
Kuwa wa kwanza kuna raha yake,kuwa wa kwanza katika historia kuna heshima yake,karibuni Washington Dc may 22-may24,MEMORIAL WEEKEND na wewe uwe mmoja wao ya wale watakao kua wa kwanza katika WABONGO REUNION EXRAVAGANZA ya kwanza ndani ya Kapitali yenye rais wa kwanza mwafrika,
mechi ya Netball ya kwanza katika historia,Dc vs out state,
mechi ya kwanza ya Houston v/s Dc ndani ya Kapitali,
Mechi ya kwanza ya Yanga v/s Simba itakayochezwa na Wabongo out state na mechi ya kikapu ya kwanza Vijana,Pazi na Don Bosco.
hii ni historia unayotakiwa uwe wa kwanza kushuhudia.
Karibuni Washinton Dc(Jina kubwa),urushe mikono na kujiachia achia ili mradi si fujo wala patashika bali ni jazba la starehe na burudani litakalo kufanya mchangamfu usiku kucha bila kusahau nyama choma.kwa maelezo zaidi bofya
www.wabongoreuniondc.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...