Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mwekahazina wa SACCOS ya Meli Nne Bi Shamsa Saleh Hilal mchango wa Shilingi Milioni Tano 5m/- kutoka kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa SACCOS hiyo uliofanyika katika Chuo cha Karume, Mwanakwerekwe, Zanzibar, leo asubuhi.Kulia nia Waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha.
Baadhi ya Wanachama wa SACCOS Ya Meli Nne jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar wakimshangalia Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubua huko Chuo cha Karume,Mbweni Zanzibar leo asubuhi.Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Tatu pamoja na viongozi wa SACCOS hiyo.
Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Meli Nne Mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa SACCOS hiyo huko Mwanakwerekwe, leo asubuhi.Katika Hafla hiyo Mama Kikwete aliahidi kuichangia shilingi Milioni Mbili na nusu 2.5m/- Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu
Mama Salma Kikwete awataka wananchi visiwani zanzibar kutokuogopa kukopa fedha benki
Na Anna Nkinda - Maelezo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) amewataka wananchi visiwani Zanzibar kutokuogopa kukopa fedha Benki au katika asasi za fedha ili waweze kuongeza mitaji nahivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Mama Salma aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa siku moja wa Chama cha Akiba na Kukopa (SACCOS) ya Melinne uliofanyika katika chuo cha Karume Mbweni visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema kuwa hakuna nchi iliyoweza kufanikiwa na kuwa na maendeleo Dunia bila kukopa fedha katika mabenki na asasi za fedha.
“Madhumuni ya mkutano huu pamoja na mambo mengine ni kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa kuwaongoza katika kipindi kinachofuata”
“Wosia wangu katika hili ni kuwapima wanachama wenu wanaogombea kwa uwezo, imani na uaminifu wao kama vile mlivyofanya kwa viongozi waliotangulia. Wapimeni viongozi kwa vigezo vya uongozi na si vinginevyo”, alisema.
Akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha ambaye pia ni Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe na ni mlezi wa SACCOS hiyo alisema kuwa SACCOS hiyo ni moja ya SACCOS imara visiwani Zanzibar.
Waziri Kiongozi alisema, chama hicho kimeweza kuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuwa na viongozi wengi wanawake na idadi kubwa ya wanachama wake ni wanawake ambao wamekuwa waaminifu katika suala la utunzaji wa fedha.
“Kinababa si watu wazuri sana katika suala la utunzaji wa fedha ukiwapa kutunza fedha zinaweza kupotea katika mazingira yasiyoeleweka ila kina mama ni wasimamizi na wachumi wazuri sana katika jamii”.
“Nawashauri msifanye makosa ya kuchagua viongozi wengi wanaume kwa kufanya hivyo SACCOS yenu inaweza kuyumba ili kuinusuru ni heri kama mmeridhika na uongozi wa viongozi waliopita muwachague haohao waendelee kuongoza”, alisema
Waziri Kiongozi alimalizia kwa kusema kuwa, ifikapo mwaka 2011 lengo la kuwa na benki ya wananchi liwe limikamilika hakuna sababu ya kusubiri muda mrefu hadi mwaka 2013.
Akisoma risala ya chama hicho Ahmada Hassan ambaye ni mjumbe alisema kuwa wamekuwa tukifuatilia sana SACCOS za Tanzania bara na kuona hatua mbalimbali za maendeleo walizofikia na kujiuliza kwa nini bara waweze na wao washindwe?
Aliendelea kusema kuwa, changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni elimu ndogo ya kuendesha ushirika, mitaji midogo kwa wanachama, gharama za uendeshaji, ufinyu wa vitendea kazi kama printer, computer na photocopy mashine na ujenzi wa ofisi unaoendelea.
“Tunatoa ahadi iwapo tutaweza kukabiliana na changamoto hizi tunaamini kuwa ifikapo mwaka 2013 SACCOS yetu itakuwa ni Benki ya wananchi”, alisema.
Wanachama 620 waliooomba mikopo wamepatiwa kwa kipindi cha miaka mitatu na jumla ya fedha zilizokopeshwa ni zaidi ya milioni mia nne ambapo asilimia kubwa ya waliokopa ni wanawake wanaofanya biashara ndogondogo.
SACCOS hiyo ilianza mwaka 2005 ikiwa na wanachama 150 wanawake wakiwa 123 na wanaume 27 hadi sasa kuna jumla ya wanachama 920 wanawake wakiwa 677 na wanaume 243.


Sasa ndiyo sinema inaanza WAMA chini ya First Lady, UWT chini ya Sophia Simba na BAWATA inarudi ulingoni sijui inarudi Profesa Anna Tibaijuka au sijui anakuja nani. Kama hizi Taasisi zitakuwa zina malengo thabiti mbona tutakula uhondo.
ReplyDeleteNimempenda huyo demu anayesmile na kupunga mkono hewani picha ya kati kati.
ReplyDeleteZanzibar oyeeee! Udumu Muungano.