Mh. Peter Alain Kalaghe Balozi wa Tanzania nchini Canada aliyekuwa Mgeni rasmi wa shughuli hiyo ya uzinduzi akikabidhiwa Katiba ya chama na Mwenyekiti Dr. Zacharia Mandara tayari kwa uzinduzi rasmi.
Mh. Balozi Peter Kalaghe akiwa katika pozi na viongozi wa TAO. Kutoka shoto waliokaa: Bi Eva Mfinanga (Katibu Msaidizi), Mh. Peter A. Kalaghe (Balozi na Mgeni rasmi siku hiyo), Dr. Z. Mandara (Mwenyekiti), Prof. Amos Mhina (Mgeni mwalikwa). Waliosimama toka shoto: Ibrahim Umba (Katibu), Bief MacKenzie (Makamu Mwenyekiti), Raphael Kajubiri (Mwandaaji), John Kalonga (Afisa Uhusiano), na Faraji Jermaine (Mweka hazina msaidizi).

Mh. Peter Kalaghe akitoa hotuba fupi mara baada ya uzinduzi wa chama cha Watanzania waishio Ottawa. Kubwa kati ya yote amekitaka chama kuwa kiini cha vyama vingine vya Watanzania vilivyoko Canada kwa kuwa TAO ipo makao makuu ya nchi.

Kama kawaida ya Watanzania, popote wakutanapo mambo fulani huwa hayawekwi kando. Hapa wadau wakikamata msosi wa nguvu, ukiangalia vizuri utaona pilau kwa mbaliiiii.

Siyo hayo tu, hata mambo ya mduara hayakuwekwa kando. Hapa wadau wakisakata kinyaunyau……yaaani we acha tu, palikuwa hapatoshi.

Watoto nao hawakusahaulika katika siku hii muhimu kwa Watanzania wakazi wa Ottawa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2009

    Hongereni sana ndugu zetu wa Ottawa. Msije mkawa kama sisi hapa Toronto mambo ya kuanzisha vyama 100.
    Umoja ni Nguvu wandugu.

    J.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2009

    Hongera wadau! Nilifikiri ni ufunguzi wa tawi la CCM Ottawa! Naona kale ka movement kako UK peke yake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2009

    Hongereni,

    Lakini kila siku hukaa nikajiuliza inakuwaje hizi jumuiya zilizoko nje zikianzishwa huwa ni watanganyika watupu? Wazenji inakuwaje huwa hawajihusishi. Kuna tatizo gani? siamini kama wazenji hawako huko ughaibuni.Lazima kuna neno. Hebu watambuzi tuambieni.
    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2009

    wazenji ukiwaalika wanakwambia hawataki mambo ya najisi. hakuna watu wabaguzi majuu kama wazenji, shughuli zao hawataki wabara, kwanza wanadai wabara hawajui kupika, hawajui kufukiza udi nk. especially wazenji wanaoishi vitongoji vya washington DC. kuna anayebisha?

    ReplyDelete
  5. Mbona wazee tupu na familia zao tu.. inamaana huko hakuna vijana kama UK...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2009

    nawapongeza sana nyie wadau wa canada nyie ndio wabongo wenye akili hoingereni
    hapo powa sio wale wenzenu wa UK eti tawi la ccm londoni lina maana gani au litawasaida nini

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2009

    Wazanzibari huku ughaibuni wala hawajiiti wa Tanzania; lakini wanatumia pasipoti za Tanzania wakisafiri ua wakizidiwa na matatizo. Inaudhi sana; kwanza hakuna tunachofaidi toka kwao bali wao toka kwetu. Waruhusiwe tu wajitenge na hao waliojazana Dar na kuishi kwenye mansions warudi Zanzibar wanakoogopa ushirikina hivyo wataishi kwenye vibanda.

    J.
    Toronto.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2009

    Bajameni, chonde chonde fungueni matawi ya Chama tuongeze wanachama nje ya nchi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2009

    Ongera sana mzee Umba kwa kuhukwaa Ukatibu.
    Best huo mduara unavyoucheza kibabe mpaka inatisha na hiyo ni moja ya dalili ya utawala wa mabavu. Big Up
    S. frm New Zealand

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2009

    Wazenji tulikuwepo mbona? si lazima tuwe na name tags kuonyeza tunatokea Unguja. Jamani mbona sote ni ndugu tunatokea Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Hongereni wana umoja wa Ottawa. Katibu, Ibrahim Kassim mwana wa Umba, mtaalam wa IFM - Dar,hujambo? Mwanzo nilidhani ni Mike Tyson! Unakula kuku tu. Nadhani sasa ushakuwa mtu mzima utundu umepunguza, umeshakuwa!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2009

    Acha mambo yako mdau wa IFM,hapo juu!mambo ya Umba alikuwa mtundu ni huko huko Ifm,unamvunjia heshima kwa mkewe!mambo kama haya yakuandika kwenye personal emails,siyo hapa!
    Hapa pongezi zinatosha!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 20, 2009

    Nawashukuru sana wa TAO kwa kujituma kufanya kitu cha maana nawasihi msiingize siasa CCM au NCCR lengo ni kujemnga hali za maisha yenu hapo Ottawa.
    Nawapongeza viongozi wote waliochanguliwa kuongoze umoja, najua hakika umoja utaenda mbele.

    Kuhusu wanzenjii kila amtu anahaki ya kujiunga na umoja na kila mtu anauwezo wa kujua ni nini kilicho chema katika maisha.

    Nwapongeza sana mzee Mandara usisahau ulikuwa Mangi, kijenge chama kama uchaggani.

    ReplyDelete
  14. Nawapongeza sana mlioanzisha huo umoja hapo ottawa.
    Napenda kuja kuishi hapo Baadae

    By Deussons Collins

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...