JK  akiwasili Dar huku mvua kubwa ikinyesha akitokea Zanzibar ambako alikwenda kuhudhuria maadhimisho ya Karume Day siku,  liyotengwa kukumbuka siku alipouawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amaan Karume tarehe 7 Aprili 1972
JK akiagana na Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid karume baada ya kuhudhuria shughuli za Karume Day Zanzibar, leo

JK akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume ikulu mjini Zanzibar mara baada ya maadhimisho ya Karume Day yaliyofanyikas Zanzibar leo
Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume(katikati) akiwa pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume (kulia) pamoja na mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein wakishiriki katika ibada ya kumuombea muasisi hiyo iliyofanyika katika Kaburi lake lililopo katika jengo la ofisi kuu ya CCM ,Kiswandui Zanzibar leo
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini walishiriki katika ibada ya kumuombea marehemu Abeid Amani Karume katika kaburi la muasisi huyo huko Kiswandui,Zanzibar leo. 

Baadhi ya Wananchi wa Zanzibar walohudhuria ibada ya Kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amaan Karume iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar leo katika kuadhukisha Karume Day. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. JK is a very simple man, hebu angalia kashikilia mwamvuli wake hana noma wala nini.
    Ingekuwa ni viongozi wengi shurti mwamvuli ushikiliwe na mlinzi.
    Big up JK, huna makuu youu are real down to earth!

    ReplyDelete
  2. Waliobuni siku hii nawafagilia. Pia tunaweza kuanzisha ya Marehemu Mwalimu JKNyerere.

    ReplyDelete
  3. jamani mambo gani hayo rais anabeba mwenyewe mwanvuli?

    ReplyDelete
  4. samahani mimi bado kijana mdogo, Karume aliuwawa na nani ?

    ReplyDelete
  5. Waliobuni siku hii nawafagilia. Pia tunaweza kuanzisha ya Marehemu Mwalimu JKNyerere.

    Mdau uliyetoa mada hiyo hapo juu kwa faida yako na kukumbusha kuwa hakukuwa na Karume Day tangu alipoaga dunia ni mpaka pale ilipoanzishwa Nyerere day ndiyo ikaonekana haiwezekani kuwepo bila ya Karume day. Kwa hiyo Nyerere Day ni Oktoba 14 (sasa na siku aliyoaga dunia.

    ReplyDelete
  6. jamani mambo gani hayo rais anabeba mwenyewe mwanvuli?

    Hiyo ni ishara wazi kuwa JK hapendi kutetemekewa nadhani kama siyo itifaki, basi JK tungekuwa tunakatishana nae mitaani au kwenye Njenje kama kama ada.

    Nahisi anai-miss Njenje, kijiwe cha kahawa mtaa wa Dossi

    ReplyDelete
  7. ok poa tu

    ReplyDelete
  8. wewe unaejidai kuwa ni mdogo kwa nini usisome vitabu vya historia ukajuwa alemua karume au unataka kuanzisha mjadala mbaya hapa? aste aste, kuna alofyatuwa risasi iliyomua karume, kuna waliopanga kumuua karume na walioshiriki katika mpango mzima wa kumua karume, na kuna ...... ah nikisema hapa post hii haitoingia ukumbini

    ReplyDelete
  9. We unaejiita kijana mdogo ipo siku utakuwa mzee kama mimi hivyo mdomo wako uuweze, maana waweza tamka neno hapa ukaamsha hisia za watu bure hapa jamvini. Ni hiviiii Abeid Amani Karume raisi wa kwanza wa Afro shirazi aliuawa na bwana mmoja anaitwa Humudi ambae siku ya mauaji alienda hapo kiswandui wakati wa jioni raisi huyo akipenda kucheza bao na rafikie bwana Thabit Kombo/Thabeet mnavyoita nyie wa leo ghafla bwana yule aliingia na sub-mashine gun na kumpiga jemedari wetu huyo risasi tatu kifuani akafia hospitali, nae muuwaji alimiminiwa risasi zisizomithikika na walinzi akafa palepale, nadhani nimejibu swali lako ila usiniulize zaidi ingawa nilikuwa mdogo kuliko wewe yalipotokea hayo.

    ReplyDelete
  10. Asante kwa mara ya kwanza nimemuona mama mzazi wa Rais wa ZANZIZABAR pia nimebahatika kumuona mama watoto

    ReplyDelete
  11. MAMA KARUME HANA MAKUU MAANA HASIKIKI KAMA WAMAMA WENGINE.NDO NAJUA LEO KAMA YUPO

    ReplyDelete
  12. Nini kizuri zaidi kusherehekia maisha yako (siku) ya kuzaliwa kwake au kusheherekea siku ya kukufa kwake (majonzi)?

    ReplyDelete
  13. mkuu umechemsha mama shadya amesimama kushoto na sio kulia kama ulivyonukuu

    ReplyDelete
  14. mama karume hana makuu, well tuulize sisi wazanzibari, labda haonekani kwenye magazeti na media zote lakini tuliopo visiwani tunajua makali yake. sisemi mengi

    ReplyDelete
  15. wahusika wakuu wa plot nzima ya kumuuwa karume wanajulikana kwani walitajwa na watuhumiwa waliokiri makosa, lakini kwa sababu ya links zao na vyeo vyao hakuna aliethubutu kuwafikisha mahakamani. wazanzibari sote tunajuwa hilo!!!!!

    ReplyDelete
  16. LONG LIVE HUMUDI'S MEMORY (RIP)

    ReplyDelete
  17. sasa jamani mlotuandkia habari hii, hebu tuambieni amani kawa dk tangu lini? izo sifa nyengine km hamna uhakika nazo msiziandike

    ReplyDelete
  18. Hivi ni kwamba tunapenda ufu au uhai??? Inaonekana tunapenda sana kushabikia wafu. Ni kwa nini tukumbuke siku aliyokufa?? Je isingekuwa jambo zuri kukumbuka siku alipozaliwa na kuenzi maisha na kazi aliyoifanya Duniani??!!
    Hainiingii Akilini kabisa??
    Labda mtu anisaidie hapa.
    Mzawa!

    ReplyDelete
  19. hii habari ya kubeba mwamvuli mh jk ameiga kwa obama nimemshuhudia mwenyewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...