UONGOZI WA FM ACADEMIA 'WANA NGWASUMA' UNAOMBA RADHI MASHABIKI WAO KWA KUWATANGAZIA KWAMBA KUTONA NA SABABU ZILIZO NMJE YA UWEZO WETU, ILE SAFARI YA KUFANYA SHOO JIJINI LONDON PASAKA HII IMEAHIRISHWA HADI ITAPOTANGAZWA TENA. NIA YA KUFANYA SAFARI HIYO IPO PALE PALE NA PINDI MAMBO YAKIKAA SAWA LONDON WATAIONA NGWASUMA LIVE!
UONGOZI WA FM ACADEMIA PIA UNABA RADHI KWA MAPROMOTA (DIDAS NEW FASHION NA BONGO DJ ENTERTAINMENT) KWA KUAHIRISHWA SAFARI HIYO BAADA YA WAO KUKAMILISHA KILA KITU IKIWA NI PAMOJA NA KUTUMA TIKETI NA VITU VINGINE MUHIMU.

MSEMAJI

FM ACADEMIA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. duuuuu nomaaa ndio mambo ya kiswahili alwayz hayakamiliki.....yote heri hela zetu tutafanyia mambo mengine nishai lakini nime mind.....mdau coventry bj

    ReplyDelete
  2. dah,ndo ivyo tena wadau mambo yameingiliana but msiwe na wasiwasi wana Ngwasuma watatua mjini tu

    ReplyDelete
  3. MZUNGU KASTUKA,kawanyima viza,anajua wote watazamia kwenye utambarare.kaeni hukohuko bongo huku kila siku kirisimasi

    ReplyDelete
  4. WAMEBANA VISA NINI?

    ReplyDelete
  5. hivi hawa wanafikiri pound inachimbwa? kama walitumiwa mpaka ticket, halafu wanaahirisha dakika za mwisho wanafikiria nini? labda kama siijui issue vizuri, wanafikiria safari yao ni Dar Mwanza? wanadhani mtu kujiandaa ku-host group UK, ni porojo? poleni mliowandaliia safari, japo msikate tamaa! na nyie Ngwasuma get ur life and program sorted out sio kusumbua watu.

    ReplyDelete
  6. Kwa masharti ya kuingia uingereza yalivyo toka mwanzo nilikuwa na mashaka kama watapewa visa.

    ReplyDelete
  7. Gharama za kuja huku MBINGUNI si mchezo ati!!
    Na Ma-promoter dizain za KUGONGEA FEGI ni lazima hata VISA zitakuwa mzozo.
    Jitahidini tu lakini muweze kuona maisha ya huku HAERA..
    Ila msilete za Kibongo bongo MKAZAMIA huku:))

    ReplyDelete
  8. Mimi nilijua kua sio rahisi kwa wa congo kupata visa ya UK kupitia tiketi ya kuiwakilisha Tanzania,ni vigumu,maana ngwasuma asilimia kubwa ni wa congo,na wakija huku hakuna atakae rudi bongo,hamtaki kusema kama wamekosa visa.

    ReplyDelete
  9. huu ni uzushi mtupu! kwa nini msiwe wazi tu kwamba mmenyimwa VISA??? watu tulisha chukua off day kazini, na ukizingatia ni double time, mmetupotezea muda na pesa nyingi saana. wakati mwingine msitangaze shoo kabla ya kupata pasi za kuingilia nchini (visa) huu ni upotoshaji na kukiuka misingi ya kazi ( nothing like proffessionalism in you guys)kwani huu uvumi wa nyie kunyimwa VISA sisi huku midlands tumeanza kuusikia tamgu Jumatatu ya wiki hii, iweje mtuambie leo kuwa ziara imeahirishwa????? what a short notice????????????? wakati mwingine mtapoteza wapenzi kwa sababu za ubabaishaji uliokubuhu kama huu!!! ngwasuma!!! ngwasuma! kumbe wababishaji tu!!!--- MUMEKULA BAMIA SASA MUNATELEZA!!!

    MDAU WA MSONDO!!!! EAST MIDLANDS

    ReplyDelete
  10. viza au?

    ReplyDelete
  11. duh naona visa zimekua mgogoro sasa.polenio saniii

    ReplyDelete
  12. Ngwasuma wameomba samahani kwa mashabiki na mapromota...huu ndio uungwana. Safi sana, ratiba ilikuwa imebana sana pasaka hii nisingeweza kuja kuwaona live ila kwa hili next time mkija nitakuwa ndani ya nyumba.

    ReplyDelete
  13. nilishahisi toka mwanzo hawa si watu wa kuja huku uk. wangerudi wawili tu bongo halafu lawama zingekuwa kwa nani,dida au balozi? lakini hakingeharibika kitu kama wangezamia,kawalee na makuta wangelamba dume.wangepata kazi bila work permit kina nyoshi!!!

    ReplyDelete
  14. Nilijua mapema that there is no way Ngwasuma wanaweza kukubaliwa kwenda nchi yoyote ya Ulaya, kwa sababu robo tatu yao wasingeweza kurudi. Hawakupata VISA ndiyo sababu ya kufutwa safari na wala wasiseme imeahirishwa ni kwamba haiwezi kuwepo tena

    ReplyDelete
  15. Kwani hiyo bendi ya FM Academia wana wa Ngwasuma hawana wanamuziki wa Kitanzania au nchi nyingineyo mbali na CONGO/ZAIRE ili waje kutupa raha huku ulaya kama wenzao wa Twanga PEPETA walivyokuja mwaka juzi? Ni ukweli wacongo hawawezi kurudi

    ReplyDelete
  16. Ha ha ha Mapoto Malili, Africa moto. MZAIRE HAWEZI KWENDA ULAYA AKARUDI AFRIKA.
    Hayo maneno juu yana maana philosiphy ya Mzaire au Mkongo ni kwamba Ulaya(Mapoto) kuna baridi lakini Afrika ni Joto(Moto). So ni bora ufe kwa baridi ya Ulaya kuliko moto wa Afrika. Duh! Asingerudi mtu hapo

    ReplyDelete
  17. Wamenyimwa Visa Nini?

    ReplyDelete
  18. WATATUA KWA UNGO AU BI NYANKELA AU KIPEPE! SI MPAKA...VISA MCHEZO

    ReplyDelete
  19. aah yani nilikuwa nimejikoki kiukweli kucheza njiwa na samaki ana vipande vingapi, yani kesho ilikuwa huyooo ndani ya reading ili niwaone j2! mbona miyeyusho jamaniiii? daaaah!!!!!!

    ReplyDelete
  20. Kichwa, tumbo na Mkia...Chezesha Mukia..ohhh lol tumekosa uhondo..!!??

    ReplyDelete
  21. bora haijawa manake ilishakuwa mambo ya aibu. huku uk kina dada wa kibongo nasikia walishaanza kugombana kisa wanapoenda bongo wana share hao mabwana wa ngwasuma.wengine mashoga wa karibu na wengine nasikia ndugu kabisa lakini ndio kwa kutaka umaarufu na kuimbwa jukwaani inakuwa hawana jinsi. WHAT A SHAME!!!!

    ReplyDelete
  22. TEACHER, DENMARKApril 12, 2009

    HAKUNA CHA AIBU WEE ANONYMOUS WA APRIL,11,2009. HAWA NGWASUMA NI MASTAA NA KAWAIDA MASTAA DUNIA KOTE WANABABAIKIWA HATA LAST YEAR HAPA DENMARK MWANA MUZIKI MMOJA ALISHINDA KWA KUIMBA ANABABAIKIWA KWELI NA VISICHANA VYA KIZUNGU ANGALIA HATA MASTAA WA MAREKANI WANVYOBABAKIWA NA WANAWAKE KISA WABONGO NDO UNAKASHFU, SAWA SAWA LAKINI TUSEME UKWELI HAWA JAMAA WOOOTE NI MAHANDSOME WAZEE WA PAMBA, WAZEE WA BLING BLING ACHA WANAWAKE WAJIUE MWEEEE... SIO WOTE WANAOPENDA NGWASUMA WANAWATAKA NGWASUMA WAKIKUJUA TU WEWE NI MSHABIKI WATAKUIMBA TUU KUNAWANOIBWA MBONA HATA HAWAJAWAHI KUWA MABWANA ZAO NA MMJOWAPO NI MIMI MSHABIKITANGU MWAKA 1996 MPAKA LEO HII NGAWSUMA KWANGU NI DAMUUUU "ANY WAY WATAKUJA TU TUTAWAONA HAWAWEZI KUINGIA MITINI HII TRUPS INAYOKUJA SIO YAKUINGIA MITINI KWANZA HIZO SCANI ZA MACHO NA VICHWA, NAWACHUKUA MPAKA VIDOLE, ACHENI KUWAKATISHA TAA MAPRODUCER ACHENI WIVU KUWASEMA WAKONGO MBONA WATANZANIA KIBAO MMEZAMIA HUKU TUMEJAA KILA KONA MPAKA TUMEFUNGUA MATAWI YA CHAMA,BALOZI WANYUMBA KUMIKUMI,KARIBU TATACHAGUA RAHISI NA WAZIRI ULAYA DUU!!!!!JINSI TULIVYO WENGI!!!! ACHENI KUONGEA YASIO WAHUSU

    ReplyDelete
  23. We dada unayejiita teacher sijui uko Demnark, mbona unatoka kwenye mada yenyewe na kumuonea anony wa 11/2/09. Hakuna anayebishia uzuri, pamba au mkorogo wowote hapa. Mada ni kwa nini hawakwenda. Hawajatoa sababu za kuridhisha ndiyo maana watu wana conclude wamenyimwa VISA. Kwani wamekiri kuwa Mapromota wao walikamilisha kila kitu including tickets. Sasa kwa nini wasiende. Ukweli ni pale pale, wamenyimwa VISA kUHOFIA WATAZAMIA. Wabongo unaowasema wamejaa huko wao walipata VISA kwa kuwa waliaminika from the begining na wanafanya kile walichokifata. Sasa hawa ndugu zetu wa jirani hawaaminiki hata kabla ya kupanda ndege yenyewe. Unachobisha ni kipi sasa?

    ReplyDelete
  24. Kinshasa Moto, Africa Moto, Mapoto malili, moto, moto, moto. Dah anonymus mmoja juu kati kati kanikumbusha enzi za niaka ya tisini nikisoma Cardiff, za rap ya Kofi Olomide ya huo wimbo wake akiimba, moto, moto, Kinshasa moto, Mapoto Malili, moto, moto tiri tiri tiri, eenh. Halafu inafuatia sauti nzito ya mzee mzima Kofi Olomidee

    ReplyDelete
  25. TEACHER, DENMARKApril 13, 2009

    KISICHOELEWAKA NINI???? TANGAZO LIKO HIVI ""KUTOKANA NA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WETU ILE SAFARI YA KUFANYA SHOO JIJINI LONDON IMEAIRISHWA"" NA WAMESEMA MAPROMOTA WAO WALISHALIPA MPAKA TICKET ZA NDEGENA MAMBO MENGINE MUHIMU"" BADO MTU ATAKAKUJUA KUWA WAMENYIMWA VISA TANGAZO LINA JIELEZA.

    ReplyDelete
  26. mdau wa 3;30 apr 13 ujue hii bongo. watu wamechoka na matapeli.

    ReplyDelete
  27. Duh! Mdau hapo juu na wewe unachemka au hilo tangazo lenyewe hujalielewa. Katika mambo muhimu yaliyokamilishwa na Promota VISA si swala la PROMOTA. VISA ni swala la muombaji VISA ambao kwa mantiki ilivyo hapa ni wao FM Academia ndio waombaji VISA.Kama umewahi kusafiri ukiangalia kwenye Application form, muombaji VISA ni msafiri na siyo aliyekualika. Sasa ni katika hizo application forms za visa,ambazo baada ya kufika Ubalozi wa UK, walipogundua hawa jamaa karibu wote ni Wa Congo na hapo bongo ukazi wao una utata kwa kuwa wengi wao walionekana kupatiwa residency permits hivi karibuni tuu, ikazidisha mashaka ya ukazi wao bongo. Habari ndiyo hiyo

    ReplyDelete
  28. TEACHER WA DENMARK inapnekana wewe ndito hujaielewa hiyo cinema. Kwanza waliopaswa kutoa taarifa ya safari kuahirishwa wangekuwa ni MAPROMOTA WENYEWE na siyo FM ACDEMIA. Baada ya FM kuatambua wamechemsha swala la VISA wakawahi kujihani mapema kwa kumsifia promota kuwa katimiza kila kitu. Hapo ina maana tatizo ni wao FM wamekosa sifa za kwenda Ulaya ndiyo maana wamenyimwa VISA. Kama huamini waalike wewe huko DENMARK kwako uone kama watapewa VISA na mtu. Cha msingi wewe nenda Bongo utafurahi nao sana pale Makumbusho NA SI NCHI YOYoTE YA ulaya.Pole

    ReplyDelete
  29. HIVI DADA TEACHER WA DENMARK, UKIWA NI MMOJA WA WAPENZI WAKUBWA WA NGWASUMA TOKA 1996, KAMA ULIVYOJISIFIA, INGAWAJE UMESAHU TUU KUWA 1996 HAKUKUWA NA NGWASUMA HAPA BONGO. KWA TAARIFA YAKO NGWASUMA IMEANZA KUWEPO HII MIAKA YA 2000 NA KITU. WEKA RECORDS ZAKO SAWASAWA KAMA KWELI WEWE NI TEACHER

    ReplyDelete
  30. DUH WATANZANIA JAMANI KWA ROHO MBAYA????HIVI TOKA LINI MKAWA NA UPEO WA KUELEWA MAMBO????MNAPENDA KURUKIA TRAIN KWA MBELE?????SASA ALIYEKWAMBIA HAWA JAMAA HAWAJAWAI KUPIGA SHOW NJE YA BONGO NANI???
    HAU NYIE NDO WALEWALE!

    ReplyDelete
  31. TEACHER DENMARKApril 14, 2009

    HAPANA SIKUBLIANI NA WEWE UKISEMA MTINDO WA NGWASUMA UMEKUJA JUZI LAKINI KAMA KUSEMA NAWAJUA TANGU 1996 NIKIIMANISHA TANGU ENZI ZILE ZA KINONDONI WAKIJULIKANA KAM "FM ACADEMIA"" WALIKUWEPO KABLA YA HUO MWAKA 2000 HAPO NITAKUBISHIA MPAKA ASUBUHI. KUHUSU SAFARI SINA COMENTS TENA HII NI BAINA YAO NA HUYO ANAYE WALETA NA UBALOZI SISI NI ILKUA KUJITAYARISHIA HICHO KIPOUND 20 TU TUWAONA WAZEE WAFUNIKA BOVU,BLING BLING,WAZEE WAKOGA,aka WAZEE WA PAMBA HAWAJAMAA PIGA UA NAWAKUBALI

    ReplyDelete
  32. TEACHER DENAMARKApril 14, 2009

    DUUU SORRY NIMESAHAU KUKUJIBU WEWE WA 9.47, APR 13. KWENDA BONGO NAENDA MARA KWA MARA NAJUA SEHEMU ZAO ZOTE WANAZOPIGA WATAKAO WAFURAHIA NIWALE AMBAO HAWAWEZI KUTOKA NA NAHAWAJAWAHI KUWAONA LIVE!!!!

    ReplyDelete
  33. nendeni congo mkachukue visa sio tz
    Ubalozi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...