hivi ndivyo ndio namna wadau wanavyoishi ambapo kufuli ni jiti na hakuna kuibiana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mbona gharama ya tundu la ndege ni kubwa kupita nyumba/ Au ndio mpende ndege wako zaidi yako binafsi.

    ReplyDelete
  2. ndio kwavile bado watu vijijini wana upendo zaidi kuliko wamijini,
    ingawaje umaskini unawarejesha sana nyuma ambao unasababishwa na serikali kwamakusudi kabisa kuwatupa mkono hawa wenzetu wa vijijini,lakini tukubali bado watu pamoja na umaskini walionao bado poa tu,mijini hadi chupi uliyovaliwa tunaibiana,yaani noma

    ReplyDelete
  3. hapo hata mje watu kumi hamuwezi toa hilo jiti.

    ReplyDelete
  4. mzee wa kijiji huyo mtu ogopa maana kwa mtazamo ni jiti mlangoni lakini kwa wataalam hiyo mtambo wa kurusha nyuklia na kuzuia nyuklia hapiti mtu hapo kirahisi.

    ReplyDelete
  5. MICHUZI UMENIKUMBUSHA MBALI SANA MIMI NIMEKULIA HUMO HAPANA JOTO KAMA NYUMBAZA MABATI NA MVUA IKINYESHA HUTAISIKIA,KINGINE MAJI YA KUNYWA HUITAJI FRIJI NA USIPOFUNGA VIZURI KAMA HIVYO UNAPATA HEWA NZURI KAMA UKO UGAIBUNI NASHANGAA KWANINI WATU WANAPOTEZA PESA KWA MABATI UCHWARA?

    ReplyDelete
  6. Hao ndege ndio walinzi.haibi mtu kitu hapa jaribu utoke busha au matende.

    ReplyDelete
  7. lol!
    Funny!

    ReplyDelete
  8. Mwenzetu huyu anaamani kama nini sijui, anachapa usingizi wake mnono mpaka asubuhi. Akitoka hapo anakula nutrition yake safi kabisa maana mchicha wa kuchemsha na njiwa wake wa kuchoma. Haya wenzangu na mimi usingizi hatulali tunogapa kuvamiwa na majambazi, kuubiwa n.k. Chakula mafuta kibao na machumvi, mapresha na madepression hayatuachhi.

    ReplyDelete
  9. Mtu akisoma maoni haya Hatashangaa kuona Tanzania tunateswa na mauaji ya Albino. Tunashindwa kabisa kufikiri nje ya wigo wa juju! Hawa ndio watanzania bwana, na wala haijalishi wamehudhuria madarasa mangapi!
    Hayo ndio makazi na maisha ya watanzania wengi vijijini, hapo hakuna cha mzee wa kijiji wala muazingaombwe. Kama kila siku tunaimba kuwa kuna watu wanaishi chini ya dola moja kwa siku, na bado twashangaa makazi yao, hiyo ni ishara mbaya sana juu ya mustakabali wa ustawi wa jamii yetu.
    Watoto wa Watanzania hao ndio mnaowambia wachangie elimu ya juu bila kujali kuwa wenu mnawapaleka ng'ambo kwa kodi za mazao yao!

    Achane kuigiza na tokeni muijue Tanzania na Watanzania wenyewe.
    Mungu na atusaidie

    ReplyDelete
  10. watanzania bwana sijui wamesoma madrasa mangepi. mbona wanongea tu hivyo hivi.

    ReplyDelete
  11. NYIE WOTE BADO HAMJATOA MAONI, MAONI YA MAFANIKIO HAYO YA VIJIJINI WANAYO MZEE MALECELA NA MAKAMBA WAO HIYO WANAONA NI BONGE LA COTTAGE AMBALO KABLA YA UHURU WATANGANYIKA HAWAKUWEZA KUJENGA. MKUMBUKE MALECELA ALISHAWAHI KUSEMA KUWA HIVI SASA WANAVIJIJI WANAZO SIMU ZA MKONONI KITU AMBACHO KABLA YA UHURU HAWAKUWA NAZO ILA HAKUTUELEZA KAMA HUKO ULAYA HIZO SIMU ZILIKUWEPO LAKINI YEYE ALIJUA SISI NI WAJINGA TUTAJUA KUWA ZILIKUWEPO!

    ReplyDelete
  12. Da! We mtoa maoni hapa juu yangu umenifurahisha na mfano wa Malecela, kweli simu za mikononi zimekuja juzijuzi tu hapa, kabla ya uhuru hazikuwepo. Km vile internet enzi za mwl hatukuwa na vitu km hivyo.

    ReplyDelete
  13. Du hii ni kali, chukulia mfano kenye hiyo nyumba anaishi albino, angepona kweli?

    ReplyDelete
  14. And the dwellers therein are as happy as happy can be. That is what I call stress-free living.

    A lot of people would stress themselves out to try and reach the skies - often in wings of feather and wax and as they draw closer to the sun the feathers start burning, the wax melts and the plunge becomes imminent. We all have got only one life to live unless you believe in re-incarnation...

    ReplyDelete
  15. AAA! YARABI NIMEGUNDUA SIRI NZITO NDANI YA HII PICHA SIRI AMBAYO MICHUZI KAIFICHA, TAZAMENI KUSHOTO YA NYUMBA HIYO MTAMUONA TRAFIKI NYUMA YA NYUMBA AKIONEKANA NUSU YA MWILI, SASA BASI, HIKI NI KITUO CHA TRAFIKI KIJIJINI KWA WILAYA YA MKUU WA NANIHII.

    ReplyDelete
  16. pasafiiii,halafu kila kitu orijino,mwe eh mungu weee maisha kama haya tutayarudia lini tena,hapo mwenyewe hana stress,mawazo wala hata hajui kuna epa,dowans,richmond,lyumba wala mkapa,natamani kama dunia nzima igegeuka tungekuwa na appatment kama hii na maisha kama haya wala leo asingelalamika mtu na finance crisis wala hakuna angemjua obama wala hata vita visingekuwepo

    ReplyDelete
  17. Picha imenikumbusha mbali sana. hari harisi ya kijijini. pamoja na umasikini lakini watu bado wanaishi kwa matumaini sana. kila mmoja ana muheshimu mwenzie na kujaliana. shida ya mmoja wao ni shida yao.
    Lakini wanatakiwa kukombolewa katika hari hii ya umasikini. ingekuwa rasilimali za nchi hii zinatumika vizuri hari hii ingekuwa hadith tu.
    Ila na wenyewe awaoni mbali san kwani uwezi kuwatenganisha na ccm hata lije greda basi kwa mtaji huo watakesha.

    ReplyDelete
  18. na huyo mwizi akakiibe kitu gani humo ndani?

    ReplyDelete
  19. omba dua asije kunguru akakuwekea kaa la moto juu ya makuti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...