kijana ibrahim saidi akitoka katika mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu baada ya kusomewa shtaka la shambulio la kudhuru, ambapo anatuhumiwa kufanya kosa hilo machi 10, 2009 kwa kumpiga kofi la shavu la kushoto rais mstaafu alhaj ali hassan mwinyi kwenye ukumbi wa diamond jubilee hall wakati wa baraza la maulid

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. nadhani utaratibu wa kutuletea picha za video utkua mzuri sana muheshimiwa mwenyekiti intia raha unapoona vijana wa said mwema wanavyotoa maelekezo kwa waandishi wa habari ,ila nashangaa imekuwaje kesi isogezwe tena mbele wakati mwenyewe ameshakiri nildhani hapo ilikuwa ni hukumu tu

    ReplyDelete
  2. Yule mwingine aliyemrushia Kiatu Rais Mstaafu George Bush wa Marekani hivi karibuni,Leo naye kalambwa Miaka Mitatu JELA kwa kosa hilo!Naye pia alikuwa anapitisha ujumbe wake kwa staili ya peke yake,baada ya kuona magazeti na mitandao haitoshi!Sasa huyu jamaa yangu anayejiita Sultan Ustaadh "moto utamwakia".Kutenda bila kufikiri kwanza,akili za Panzi kwelikweli!Majuto mjukuu sasa!Sitashangaa akilamba miaka mitano!

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha kuwa mbali ya kujaa jela zetu, mtu anapokiri kosa lake bado anapelekwa tena kumande. Nafikiri kwa kesi kama hizi inabidi hukumu hapohapo
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  4. Namvizia huyo jamaa nimlambe kibao hapo kisutu! hawezi kumpiga Mzee wetu na sisi tukamwachia! Dini inaheshimu sana watu wakubwa waliokuzidi umri...huwezi kumpiga mzee wako kofi tena mbele ya hadhara eti kwa kisingizio cha dini!!Mbona sijaona mtu anapigwa vibao au hata kutukanwa anapozungumzia kondom barabarani??/ kwa nini iwe mzee Mwinyi?? alaaniwe huyo kijana hata kama anatetea Dini!! Namlaani huyo kijana na hata asipofungwa hilo kosa alilofanya litamfata kila atakapokuwa na hatafanikiwa maisha yake yote!! Kitendo cha kumpiga kosa Mzee wetu mpendwa kimeniuma sana na sina raha toka siku ile...Namwomba mzee wangu Mwinyi atulie na mimi nitamlipizia kisasi!!Wadau tushirikiane kumlaani huyu kijana

    ReplyDelete
  5. hivi ndio vitu unavyotakiwa kuviongeza ktk blog yetu ya jamii,
    kuna wanablog millions wanaotembelea hapa tokea ifunguliwe,kila kitu kipo poa hapa,lakini naona tusiendlee na kila siku mmbo hayo hayo,tubadilike kwa kuweka video sasa ili wanablog wajionee watukio mbali mbali pamoja na kauli za kusikia ,na kuchangia maoni,video ni muhimu sana,na sio picha tu miaka yote.

    ReplyDelete
  6. Dawa wamweke Jangwani na apigwe risasi hadharani! Wakifanya hivyo wengine hawatamwiga!

    ReplyDelete
  7. mie naona mwinyi ndio mwenye makosa kuzungumzia watu kutumia kondomu kwenye sherehe ya dini ni kama unaunga mkono zinaa.hio topic angeiruka tu na angeizungumzia kwenye sehemu zingine.kwahio ustadhi kama alivyojielezea yeye alitaka kutuma ujumbe tu kupinga zinaa na njia hile ndio aliona ina faa kwa vile yeye mlala hoi.
    diwani alicha bakora walimu sasa raia kamchapa kibao kiongozi ha ha ha.tanzania tambarare.

    ReplyDelete
  8. Hongera Michuzi kwa kutuwekea video ya mbaya wa Rais Mwinyi akitoka mahakamani.... tunaomba utuwekee na video wakati akimulamba kibao Rais Mwinyi...tafadhari

    ReplyDelete
  9. Like if I was dreaming...niliangalia ile picha ya maulidi nikajiuliza hivi wanawapa walinzi kwa muda gani baada ya kuachia uongozi??????

    Jamani wamlinde baba wa watu....hata kama mtu humpendi mtu mwingine huna right ya kumpiga....kwanza kapiga the wrong person baba wa watu hakufilisi nchi...waliofilisi nchi wako na mabody guard kila siku

    ReplyDelete
  10. Hekima sio kuzungumza neno zuri tuu, ni kuzungumza neno zuri pahala na wakati muafaka na kwa hadhira muafaka ukitumia njia bora kabisa bila kukinzana na maadili ya hadhira.

    ReplyDelete
  11. Kijana alikuwa anaondoa tatizo kwa mkono.

    ReplyDelete
  12. Basi tu kwa sababu sisi ni wepesi wa kusahau vinginenyo. Shinyanga siku ya kupigwa kibao Rais Mstaafu kungekuwa na Bugobogobo la kufa mtu.

    ReplyDelete
  13. BAADA YA KUTOKA KATIKA GIZA KALI LA 70s NA 80s WATANZANIA WANAMUONA MWINYI KAMA ALMASI.VIPI AL HAJI TENA MZEE MBELE YA WAUMINI UNFUNDISHA UCHWARA INAMAANA WEWE UNAYAFANYA HAYO. INASIKITISHA KUPIGWA. LAKINI INASIKITISHA ZAIDI KUPINGA AYA ZA M MUNNGU.TUBU NA UMSAMEH HUYU MUUMINI.

    ReplyDelete
  14. fair play ni kuwa mzee mwinyi mwenyewe amsamehe huyu jamaa,kwani hata yeye mwenyewe nadhani alikose kuongelea ngono sehemu hio,pia hata ktk utawala wake sio yote mazuri aliyoyafanya,kuna makosa kibao,lakini binadamu wote wa bongo tumemridhia na kumsamehe kama mzee wetu,

    hakuna aliekuwa hana kosa,

    ReplyDelete
  15. Ningefurahi sana angemchapa kibao mkapa.

    ReplyDelete
  16. Tuanzishe tamaduni za kuwachapa vibao MAFISADI na kuwazomea,Sio Mzee Mwinyi.Yani Imeniuma sana

    ReplyDelete
  17. JIONEE VEDIO YA MZEE RUKSA AKILA KIBANO www.youtube.com/watch?v=DFzsCShW-Xg

    ReplyDelete
  18. Watoa maoni wengine hawana akili kabisa!Sipendi kuwaita watoa maoni watanzania,kwasababu natambua wazi kwamba watoa maoni wengine humu wako ughaibuni na hata Mashariki ya Kati!Kumbe usipozungumzia mambo ya Ngono na Zinaa katika mihadhara ya Dini,iwe makanisani au misikitini,kumbe Ukazungumzie Wapi?Vilabuni na kwenye Madanguro? Wajinga kwelikweli!Ukweli hauta badilika,utake usitake watu wataendelea kufanya zinaa kila siku!Maelfu ya watu wanakufa kila siku kutokana na maambukizo ya ukimwi!Lipi jema na la busara zaidi,Kiongozi wa Dini akae kimya na kuacha kulizungumzia tatizo hilo na maelfu ya waumini wake waendelee kuteketea AU Kiongozi wa Dini awe jasiri wa kuzungumzia masuala hayo katika hali ya uwazi na kistaarabu zaidi? Wajinga watatamka,acheni hao malaya wafe,wakumbane na hukumu ya Mola!Lipi Baya zaidi,kuoa wanawake wengi au kutumia kondomu hata kama una mke mmoja tu wa ndoa? Huyu Kijana Laana itamshukia!Labda ahame nchi hii akatafute huko kunakomfaa wanako ishi kwa "Sharia!"Tanzania hatutaki "shari".

    ReplyDelete
  19. annon apo uko sawa

    ndo nchi sasa ikiongozwa na SHARIA NA MAHAKAMA YA KADHI

    yan sheria mkononi,kukatana vidole,kupigwa mawe,kuchapwa makofi nk

    kaaazi kweli

    Tz is secular state,,,basi

    hawa wenye imani kali sijui waangaliwe sana wako wengi sana misikitini.watafutiwe kisiwa chao wakae huko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...