
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Morogoro, Wafram Ngonyani ( kulia) akisoma baadhi ya orodha ya wanachuo waliosaini fomu maalumu ya kukubali kuendelea na masomo na kufanya mtihani wa ndani Machi 24, mwaka huu kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Said Kalembo ( kushoto) leo Chuoni hapo.



Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Ualimu Morogoro wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo ( hayupo pichani) jana ( machi 20) kwenye ukumbi wa Chuo hicho kuhusuana na madai yao mbalimbali yaliyotishia kugoma kwa wanachuo hao. Picha zote na mdau wa Mji kasoro bahari John Nditi
Poleni Sana.
ReplyDeleteJamani Ualimu shida na mateso hii fani jamani manyanyaso juu ya manyanyaso.Nimesoma hapo miaka 3 iliyo pita na sisi tulitaka kugoma tukaambiwa ualimu ni wito.Wakuu mnao soma angalieni yaani unaenda kufanya mafunzo ya vitendo kwa mwezi mzima unapewa 15000/= maanake 500 au jero jero kwa siku wapi na wapi jamani?
ReplyDeleteNi mateso juu ya mateso nashukuru Mungu baada ya kumaliza niligoma hata kwenda kufundisha mpaka leo hii nimekuwa mjasilia mali.
Nashangaa toka miaka hiyo hiyo BTP watu tulikuwa tunalipwa hiyo hiyo 15000/= mpaka leo hii wanachuo wanalipwa hiyo hiyo....dah maumivu kweli.
Wakati mafisadi wanajipendelea mikate mikubwa mikubwa.Fani nyingine zisikieni tu wadau.
Mi mdau Fidel.
michuzi picha tele na umeshindwa kueleza la muhimu nalo ni sababu za wanafunzi kutishia kutoingia madarasani
ReplyDeleteNaungana na Mdau wa hapo juu,Sababu za kugoma ni zipi? kwani hata wanajamii tunashindwa kutoa mchango juu ya tatizo linalowasibu.Mimi nami nilipata kua mwanachuo hapo MOTCO. Hakuna fani yoyote isiyokua na matatizo.Tufahamishe TATIZO. " Unaweza kukuta wanalazimishwa kula chakula mara tano kwa siku kumbe suluhisho lake ni kwenda kupeleka chakula hicho kwa watu wengini.
ReplyDeleteTUELEZE TATIZO.