
Ras Makunja (nyuma) na The Ngoma Africa Band
The Ngoma Africa band,bendi ya mziki wa dansi yenye maskani yake nchini Ujerumani,
imeachia hewani vibao vikali ! mara hii wamekuja na kwa heshima na adabu kwa kuanza kuwasilimia wakubwa hapa nyumbani! kwa kuanza na wimbo Uliobeba jina la "SALAM ZENU" wimbo ambao unachezeka katika kila hali.
Lakini kama kawaida yao wanapofyatua vitu vipya! mtunzi wa nyimbo hizo Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu akuacha tabia yake ya kutoa hoja kwa Jamii kwa kupitia wimbo mpya uliobeba jina "Furaha ya maisha iko wapi?" pia akusita kuomba asamehewe kwa aliyoyakosa kwa kupitia wimbo wa "Unisamehe" kitu ambacho kinatakiwa kufanywa na kila mwanadamu anapojiona kuwa kuna kosa la aina yoyote lazima amombe msamaha!
Nyimbo hizo mpya utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Ras makunja ameimba kwa kushirikiana na mpiga solo Christian Bakotessa aka Chris-B.
Nyimbo hizo mpya ni baadhi tu ya nyimbo zikazokuwamo katika Album yao mpya ambayo itafyatuliwa wakati wowote kuanzia sasa.
Tafadhali usikose kusikiliza kwa kubonyeza hapa.
www.myspace.com/thengomaafrica
huyu ras makunja utafikiri hana hakili nzuri? nimezisikiliza !lakini bado madongo aau mawe yapo pale pale hawezi kuacha tabia yake!
ReplyDeletetena naona safari hii kapoza kidogo kwa hilo song la salam zenu,
lakini naona vijembe vipo pale pale any way naweza kumtaja ni mtunzi mkolofi mwenye uzito wa nguvu ya hoja
kaka bro! ras makunja kulikoni?hapa unaomba usamehewe lakini mbona madongo na mawe bado unarusha?sasa msamaha gani huu wa kupiga masaji kwa mgongo wa chupa
ReplyDeleteunajua kaka ras makunja,mara nyingi kama si mchokozi basi wewe ni mkorofi katika tungo zako!!
ReplyDeletesi unaona wewe mwenyewe jinsi kwa upande moja unawasalimia wakubwa kwa SALAM Zenu! lakini hapo pia unatupa dongo kwa kupambana na Baba yako wa kambo,sasa kama huo sio uchokozi nini ?basi
Ngoma Afrika,kamanda wenu anawaponza kwa kuwachombeza mgombane na baba wa kambo.
ReplyDeleteMkuu kaka ras makunja,hili song la furaha ya maisha iko wapi? mpini na mdundo wake unatisha,tena umesindikiza mawe yako bila uruma
ReplyDeleteBig Up
te!te te wazee wa kazi moto wenu mkubwa teba babkubwa nyimbo zenu nimezipenda kwa kuwa kila nyimbo ina beat yake
ReplyDeletekazeni buti
vipi? FFU hapa naona mnawatishia nyau wenzenu,ongereni sana sana kazi nzuri
ReplyDeletebaba kubwa, vichaa wetu mnatisha huu mziki wenu mkubwa kuliko nyinyi wenyewe,hapa kweli nakubali nyinyi ni mzuka wa dansi.
ReplyDeleteMdau ras makunja bin madongo,hapa kidogo unatuziba midomo !hizi beat!zimekaaje? mziki unasikika kuwa ni wa kitaalamu na unaleta changamoto fulani ya kulirudisha dansi la bongo katika enzi zake?
ReplyDeleteSasa ndio tuseme umedhamiria kuwaziba kuwasha vijana wenzio au??
Kila penye nia pana njia
ReplyDeleteffu hapa mmewasha moto mwingine.Sijasikia bado kesi ya paka aliyewakwapulia mishkaki au hana hatia? maana nyie kila kitu ni song tu sasa hii ya Paka mwizi vipi?
wazee wa kazi mie nauliza hivi?mnalala saa ngapi??
ReplyDeleteunajua hizi mnazopakua zinatuunguza vinywa nakubaki bumbu wazi
vichaa naona mnacheza mchezo mchafu kwa kuwabipu wakongwe,hili song la furaha ya maisha iko wapi? mpini wake umetulia tena unatisha.
ReplyDeletepia mjiwe mikubwa mikubwa inatia uchungu kweli moyoni,wengine hapa bongo wanazo na wengine wanalala njaa! sijui mzee wa vijisenti kausikia ujumbe wenu.
nasikia uzushi kuwa wimbo wa furaha ya maisha iko wapi? umetungwa wakati wafanyibiashara wawili hapa bongo wanachuana? na nyinyi vichaa ndipo mnapopata nafasi ya kutuma madongo yenu?
ReplyDeletehello machizi wetu,mnakubalika kweli nyie wazee wa kukaanga mbuyu,
ReplyDeleteBaaaaab K
kaka bro ras makunja,hivi utaombaje usamehewe na wakati bado unaendelea kurusha madongo tena kwa manati? huu wimbo wako UNISAMEHE umetulia,tena ndani naona umeyataja majina ya wazee la baraza,kina mjengwa ,michuzi n.k,lakini msamaha ni mgumu kwa kuwa libeneke la madongo bado unaliendeleza
ReplyDeletewimbo wa furaha ya maisha iki wapi?
ReplyDeletenimeupenda sana sana,mtunzi kanigusa moyoni.
Mdau wa Uswid