Pole kwa kazi kaka Michuzi.Naomba unipatie nafasi ktk blog yako ili kupata msaada kutoka kwa wadau.

Nina rafiki yangu kutoka UK,alinifuata na kuniambia kuwa anatafuta nyimbo yeyote ya kiingereza iliyoimbwa na mwana muziki yeyote kutoka Afrika na ingekuwa vizuri zaidi kama atakuwa ni wa kutoka nchini kwangu (Tz).Kwa kweli sikuwa na nyimbo yeyote ya kiingereza kutoka Tz,ila niliahidi kumtafutia.

Kwa hiyo ninaomba kama kuna yeyote anayefahamu nyimbo yeyote ya kiingereza kutoka Tanzania anisaidie au anipatie jina la wimbo na muimbaji.Nina nyimbo nyingi tu za kiingereza kutoka Africa lkn ningependa sana kumpatia ya kutoka nchini kwangu.

Ni hayo tu kwa leo,kazi njema.

Mdau,
TLS,FR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Mdau . Kuna mwimbaji wa Kitanzania anaitwa Emanuel Nkulila, ameimba nyimbo kama Hello na The pain in me. Nenda www.eastafricantube.com ,tafuta utakuta wimbo wake wa "pain in me"..Kila la kheri!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hello mambo jmn mm nautafuta sana huo wimbo but nimeshindwa kuupata pls pls pls nisaidie namna ya kuupata

      Delete
  2. nyimbo ipo na inaitwa "you are always welcome to zanzibar" ambayo imeimbwa na Chimbeni Kheri katika culture musical club, Zanzibar

    ReplyDelete
  3. mdau unataka wimbo wa aina gani?

    bongo flava kuna "performer" wa ngwair na TID
    kuna mr politician wa nakaaya, ameimba kiingereza na kiswahili

    nikifikiria zingine ntakupa....

    ReplyDelete
  4. Hahaha.... Huyo mpatie ya Dr Remmy Ongala, I wish to go back Home ili ajifunze na kiswahili pia.
    Asenti

    ReplyDelete
  5. mdau ungewaandikia Basata wakusaidie wpo wengi tu hata wkina Karola Kinasha Wameimba

    ReplyDelete
  6. Sauda Simba Kilumanga na Caroline Kinasha wana nyimbo kibao walizoimba kwa Kiingereza, ila inabidi uzinunue sio za bure!

    Mzalendo

    ReplyDelete
  7. mdau kama huyo rafiki yako anao mshiko mlete kwangu mimi nitamuimbia live hio nyimbo kwa kiingereza

    ReplyDelete
  8. pia unaweza kumsikiliza dogo mmoja hivi alikua kwenye kikundi cha park lane zamani sasa anafanya kazi peke yake. anaitwa c pwaaa anafanya siku hizi bongoflava kwa kiingereza na anachanganya kidogo na kiswahili kama kuna track yake moja inaitwa revenge ni amefanya kiingilish kitupu musikilie hapa copy and paste hii link http://profile.myspace.com/index.cfm?fuseaction=user.viewprofile&friendid=214133407

    ReplyDelete
  9. wimbo JAH SPIRIT wa Justine Kalikawe (R.I.P) nadhani utakufaa.

    ReplyDelete
  10. kama ni jina la msanii na jina la wimbo ushapewa!!!

    lakini kama wataka wimbo,koma tena KOMA vya bure na uyo mzungu wako km wataka kufilisi wabongo wezio,MNUNUE IZO NYIMBO,YANI UYO SHEFA LAKO ANUNUE KABISA sio kukosesha mapato wa-bongo

    ENSI MWALUKASA wimbo "my home"full kiinglishi,nk nk for gospel musics

    ushanfahamu wewe???

    ReplyDelete
  11. (..jaribu kuimba kwa sauti kavu ila ya puani):'mwalimu kasema iti ken bee daan, plei yua paaatii..mwalimu kasema iti ken be daaaani, plei yua paaatiii'...hivi huu bado wapatikana? hebu wadau saidieni jinsi ya kumpatia huu!...

    UZENG

    ReplyDelete
  12. Innocent Galinoma, "Kilimanjaro".

    Standing on the mountain top
    of Mt Kilimanjaro
    The highest mountain in Africa....

    ReplyDelete
  13. wadau nashukuru sana kwa msaada wenu,mpaka sasa nimeweza kufanikiwa kupata nyimbo kutoka kwa Cpwaa na Emanueli Nkulila

    Anon wa March 05, 2009 3:50 PM asante kwa link ya Cpwaa.

    Anon wa March 05, 2009 12:59 PM asante kwa link ya Nkulila
    Kama kuna zaidi, tusaidiane wadau!

    Mdau TLS,FR.

    ReplyDelete
  14. siku ni hii x 2 bwana ameifanya x2 furahini shangilieni

    sasa mwimbie kwa kidhungu


    na ule if you are happy and u know claps ur hands

    lol hizo ni free zingine mwambie anunue.....frugal

    ReplyDelete
  15. Nyie, Nkulila is a joke!

    Tafuta mwimbo wa "Zanzibar" aliimba mzaliwa wa Unguja na aliuimba akiwa na bandi ya "Queen"

    Vilevile, Innocent Galinoma Mfalingundi ana album kama tatu hivi katika miondoko ya Reggae, mmojawapo ndio huo "Kilimanjaro", but "Full Moon Rising" is my personal favorite!

    ReplyDelete
  16. MR.PAUL ANA NYIMBO AMEIMBA KWA KIINGEREZA PIA...

    ReplyDelete
  17. Sijui nimechelewa kucomment lakini wacha niandike. kibao cha KILIMANJARO cha INNOCENT GALINOMA kimetulia sana tena sana. Standing on the mountain top of mount kilimanjaro the highest mountain inAfrica there i see a vision.
    NImemaliza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...