
Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, Fatma Mwassa akila kiapo cha utii katika kazi yake ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa.


Si mnajua jamani mimi ni mwezenu…ndivyo ishara inavyoonyesha na Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, Mh. Fatma Mwassa, ( kushoto), wakati akibadilishana mawazo na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwake jana ( Aprili 11) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Mh. Mwassa ni mwandishi wa habari wa siku nyingi na kabla ya uteuzi huu alikuwa msaidizi maalumu wa Mama Salma Kikwete. Picha na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi
Alahala, naye asije charaza walimu viboko.
ReplyDeleteHongera sana Da Fatmah
ReplyDeleteKil la heri Mheshimiwa,
Pius ex -co staff Business Times
Kuwa mkuu wa wilaya na nafuu uje huku kubeba mabox. Mshahara haufiki $500 kwa mwezi na bado hapo Dr. Slaa anakuambia unalipwa hela nyingi.
ReplyDeleteInakera sana kusoma mambo ya watu wasiofuatilia vitu, kama wale jamaa wanaojaza blogu na makala za Kiingereza kibovu na kudanganya kuhusu nafasi zao.
ReplyDeleteDkt. Slaa hajalalamikia mishahara ya Wakuu wa Wilaya, yeye analalamikia posho (siyo mishahara) ya Wabunge.
Pili, DC halipwi dola 500 pekee, nadhani mshahara wao unazidi dola hizi ukibadili. La msingi ni kwamba wana kasma ya shilingi milioni 10 kila mwezi ambayo haikaguliwi kinoko, kwa kuwa ni ya utendaji wilayani. Hapo ndipo kwenye hela. Si unawaona hao wanaocheka hapo?
Tujifunze kuhusu nchi yetu, siyo kukalia kusema lolote tu!
Duh ni kweli hiyo kwamba DC analipwa $500 ??!!
ReplyDeleteMbona kituko! Je ana marupurupu gani mengine (eg, gari? nyumba? bima ya afya? per diem akiwa safarini? per diem akiwa kwenye vikao? what else ...?)
Kalio.
ReplyDeletekama hamna habari siasa ni ulaji na WIZI MTUPU. Ndio maana kila mtu anakimbilia huko sasa.
ReplyDeleteWatu wengine ovyo badala wafikirie ni maendeleo gani atakayoyalete ktk wilaya wanabaki kujadili ni mshahara kiasi gani anapata,tunamuombea kila la kheri na atuletee maendeleo.
ReplyDelete