Mkuu wa Chuo cha Ualimu Morogoro, Wafram Ngonyani ( kulia) akisoma baadhi ya orodha ya wanachuo waliosaini fomu maalumu ya kukubali kuendelea na masomo na kufanya mtihani wa ndani Machi 24, mwaka huu kwa Mkuu wa  Mkoa wa Morogoro Said Kalembo ( kushoto) leo Chuoni hapo.
 

Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Ualimu Morogoro wakisomba viti tayari kwa ajili ya mkutano wa dharura kati ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Said Kalembo ( wote hawapo  pichani) , Viongozi wa Chuo  kwa lengo la kufikia muafaka wa tishio la mgomo leo
Baaadhi ya wanachuo wa Chuo cha Ualimu Morogoro wakijifunika nyuso zao na wengine wakiuchapa usingizi kutokana na uchovu wa aza ya tishio lao la kutaka kuonga kuingia madarasani na kufanya mtihani wa ndani
 Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Ualimu Morogoro wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo ( hayupo pichani) jana ( machi 20) kwenye ukumbi wa Chuo hicho kuhusuana na madai yao mbalimbali yaliyotishia kugoma kwa wanachuo hao. Picha zote na mdau wa Mji kasoro bahari John Nditi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poleni Sana.

    ReplyDelete
  2. Jamani Ualimu shida na mateso hii fani jamani manyanyaso juu ya manyanyaso.Nimesoma hapo miaka 3 iliyo pita na sisi tulitaka kugoma tukaambiwa ualimu ni wito.Wakuu mnao soma angalieni yaani unaenda kufanya mafunzo ya vitendo kwa mwezi mzima unapewa 15000/= maanake 500 au jero jero kwa siku wapi na wapi jamani?
    Ni mateso juu ya mateso nashukuru Mungu baada ya kumaliza niligoma hata kwenda kufundisha mpaka leo hii nimekuwa mjasilia mali.
    Nashangaa toka miaka hiyo hiyo BTP watu tulikuwa tunalipwa hiyo hiyo 15000/= mpaka leo hii wanachuo wanalipwa hiyo hiyo....dah maumivu kweli.
    Wakati mafisadi wanajipendelea mikate mikubwa mikubwa.Fani nyingine zisikieni tu wadau.
    Mi mdau Fidel.

    ReplyDelete
  3. michuzi picha tele na umeshindwa kueleza la muhimu nalo ni sababu za wanafunzi kutishia kutoingia madarasani

    ReplyDelete
  4. Naungana na Mdau wa hapo juu,Sababu za kugoma ni zipi? kwani hata wanajamii tunashindwa kutoa mchango juu ya tatizo linalowasibu.Mimi nami nilipata kua mwanachuo hapo MOTCO. Hakuna fani yoyote isiyokua na matatizo.Tufahamishe TATIZO. " Unaweza kukuta wanalazimishwa kula chakula mara tano kwa siku kumbe suluhisho lake ni kwenda kupeleka chakula hicho kwa watu wengini.
    TUELEZE TATIZO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...