Brain Drain?: A response to the post:
YU WAPI MWALIMU INNOCENTUS ALHAMIS?
Mr. Michuzi mimi ni mpenzi sana wa blog yako. Leo nilikuwa nikipitia pitia nikakutana na post moja ya: Yu wapi mwalimu Innocentus Alhamis. Binafsi simjui huyu mwalimu ila kutokana na sifa alizozitoa ndugu Mtei, hasa kwamba jamaa ni tofauti na ma lecturer wa bongo ambao ninawafahamu fika, nikaamua kum google huyu mwalimu (mwenye majina yanayovutia pia) kujua wasifa wake zaidi. Nilikumbana na site nyingi kumhusu lakini hii ilinipa changamoto zaidi:
http://www.ratemyprofessors.com/ShowRatings.jsp?tid=1002993&page=1
Je tuiite hii ni brain Drain ama ni kitu gani? Je Open University wanaiona hii? Imekuwaje hadi wananyanganywa jamaa kama huyu muhimu?
Pengine ni Chuo chenyewe kimemsomesha huko majuu kwa gharama kubwa za chuo (inaonekana amesha ikwaa PhD yake) na ofcourse gharama za walala hoi. Nilifika pale Open university nikakuta ni kama hawana waalimu wa kutosha na wenye sifa za kutosha hasa eneo la Economics ambayo mjamaa anawapagawisha nayo wazungu huko majuu.
Je ni wabongo wangapi wanafanya makubwa kwenye nchi za wenyewe na skills zao zinakubalika sana? Je kuna shida gani zinawakumba wabongo hadi wazamie?
Huyu jamaa ni just a fraction ya wabongo wanaotumiwa na wenye kujua jinsi ya kutumia bongo za wabongo hwakati bongo inazidi kubongolewa na mafisadi wenye bongo zilizo chafu. Kumbe basi sio tu kwamba tunaibiwa madini, nyara za serikali tu na wenye meno ya kutafuna huku tukikaanga ubuyu bali hata na bongo zetu.
Je serikali ifanyeje watu kama Sheikh Ali-Hamis ama Fr. Innocentus warudi ?
Je serikali imewawekea mazingira gani ya kuwafanya warudi wakisha kula nondo badala ya kuzigawa hukowaliko zifuatia?
Je ni halali fedha za wabongo zitumike kuwasomesha akina Shekh Ali Khamis na Fr. Innocentus halafu wao watokomee?
Nadhani akina Shekh Ali-khamis na Fr. Innocentus Na wengineo wanapaswa kutueleza sababu za wao kula za kwetu na kuwafaidisha wengine.
Kama mishahara ya Bongo haiwatoshi ama mazingira hayafai kuwawezesha basi sisi wana jamii tule na serikali sahani moja kujua kwanini Mafisadi yanaifilisi nchi badala ya kuwawezesha akina Alhamis ama Innocentus warudi kuiinua?
Imagine huyu mjamaa huko majuu anaitwa a “hot Professor”
A debate
Mdau Sunday Maneno
tanzania haijali sekta ya elimu. haitaki kuwekeza kuhakikisha kwamba "academicians" kama hawa wana infrastructure iliyotulia ya kufanyia kazi. most academicians hata huku ughaibuni do not really care for the money, wanachotaka ni wawe na nafasi ya kufanya kazi yao kwa ufanisi. bongo bila bila. what do you expect? hata mimi nikipata nafasi kwenye hizi serikali zenye hivi vyuo vinavyowezesha kazi ya academician nabaki tu, bongo ufisadi mwingi macho yote kwenye wizi mtupu!!!
ReplyDeleteUS-Blogger)
ReplyDeleteWW Sunday Maneno, vipi Ulitumwa na Nabii, Mtakatifu Yohanna Mashaka kuposti hii atiko nini?
Nadhani siyo yake kwa sababu ingekuwa yake Ingeandikwa na chiinglishi kigumu cha Zamani cha Dictionary
Nadhani lekcha yuko huko majuu anamfundisha yohanna mashaka
US-blogger.
Serikali iongeze majimbo ya wabunge ili wasomi wote wakirudi wapate nafasi.Tanzania inalipa ukiwa waziri mbunge or Rais.(UFISADI)
ReplyDeleteShida ni Miundombinu Bongo....Maneno kibao.
ReplyDeleteWe have to walk the walk not talk the walk,man!
Yaani jamaa yupo Southern New Hampshire university,Economics department, anakula kuku wake kilaini na wazungu wanamkubali kinoma maana jamaa ni kichwa kwelikweli!
ReplyDeleteBongo tambarare!
mdau ughaibuni!
ni habari ya kuskitisha sana.
ReplyDeleteIla napenda kukufahamisha kuwa hii siyo bahati mbaya au ezembe.
Hii ni planned kabisa, watu wamekaa na wanaona ili watutawale vizuri bila vurugu kama nigeria, ni muhimu watanzania angalao asilimia 70 wawe mazezeta.
Ndio mkakati, yani wao na watoto wao wachache, na watu wachache sana ndio wataingia kwenye circle ya kula matunda ya utanzania.
Wengine mlie tu.
Nyie na watoto wenu na wajukuu wenu mtadumaa (kiasi), kiafya tangu tumboni mwa mama zenu (hawaweki plans za afya) chekechea haina hata sylabus, lakini wao wanapeleka watoto wao kwenye acredited schools, primary ndio hivyo tena, minyoo tu na surua inarudi, huko mbele ndo mko nyie wachache,
WHAT ARE YOU PLANNING TO DO NOW?
Naelewa inasikitisha kuwa nchi inasomesha watu halafu unakuta wanaosomeshwa huwa hawarudi but mie naomba kuuliza wadau wasomi wangapi ambao wamerudi Tanzania wakawa na mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa ufanisi. Wengi wao huishia kama sio fustration of finding out mazingira magumu ya wao kuendelea basi huishia na wao kuwa mafisadi. Wanaishia kutengenezea projects ambazo mtu anakwiba ndani yake kiasi kikubwa huku akihalalisha utumiaji wa fedha zake. Wengine huingia katika siasa na kuishia kuwa mafisadi mifano hai ipo na inajulikana wazi lakini unajiuliza kwanini mbona huku ulaya maprofesa hadi ateuliwe ndio huingia katika siasa tena sio mwanasiasa bali mshauri wa wanasiasa.
ReplyDeleteMie siwaungi mkono wanakimbilia nchi za nje kwasababu bado damu ya utaifa ipo ndani ya damu. But naelewa kwanini wanaishia huko ninasoma na watu wanaochukua PhD ni shule ngumu si lelemama kuna jamaa mbeirut aliwahi kuniambia anajiuliza kwanini anateseka hivi alitaka kulia. Hawa madr na maprofesa huwa hawasemi hivi vitu but mie nawaambia si shule rahisi wala kuimba kwaya waulizeni watawaambia sasa mtu anapoteseka hivi unadhani akirudi bongo kama hajawezeshwa atakaa kweli????
Mie na kimasters changu tu chanitoa jasho sasa unakuta mtu anahenyeka hivyo halafu mtu akaja kila akianzisha kitu ideas uwezeshaji, miradi vyote huangaliwa huyu ni mwenzetu au si mwenzetu unadhani mtu anabaki???
Tukae tukijua gharama za PhD si pesa tu mpige hesabu na muda wake aliotumia, vitu alivyosacrifice angelikuwa akifanya kazi kwengu just kuja kuwa mtafiti wa sekta fulani, pension yake halafu mjiulize gharama ya PhD kiasi gani acheni kuosha vinywa jamani tuweni binaadamu. Kuna mshkaji mmoja nilimkuta hapa ndio anamalizia PhD anatokea Vietnam alilia alipomaliza thesis yake nyie mnakaa mnaosha vinywa tu waambieni wanasiasa na watunga sheria wafikirie mara mbili kabla ya kuanza kunyoosha vinywa kwa vichwa kama hivi tunahitaji wasomi wetu kama mkuu imf alivyosema but tuweke mazingira mazuri ya utendaji kazi na sio title tu. Matokeo yake unakuta professa anafariki hata hela ya jeneza hana halafu aliowasema ndio wanamchangia this is a disgrace
mengi mazuri yameelezwa,kwa sisi watz,umuhimu wa elimu na mazingira ya kazi bado ni tatizo kubwa,
ReplyDeletemfano mdogo tu,kwa elimu yako yoyote,ukitoa japo ushauri mzuri kwa jambo lolote lile,hisia ya kwanza kwa malimbukeni "unajifanya unajua sana"-"wengi tuna roho mbaya na roho za kwanini".
mtu akiwa na ari ya kujituma,atakatishwa tamaa ama kutishwa kwa hili ama lile,ili mradi watu watetee ufisadi wao!-tutafika wapi kwa mtindo huu...?
kasumba ya wachache/wengi waliowekwa ama kulindwa katika nafasi zao(kati ama juu),wanahofu kupoteza nafasi zao kwa kuwa na cv zenye mapungufu,
lazima wawe wababe kijinga,akionekana msomi anaelekea lazima adhoofishwe kwa jinsi yoyote ili watu waendeleze yao!!!
kwakweli katika sekta nyingi watatukimbia wengi,hata mimi nitaweza kupotea vilevile,bora nikawape faida wanaojali na kuona umuhimu wake kuliko kukomaa na mashaka ya maisha-
shule/kusoma siyo kulipiwa ada tu bali pia ni kichwa na juhudi ya mtu binafsi ambavyo pia vinahitaji support kufanikisha,(ni maumivu mazito,yanahitaji kujali).
kwa hilo uzalendo utamshinda mzalendo.
-nilikuwepo.
Du wadau, kwa mtaji huu lazima sasa tuwaweke sawa vijana wetu wisaidie serikali ya mzee JK, hata kwa mawazo tu kunatosha
ReplyDeletejust fikiria
ukawa na kakikundi cha akina
Alhamis USA
Mashaka USA
dr shayo UK
Ridhiwani TZ
Juanuary TZ
Alex UK
si wengi mnamfahamu ALEX, ila huyu jamaa ni mtanzania miaka yake haijakita miaka 34 na ni mtaalamu wa kutegemewa huko UK kwa maswala ya energy. Hata maprofessor wa Cambridge na Oxford wanapiga hodi kwake kupata utaalamu wake.
Joseph Minja-British Council UK
Nk Nk
Kuna haja ya kuunda mtandao wa wataalu wetu hata waweze kusaidia kwa mawazo tuuuuu
Jamani, jamani tuwadhamini wasmi wetu. hawa ndiyo watakaoikomboa tanzania. Tuwatumie kwa mawazo yao kabla haujawa To late!
Mungu ibariki Tanzania
Kuna mdau amehoji inakuwaje watu wamesomeshwa na bongo halafu wanaenda kufaidisha ughaibuni. Jibu lake rahisi ni kuwa hawa watu hawakusomeshwa bure kama ilivyokuwa enzi za mwalimu. Wanadaiwa kiasi walichokopeshwa na bodi ya mikopo, basi. Kingine ni kuwa wengine hawa japo walisoma shahada moja au mbili bongo, wamepata PhD zao ughaibuni kwa gharama za mataifa ya ughaibuni. Kwa hiyo na huko nako wana deni.
ReplyDeleteKinachowafanya wawe radhi kulipa madeni ya ughaibuni licha ya ugumu wa kukabiliana na mabadiliko ya kimaisha ni kuwa wanapata mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Wana vitendea kazi vya kufanyia utafiti na vipato vya kuwawezesha kuishi maisha mazuri ya kawaida. Wengi wao hawana vipato vya kuwafanya wawe na pesa kama wanasiasa wa Tanzania. Lakini wana uhakika wa kula, kulala, kufanya kazi wapendayo na kusomesha watoto wao katika shule za kuridhisha. Vilevile wana uhakika wa pensheni itakayowawezesha kuishi maisha mazuri ya kawaida watakapofikia umri wa kustaafu. Watu hao kama wangeamua kurudi bongo, wangekumbana na ukosefu wa vitendea kazi, maisha ya kubahatisha hata katika masuala ya msingi kama mlo, pa kulala, kusomesha watoto na kumwagiwa maji na mashangingi ya wanasiasa wakisubiri daladala na kushuhudia ana kwa ana watu wakidhalilisha kazi waliyoifanya wao kutafuta PhD kwa kujiita madokta kwa shahada za vyuo ambavyo havitambuliki.
Je mtoa mawazo kwamba kuwe na kakikundi ka kumshauri kiwete,je bwana US blogger naye atakuwa wapi?
ReplyDeleteUS BLOGGER ANA PhD ya oxford lakini michango yake humu ni ya kizezeta tupu la bongo
ReplyDeleteWadau
ReplyDeletehivi huyu Alex ni yupi? kuna mwenye wasifu wake?
Inaonekana jamaa ni kichwa kweli kweli, mpaka maprofessor wa cambidge kwenda kwake kuomba ushauri si mchezo
Huyu ni yule alex aliyekuwa chuo kikuu, kwa muda kabla ya kwenda UK?
NDugu Alex, unamfahamu kichwa kingine kilichoko huko UK kiitwacho shayo?
Vipi mchangiaji unamaanisha Alex Paurine? maana naelewa ndo amesomea maswala ya energy. Kama ni huyu basi ni kweli jamaa ni mzuri kwa ayafanyayo. Ukweli sijui kama ni kichwa maana sijakaa naye darasani na wala sina utaalamu wa fani yake lakini namuelewa vizuri kiasi. Sijui pia kama alisoma UDSM, lakini jamaa anakwenda mpaka nchi za nje za ulaya kusolve maswala ya energy. Wasifu wake ninajua anashahada ya tatu ikiwamo PhD lakini ni mtu wa chini, simple hapendi kujionesha, hana dharau wala misifa na anaupendo wa pekee. Huyu jamaa alisha feature kwenye BBC world service discovery channel kwa ugunduzi wake wa mitambo ya nishati. Kama ni yeye sifurahii sifa yake moja ya kutojichanganya na watu. Mkitaka kumjua vizuri muulizeni huyo mtaalamu na mwandishi wenu Dr Shayo anamjua vizuri.
ReplyDeleteMdau Birmingham