ni usiku wa manane maeneo ya mataa ya barabarani karibu na kanisa la mtakatifu peter jijini dar wakati shangingi linakata kona kwa kasi na kuelekea kunako jengo lenye maduka ya biashara.....
mara mshindo mkuu unasikika na kuangalia shangingi hilo limeshaparamia ukuta wa vioo wa duka la honey's furniture
dereva wa shangingi anafungua mlango na kutoka unyoya, ufunguo akiwa kauacha mahala pake. inasemekana kakimbilia kituo cha polisi cha oystebay kilicho jirani kujisalimisha. anaonekana hajajeruhiwa na mlinzi anayekaa hapo nje kwa bahati hakuwepo sehemu hiyo. mwenye duka na wapita njia wanafika, na landrover za break-down zinawasili. globu ya jamii inaondoka mahali hapo kukiwa na amani na mwenye duka anasubiri polisi wafike waanze kazi. ni siku ingine ya hekaheka za jiji la dar nyakati za usiku imeshapita...



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2009

    Du nawe michuzi hulali?usiku wote huu na kamera yako ulikuwa unatafuta nini?angalia utapewa talaka na my naniiii wako,na jana tu umetoka vekesheni,tehe tehe tehe tehe.nice job keep it up

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2009

    nDUGU WADAU HII NI HATARI SANA

    HEBU ONENI HII LINKI

    http://jamiiforum.blogspot.com/2009/05/freeman-mbowe-fisadi-papa.html

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2009

    Matatizo ya leseni za kuletewa nyumbani hayo!

    Dereva aliyepitia mafunzo hawezi kuleta ajali ya kijinga namna hiyo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2009

    Mi naona umekosea, tatizo hapo si leseni, nafikiri ni pombe tu ukizingatia muda wa ajali yenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...