Juma Nature akighani kiitikio cha wimbo wake mpya uitwao Ulevi,anaefuata ni Feruzi pamoja na Jb wa Mabaga Fresh ambaye amejiunga na Wanaume Tmk Halisi kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kundi hilo. Jb alisema kuwa ameamua kujiunga ndani ya kundi hilo kutokana kulipenda na watu waliomo wanajua wanachokifanya, aidha Jb amelifananisha kundi hilo na timu ya Taifa Stars , kwamba inaweza kufanya usajili kutoka kwa timu yeyote ile, hivyo na ndivyo vivyo kwa kundi hilo ambalo limekuwa likijizolea umaarufu kila kukicha.

 Juma Nature a.k.a Kibra a.k.a Kiroboto na  msanii mwenzake Feruzi Mrisho a.k.a Feruzi  leo wanazindua albamu zao mpya (ya Juma Nature inaitwa TUGAWANE UMASKINI, na ya Feruzi  ni SAUTI NA VYOMBO).

Uzinduzi huo utafanyika katika  ukumbi wa diamond jubilee ambapo  kiingilio kimepangwa kuwa buku tano kwa kila kichwa.

Katika uzinduzi huo kutakuwepo na wasanii kadhaa watakaotoa kampani kwa wasanii wenzao, ambao wametajwa kuwa ni Fid Q, Afande Sele,Wakali kwanza (Q jay &Makamua), Jua Kali kutoka Kenya, Jaffarai, na wengine kibao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Juma Nature ni mwizi mtupu na rasta zake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...