Habari kaka Michuzi,
Leo napenda kugusia kidogo tu juu ya adha na taabu tunayoipata wazawa wa nchi hii juu ya mgao wa umeme.Kama mwananchi wa kawaida na mzawa nasikitishwa na suala zima la mgao wa umeme lakini kwa kuwa inabidi hatuna haja kuvumilia.
Kinachonikwaza katika ‘wito huu’ nipale kuonekana kwa dhahiri ‘upendeleo’ au ‘uonevu’ wa baadhi ya maeneo.Tunaelewa mgao umetangazwa kwa masaa yasiyozidi manne (kama sijakosea),ila kuna maeneo tunakatiwa kwa zaidi ya masaa kumi na mbili kwa siku na kila siku.Wakazi wa Mikocheni viwandani,coca cola,avocado na Kawe ni waathirika wa ‘vitendo hivi vya makusudi’.Imagine umeme unakatwa saa nane au tisa usiku na kurudishwa kesho yake saa nne au tano usiku.Maisha yetu yanakuwa mashakani na vitendo vya uharifu,vyakula tulivyojihifadhia kwa vijisenti vyetu vya manati vinaharibika,tunashindwa hata kunyoosha nguo asubuhi,simu hazina charge na karaha kadha wa kadha…!
Kwa kweli tunaomba yeyote alie na ukaribu wa wahusika wakuu tanesco (Msasani au HQ) watufikishie ujembe wetu,maana tunaumia sana kwa huduma mbovu na zisizokidhi haja na zenye kutia aibu.
Tafadhali usiweke jina wala anuani yangu ila naomba ujumbe wangu uweke hewani,tusaidiane kukomesha baadhi ya adha zinazotusumbua wapiga kura.
Natanguliza kwanza shukrani.
Mdau Mikocheni
KAKA MICHUZI HIZO NI KAMA BREAKING- NEWS KWANGU HAPA NILIPO,MANAKE NILIZANI ZILE STORY ZA DR RASHID WA TANESCO ZILIKUWA NI MIKWARA!NILIKUWA NA MPANGO WA KURUDI BONGO KUANZA MAISHA BAADA YA KUMALIZA MAMBO YANGU HUKU NILIPO LAKINI NAONA TU AFADHALI NIGAILI KABISAA!YANI KWA MTINDO HUO BONGO SIJI MPAKA 2010 MUNGU AKIPENDA!INAUMA SANAA,NAHISI KAMA NAMIMI NDIO HUYO JAMAA ANAYE LALAMIKA AISEE,DAAA BONGO KWELI TAMBARALE.
ReplyDeleteWiki iliyopita mii nimekosa umeme kwa siku tatau mfululizo maeneo hayo hayo ya Kawe. Sasa saa 4 kwa siku na siku tatu kwa wiki.....wapi na wapi.Au kwa sababu mitambo ya Dowans haikununuliwa?
ReplyDeleteLakini takwimu nilizosoma leo kwenye Daily News zinasema mahitaji ya juu kabisa (peak demand) 782 megawatts, uwezo mkubwa kabisa wa kuzalisha wa TANESCO ni 570 megawatts. Na uwezo wa mitambo ya ni 40 megawatts. Kwa hiyo hata ingenunuliwa mbona kungekuwa na nakisi bado ya 122 megawatts wakati wa peak demand? Kwa hiyo ilikuwa ni porojo tu kwamba tukinunua Dowans mambo yatakuwa mswanu!!
Lakini kuna matatizo ya msingi ya kiutendaji hata tukiacha uwezo wa Tanesco kuzalisha. Kwa nini ichukue siku tatu kumrudishia mtu umeme wakati akiangalia majirani zake wanapata umeme- japokuwa kwa vipindi?
Acheni komplain nyie-- Bongo Tambarale bwana.
ReplyDelete....hivi kuna sababu gani ambayo inaifanya tanzania isiwe na umeme tegemezi??naona kila kitu hapo tanzania ni shida tu!maji ya uhakika hakuna,umeme wa uhakika hakuna,hospital huduma mbovu,jiji la dar chafu,hivi kipi WADANGANYIKA tunakiweza??!!mvua ikinyesha mjini mpaka uswazi hakupitiki sababu hakuna mitaro,kinachokera zaidi viongozi wanashtuka pale tatizo linapotokea,YAANI VIONGOZI WA BONGO WANA MATATIZO YA AKILI,mimi niko unyamwezini napumua hewa safi mwaka wa kumi sasa,POLENI SANA WADANGANYIKA INCLUDING MY FAMILLY.
ReplyDeleteBONGO HIYOOOOOO TAMBARAREEEEEEEE. UMEME MCHEZO. GESI MNAZALISHA, MAJI BWELELEEEE TATIZO KILA MTU ANATAKA MASHINE MBOVU ILI WAPATE ULAJI. UKEREWE AKHAAAA...BWELELEEE UMEME MPAKA VICHOCHORONI NA GESI WANAODA UKRAINE...HUKU NDIYO TAMBARAREEEEEE
ReplyDeleteNgoja niwape machungu yangu ya hao jamaa wa TANESCO MSASANI.Siku moja natoka DODOMA baada ya kumaliza shughuli zangu,nikapa mjini nikanunua ndoo,zile plastic za lita 20 kama nne hivi.Nikaja mpaka KONGWA RANCH(kama unakaribia kwenye mpaka wa Dom na Moro) nikachukua nyama kibao kwenye hizo ndoo.Hao jamaa wanasifika maana wana Bucha moja tu hapo mjini lipo opp na TOTAL(HQ),mtaa wa Nkruma nadhani.
ReplyDeleteBasi kufika nyumbani,kama kawaida yetu wazawa,nikagawa karibu mtaa mzima na kwa ndugu na jamaa wengine nami nikabagiwa na akiba kidogo ya kutumia kwa siku chache zijazo.Kutahamaki usiku ule umeme ukakatika gafla,yaani nilikua nimelala lakini mawazo yangu yakaenda kwenye nyama moja kwa moja.Nikaendelea kulala nikidhani kwamba ni mji mzima kumbe kuna line mbili zinazokuja kwenye eneo letu ndo zimekorofisha.Nikawafuata jamaa wa TANESCO MSASANI kama mara tatu,achilia mbali kuwapigia simu.Jamaa wapo very smart,they how to fool people/customers,kila ukifika pale wanakwambia gari la mafundi umepishana nalo,limeshakuja huko kwenu,halafu wanakuuliza,kwani hukuliona?ha ha ha ha ha ha ha!!Kumbe hamna lolote.
Sitaki kuwaambia kilichotokea kuhusu ile nyama maana inaniuma mpaka leo kila nikikumbuka......lol!!
Lakini ndyo nyumbanitutafanyaje sasa.
Mkulima-Kijijini Gezaulole.
Nini Bongo sasa , Nyinyi midomo yenu imejaa pilipili na machafu tu, kuwacheka walio Ulaya na America kuwa wasafisha mavi na kulea wazee.
ReplyDeleteBONGO TAMBARARE.
1. ULAYA HAKUNA HAYA
2. WAZAZI HAWATII KUFULI SIMU ZA NYUMBANI.
3. MAJI YA KUJIPIMIA.
4. MATIBABU YA KURIDHISHA.
5.NA MENGINEYO MPAKA 5,000.000.000.
Sasa mnapoanza kuwashambulia walio ulaya angalieni haya kwanza, mvua ikinyesha hata nyumba na mtaa wako mwenyewe haufai, gari lako mwenyewe haliendesheki na mengi tu.
MANENO MEEEENGI.
MPAKA LEO MFANYAKAZI WA BANK ANAWARINGIA WATEJA.
POLISI ANADHANI YEYE NI HAKIMU
BOSI ANADHANI WAFANYAKZI WAKE WA KIKE WOTE NI WAKE ZAKE
MWANASIASA ANADHANI AMESHINDA BAAHATI NASIBU.
WENGINE BADO WANAITA MEREKANI ULAYA
MTU AKIANGALIA MOVIE KWENYE TV ANASEMA ANAANGALIA SINEMA
NK.
WENU
Pole sana, tumeyataka wenyewe, na kwamtindo huu tutaishia kulalama. Kumbuka siku ile ulipoingia chumba cha kupiga kura, ulikuwa pekeyako,na kwa moyo safi ukakandamiza, zidumu
ReplyDelete