Habari za vekesheni Nanihii wa Naniliii.?
Ni matumaini yangu kuwa wewe pamoja na Nanihino wa Nji yetu hamjambo huko Nonihino.
Wadau mimi nimenunua gari toka Japan, na nimeifurahia sana.
Hii gari imefungwa muziki toka hukohuko Jepu, na ngoma inaonekana ina vitu kibao. Tatizo langu ni kuwa sijaweza kuitumia kisawasawa kwa sababu imeandikwa Kijapan kwa sehemu kubwa.

Sasa naomba msaada tutani kwa;
1. kama kuna jinsi ya kubadilisha lugha (kuweka kimatumbi au kiingilishi)
2. kama kuna mtu ana kijitabu cha maelekezo ya jinsi ya kutumia redio hiyo (MULTI AV STATION model No. NCN-D53 76014) inafanana na hiyo hapo kwenye picha

Nimejaribu kutafuta kwenye mtandao (tovuti) bila mafanikio, zaidi nimekutana na wadau kibao wa Urusi ambao nao wamegongwa na hii ishu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2009

    Nenda kwa google utaipata.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2009

    kaka hongera kwa kununua mchuma! hata hivyo kaka ninakushauri ubadili tu hiyo redio maana hamna jinsi! labda usailiane na BAKITA au TUKI watafsiri! vinginevyo wasiliana na ubalozi wa japan TZ kwa msaada tutani!

    ReplyDelete
  3. ww mdau chiggs nawe ni mzushi.Hata kipofu anaweza kuona kuna panel kadhaa zimeandikwa kwa kizungu cha Uk hapo lazima patakuwa na jinsi ya kubadilisha.After all vitu vingi vyatengenezwa vikiwa na maelekezo ya kizungu cha uingereza.Sema lugha ya mazeruzeru haipandi LOL

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2009

    Nakushauri nenda ktk embassy ya Japan mahali ulipo waombe wakutafutie address ya manufacturer uwasiliane naye. Hapa ktk blog hii itakuwa kudanganyana.

    ReplyDelete
  5. nenda google.com, type swali lako pamoja na model #...utapata kila kitu.....simple

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2009

    kama kijitabu cha maelekezo unacho, jaribu kuangalia pictorial instructions itaweza kukusaidia kwa kufuata maelekezo. Mimi nilipata hali hiyo twice na mara zote nilijaribu kufuatisha maelekezo ya picha na kuweza kutumia radio hizo na maelezo hayo hayo ya KiJapan ingawa lugha siielewi hata A lakini ilinisaidia na kuweza kuconfigure radio na kuweza kujua nianze kipi kufanya nini kwa kuwa basics za radio na music player ziko wazi kwa kiingereza kama zinavyoonekana kwenye console

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2009

    inaonekana hio component ni for japan domestic use only au ni kwa ajili ya gari zao za hapo hapo japan.
    usitarajie kama itakuwa na "bi-lingual" jaribu kutafuta mtu akutafsirie basic uses zake tu nawe ukariri kama kasuku!
    pia sina hakika kama TV itafanya kazi huko kwani wenyewe wanatumia NTSC na hapo kama nakumbuka vizuri ilikuwa pal system miaka ile...
    goodluck na kifaa na gari lako!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2009

    NENDA UBALOZI WA JAPAN MDAU WATAKUSAIDIA BILA WASI WASI.GOODLUCK.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2009

    Dah!, pole sana mzee mwenzangu kwa hili zengewe la lugha. Unatakiwa ubadilishe IC moja (ambayo ndiyo inayotafasiri lugha) uweke ya kiingereza. Tatizo ni upatikanaji wa hizo ICs. Ukinifuata hapo Chuo Kikuu Mlimani, nitakuonyesha hiyo IC husika, halafu ukopi namba zake na kuuiagiza moja kwa moja kutoka Japan; zinatengezwa na Toshiba. Kama una mashikaji huko Tokyo Japan, anaweza kukununulia kwa machinga walioko kwenye mitaa ya Akihabara.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2009

    Mdau

    Usikonde.
    Hiyo inayoonekana ni ramani navigation system ya Japan.
    Kwa mambo ya mziki na redio tumia
    buttons ambazo zimeandikwa kwa kiinglish (AM/FM/DISC) kwa hiyo unaweza kupata mambo kama kawaida.

    Sidhani kama unahitaji kitabu maana mishale inakuonyesha la kufanya.

    Jaribu na utupe feedback watu wa tutani.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2009

    Madau hapo juu wa chuo kikuu mpe cntact basi akutafute! Mpe mail manake unaonekana unajua halafu umemwacha jamaa kwenye mataa pale Ubungo!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2009

    chiggs niuzie mimi nimeipenda,mi kijepu napandisha kichizi ntakutafuta unitolee hapo
    Mdau

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2009

    chiggs usipate taabu mtafute Kingwendu Ngwendulile najua kijapani,ofisi sasa hivi hana lakini mara anakutana na wateja wake pale ferry

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 27, 2009

    Nadhani walio wengi wametoa ufafanuzi mzuri na mimi naongezea kama hivi:
    1. Mbali za na function zilzotajwa, hii ina uwezo pia wa kucheza DVD za navigation system(sio Japan tu) ila ukiwa na DVD ya ramani za Southafrica utaweka, za Europe utaweka. #2. DVD za kawaida itacheza na ndio maana hiyo displya itaonyesha picha
    3. TV
    4. Ina bluetooth( signals za juu kushota kama mwangwi) ambayo kama simu yako ina blue tooth, unaweza kuziunganisha ili utumia spika za gari kuongelea badala ya headphones au blue tooth headphones.
    Ila kam aulivyosema kama menu za hizo functions ni kajapan, badi inakuwa kasheshe ndiyo maana mdau mmoja kasema tupe feedback kwani buttons hizo zimeandikwa kiingereza ila maelezo inawezekana ni kajap.

    Kwa hiyo wadau wanosema ocheki kwenye google, nadhani hawakusoma maelezo yako kwani ulishajaribu huko ikashindikana na mimi nimesearch bado ikawa kapa.Ukibonyeza FM

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 27, 2009

    Chiggs, mimi niliyetoa maelezo ya mwisho nilisahau ili:
    1. Ukiweka DVD au CD, utatumia hiyo button ya Track/Tune kutafuta tracks mbali mbali kweney CD
    2. Ukibonyeza TV au AM au FM, utatumia button hiyo hiyo kutune, kusearch stattions za Bingo na sio za Japan, hasa FM. Juu na chini kama mishale inaavyoonyesha.
    2. Powe button imo mule mule na volume button. Ukizungusha unaongeza au punguza sauti, ukibonyeza ni off au on.
    Haya ni maelezo zaidi ya yale nimekupa kwa function ya blue tooth, ambayo ukibonye, itakuuliza -n isearch ? na hap simu yako lazima uwe ume turn on blue tooth function.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 27, 2009

    Wadau, nakushukuruni nyote kwa michango yenu. hadi sasa nimeshapata mawasiliano na wadau watatu (mmoja kanipigia simu na wawili tunawasiliana kwa email) TUTAKAPO PATA UFUMBUZI WA HII ISHU, TUTAMTUMIA NANIHII AIWEKE KWENYE blog ili wengine wafaidike pia.NASHUKURU

    mdau chiggs, deslam

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 27, 2009

    hivi hapo cha kuangahika ni nini hasa maana we kaka bonyeza chochote utaona kitakachojiri mambo mswano, hivi umekaa siku moja ukajiuliza aliyeanzisha kusoma au kutengeneza kitu alianzaje?? Acheni mambo rahisi rahisi lazima uumize kichwa kidogo, maelezo ya nini...!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 29, 2009

    gari zinauzwa hata kama ya zamani na mabook yake, MANUALS FOR REFERENCES, HATA HIVYO HIYO NI KITU YA KAWAIDA TU BONYE BONYE ITAFANYA KAZI, UNLESS BASED ON PAID SATTELITE THEN KATUPE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...