Mkuu mpya wa  Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, Fatma Mwassa akila kiapo cha utii katika kazi yake ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu  Said Kalembo leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh. Saidi Mwambungu akimpongeza Mkuu Mpya wa Wilaya ya Mvomero Mh. Fatma Mwassa baada ya kuapishwa.
Si mnajua jamani mimi ni mwezenu…ndivyo ishara inavyoonyesha na Mkuu mpya wa  Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro,  Mh. Fatma Mwassa, ( kushoto), wakati akibadilishana mawazo na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwake jana ( Aprili 11) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Mh. Mwassa ni mwandishi wa habari wa siku nyingi na kabla ya uteuzi huu alikuwa msaidizi maalumu wa Mama Salma Kikwete. Picha na mdau wa mji kasoro bahari John  Nditi
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Alahala, naye asije charaza walimu viboko.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Da Fatmah
    Kil la heri Mheshimiwa,
    Pius ex -co staff Business Times

    ReplyDelete
  3. Kuwa mkuu wa wilaya na nafuu uje huku kubeba mabox. Mshahara haufiki $500 kwa mwezi na bado hapo Dr. Slaa anakuambia unalipwa hela nyingi.

    ReplyDelete
  4. Inakera sana kusoma mambo ya watu wasiofuatilia vitu, kama wale jamaa wanaojaza blogu na makala za Kiingereza kibovu na kudanganya kuhusu nafasi zao.

    Dkt. Slaa hajalalamikia mishahara ya Wakuu wa Wilaya, yeye analalamikia posho (siyo mishahara) ya Wabunge.

    Pili, DC halipwi dola 500 pekee, nadhani mshahara wao unazidi dola hizi ukibadili. La msingi ni kwamba wana kasma ya shilingi milioni 10 kila mwezi ambayo haikaguliwi kinoko, kwa kuwa ni ya utendaji wilayani. Hapo ndipo kwenye hela. Si unawaona hao wanaocheka hapo?

    Tujifunze kuhusu nchi yetu, siyo kukalia kusema lolote tu!

    ReplyDelete
  5. Duh ni kweli hiyo kwamba DC analipwa $500 ??!!

    Mbona kituko! Je ana marupurupu gani mengine (eg, gari? nyumba? bima ya afya? per diem akiwa safarini? per diem akiwa kwenye vikao? what else ...?)

    ReplyDelete
  6. kama hamna habari siasa ni ulaji na WIZI MTUPU. Ndio maana kila mtu anakimbilia huko sasa.

    ReplyDelete
  7. Watu wengine ovyo badala wafikirie ni maendeleo gani atakayoyalete ktk wilaya wanabaki kujadili ni mshahara kiasi gani anapata,tunamuombea kila la kheri na atuletee maendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...