Haya ni mabasi yanayotoa huduma kati ya Kituo kikuu cha Mabasi na Train cha KL Central kwenda uwanja wa ndege wa LCCT hapa Malaysia. Air Asia ni wadhamini wa Manchester United na mabasi yao yote yamepambwa na picha za Manchester ambao wanaanza ziara ya Asia hivi karibuni na watakuwa Malaysia tarehe 18 July kwa kiingilio kati ya 15,0000/- na 100,000/-. Kazi kwenu wadau pakulala papo nauli yako tuu.
Dege la Air Asia ikiwa imepambwa kwa picha za Manchester United ikiwa uwanjani LCCT kabla ya kuruka kwa safari zake za ndani na nje ya Malaysia. air Asia ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Manchester United.Mambo haya na mengine ya kimichezo na burudani yanapatikana http://spotistarehe.wordpress.com/


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2009

    hicho kiingilio kiko in terms of Tsh, USD, Pound, Euro, Ringgit au? Pls clarify

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2009

    SASA WE MDAU HAPO JUU KWANI HUJUI NAMBA YA PESA IKIFUATIWA NA /- AU /= INAMAANA NI SHILLING HUJAENDA SHULE AMA? EBOOO

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2009

    May 28, 2009 12:47 PM matatizo yako ni makubwa.unajua lkn unajifanya hujui. US$ 150,000? or RM 150,000= 35m tshs/=

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2009

    Jamani kwani kuuliza ni ujinga? mbona unajibu kwa shari? kuna vitu vingine havifundishwi shule au huenda shule zinatofautiana.Wengine tumesomea chini ya mwembe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2009

    Unajua mtu anapo uliza swali kutaka kujua kama unalo jibu la kumuelimisha fanya hivyo na sio kumpa majibu ya kashfa shule na uelewa wa mtu tunatofautiana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2009

    kweli nakubaliana nanyi kwamba uwezo wa mdau kufikiri ni mdogo sana.
    hizo ni fedha za kitanzania, na pia uweunajaribu kuangalia currency exchange rates japokuwa huzitumii,ukiwaunapita barabarani soma mabango ya bureau de change au kwenye home page ya yahoo hapo juu click finance and then exchange rates utapata updates zote.

    May 28, 2009 8:48 PM

    ReplyDelete
  7. Baba UbayaMay 29, 2009

    huyo mdau aliyeuliza kuhusu clarification mnamuonea bure.sasa hiyo 15,0000/-(4 zeros) nayo ni vipi?au naye hakwenda shule?
    sometimes ni vizuri kutoa jibu kwanza alafu ndipo zianze kashfa.wakati mwingine kwa baadhi ya watu ni ngumu kutofautisha kati ya manyunyu na mvua.ama jua na mwezi,ingawa inaweza kuwa usiku ama mchana.pia sometimes utata wa swali huwa haviendani na elimu kwani wakati mwingine mtu hurukia kuuliza swali bila kutafakari ya kile akiulizacho haswa.na pia sio wote wajuao kusoma ama kuandika wanajua alama hizo za tshs.

    kumbukeni ktk kunde la panzi,"Baranguru" hakosekani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...