
Habari za vekesheni Nanihii wa Naniliii.?
Ni matumaini yangu kuwa wewe pamoja na Nanihino wa Nji yetu hamjambo huko Nonihino.
Wadau mimi nimenunua gari toka Japan, na nimeifurahia sana.
Hii gari imefungwa muziki toka hukohuko Jepu, na ngoma inaonekana ina vitu kibao. Tatizo langu ni kuwa sijaweza kuitumia kisawasawa kwa sababu imeandikwa Kijapan kwa sehemu kubwa.
Wadau mimi nimenunua gari toka Japan, na nimeifurahia sana.
Hii gari imefungwa muziki toka hukohuko Jepu, na ngoma inaonekana ina vitu kibao. Tatizo langu ni kuwa sijaweza kuitumia kisawasawa kwa sababu imeandikwa Kijapan kwa sehemu kubwa.
Sasa naomba msaada tutani kwa;
1. kama kuna jinsi ya kubadilisha lugha (kuweka kimatumbi au kiingilishi)
2. kama kuna mtu ana kijitabu cha maelekezo ya jinsi ya kutumia redio hiyo (MULTI AV STATION model No. NCN-D53 76014) inafanana na hiyo hapo kwenye picha
Nimejaribu kutafuta kwenye mtandao (tovuti) bila mafanikio, zaidi nimekutana na wadau kibao wa Urusi ambao nao wamegongwa na hii ishu.
Shukran
chiggs_2000@lycos.com
chiggs_2000@lycos.com
Nenda kwa google utaipata.
ReplyDeletekaka hongera kwa kununua mchuma! hata hivyo kaka ninakushauri ubadili tu hiyo redio maana hamna jinsi! labda usailiane na BAKITA au TUKI watafsiri! vinginevyo wasiliana na ubalozi wa japan TZ kwa msaada tutani!
ReplyDeleteww mdau chiggs nawe ni mzushi.Hata kipofu anaweza kuona kuna panel kadhaa zimeandikwa kwa kizungu cha Uk hapo lazima patakuwa na jinsi ya kubadilisha.After all vitu vingi vyatengenezwa vikiwa na maelekezo ya kizungu cha uingereza.Sema lugha ya mazeruzeru haipandi LOL
ReplyDeleteNakushauri nenda ktk embassy ya Japan mahali ulipo waombe wakutafutie address ya manufacturer uwasiliane naye. Hapa ktk blog hii itakuwa kudanganyana.
ReplyDeletenenda google.com, type swali lako pamoja na model #...utapata kila kitu.....simple
ReplyDeletekama kijitabu cha maelekezo unacho, jaribu kuangalia pictorial instructions itaweza kukusaidia kwa kufuata maelekezo. Mimi nilipata hali hiyo twice na mara zote nilijaribu kufuatisha maelekezo ya picha na kuweza kutumia radio hizo na maelezo hayo hayo ya KiJapan ingawa lugha siielewi hata A lakini ilinisaidia na kuweza kuconfigure radio na kuweza kujua nianze kipi kufanya nini kwa kuwa basics za radio na music player ziko wazi kwa kiingereza kama zinavyoonekana kwenye console
ReplyDeleteinaonekana hio component ni for japan domestic use only au ni kwa ajili ya gari zao za hapo hapo japan.
ReplyDeleteusitarajie kama itakuwa na "bi-lingual" jaribu kutafuta mtu akutafsirie basic uses zake tu nawe ukariri kama kasuku!
pia sina hakika kama TV itafanya kazi huko kwani wenyewe wanatumia NTSC na hapo kama nakumbuka vizuri ilikuwa pal system miaka ile...
goodluck na kifaa na gari lako!
NENDA UBALOZI WA JAPAN MDAU WATAKUSAIDIA BILA WASI WASI.GOODLUCK.
ReplyDeleteDah!, pole sana mzee mwenzangu kwa hili zengewe la lugha. Unatakiwa ubadilishe IC moja (ambayo ndiyo inayotafasiri lugha) uweke ya kiingereza. Tatizo ni upatikanaji wa hizo ICs. Ukinifuata hapo Chuo Kikuu Mlimani, nitakuonyesha hiyo IC husika, halafu ukopi namba zake na kuuiagiza moja kwa moja kutoka Japan; zinatengezwa na Toshiba. Kama una mashikaji huko Tokyo Japan, anaweza kukununulia kwa machinga walioko kwenye mitaa ya Akihabara.
ReplyDeleteMdau
ReplyDeleteUsikonde.
Hiyo inayoonekana ni ramani navigation system ya Japan.
Kwa mambo ya mziki na redio tumia
buttons ambazo zimeandikwa kwa kiinglish (AM/FM/DISC) kwa hiyo unaweza kupata mambo kama kawaida.
Sidhani kama unahitaji kitabu maana mishale inakuonyesha la kufanya.
Jaribu na utupe feedback watu wa tutani.
Madau hapo juu wa chuo kikuu mpe cntact basi akutafute! Mpe mail manake unaonekana unajua halafu umemwacha jamaa kwenye mataa pale Ubungo!
ReplyDeletechiggs niuzie mimi nimeipenda,mi kijepu napandisha kichizi ntakutafuta unitolee hapo
ReplyDeleteMdau
chiggs usipate taabu mtafute Kingwendu Ngwendulile najua kijapani,ofisi sasa hivi hana lakini mara anakutana na wateja wake pale ferry
ReplyDeleteNadhani walio wengi wametoa ufafanuzi mzuri na mimi naongezea kama hivi:
ReplyDelete1. Mbali za na function zilzotajwa, hii ina uwezo pia wa kucheza DVD za navigation system(sio Japan tu) ila ukiwa na DVD ya ramani za Southafrica utaweka, za Europe utaweka. #2. DVD za kawaida itacheza na ndio maana hiyo displya itaonyesha picha
3. TV
4. Ina bluetooth( signals za juu kushota kama mwangwi) ambayo kama simu yako ina blue tooth, unaweza kuziunganisha ili utumia spika za gari kuongelea badala ya headphones au blue tooth headphones.
Ila kam aulivyosema kama menu za hizo functions ni kajapan, badi inakuwa kasheshe ndiyo maana mdau mmoja kasema tupe feedback kwani buttons hizo zimeandikwa kiingereza ila maelezo inawezekana ni kajap.
Kwa hiyo wadau wanosema ocheki kwenye google, nadhani hawakusoma maelezo yako kwani ulishajaribu huko ikashindikana na mimi nimesearch bado ikawa kapa.Ukibonyeza FM
Chiggs, mimi niliyetoa maelezo ya mwisho nilisahau ili:
ReplyDelete1. Ukiweka DVD au CD, utatumia hiyo button ya Track/Tune kutafuta tracks mbali mbali kweney CD
2. Ukibonyeza TV au AM au FM, utatumia button hiyo hiyo kutune, kusearch stattions za Bingo na sio za Japan, hasa FM. Juu na chini kama mishale inaavyoonyesha.
2. Powe button imo mule mule na volume button. Ukizungusha unaongeza au punguza sauti, ukibonyeza ni off au on.
Haya ni maelezo zaidi ya yale nimekupa kwa function ya blue tooth, ambayo ukibonye, itakuuliza -n isearch ? na hap simu yako lazima uwe ume turn on blue tooth function.
Wadau, nakushukuruni nyote kwa michango yenu. hadi sasa nimeshapata mawasiliano na wadau watatu (mmoja kanipigia simu na wawili tunawasiliana kwa email) TUTAKAPO PATA UFUMBUZI WA HII ISHU, TUTAMTUMIA NANIHII AIWEKE KWENYE blog ili wengine wafaidike pia.NASHUKURU
ReplyDeletemdau chiggs, deslam
hivi hapo cha kuangahika ni nini hasa maana we kaka bonyeza chochote utaona kitakachojiri mambo mswano, hivi umekaa siku moja ukajiuliza aliyeanzisha kusoma au kutengeneza kitu alianzaje?? Acheni mambo rahisi rahisi lazima uumize kichwa kidogo, maelezo ya nini...!!
ReplyDeletegari zinauzwa hata kama ya zamani na mabook yake, MANUALS FOR REFERENCES, HATA HIVYO HIYO NI KITU YA KAWAIDA TU BONYE BONYE ITAFANYA KAZI, UNLESS BASED ON PAID SATTELITE THEN KATUPE
ReplyDelete