu ya kufurahisha, eiwaa! nimecheka sana kuona mzee wa mikindani alipochokonoa mada, nikajua leo abaa kunankanyaga nyenga wa mshihiri. utajibiwa humu mpaka ukose dira.
ReplyDelete