Juma Nature akighani kiitikio cha wimbo wake mpya uitwao Ulevi,anaefuata ni Feruzi pamoja na Jb wa Mabaga Fresh ambaye amejiunga na Wanaume Tmk Halisi kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kundi hilo. Jb alisema kuwa ameamua kujiunga ndani ya kundi hilo kutokana kulipenda na watu waliomo wanajua wanachokifanya, aidha Jb amelifananisha kundi hilo na timu ya Taifa Stars , kwamba inaweza kufanya usajili kutoka kwa timu yeyote ile, hivyo na ndivyo vivyo kwa kundi hilo ambalo limekuwa likijizolea umaarufu kila kukicha.
Juma Nature a.k.a Kibra a.k.a Kiroboto na msanii mwenzake Feruzi Mrisho a.k.a Feruzi leo wanazindua albamu zao mpya (ya Juma Nature inaitwa TUGAWANE UMASKINI, na ya Feruzi ni SAUTI NA VYOMBO).
Uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa diamond jubilee ambapo kiingilio kimepangwa kuwa buku tano kwa kila kichwa.
Katika uzinduzi huo kutakuwepo na wasanii kadhaa watakaotoa kampani kwa wasanii wenzao, ambao wametajwa kuwa ni Fid Q, Afande Sele,Wakali kwanza (Q jay &Makamua), Jua Kali kutoka Kenya, Jaffarai, na wengine kibao.
Juma Nature ni mwizi mtupu na rasta zake!
ReplyDelete