Ras Makunja (nyuma) na The Ngoma Africa Band

The Ngoma Africa band,bendi ya mziki wa dansi yenye maskani yake nchini Ujerumani,
imeachia hewani vibao vikali ! mara hii wamekuja na kwa heshima na adabu kwa kuanza kuwasilimia wakubwa hapa nyumbani! kwa kuanza na wimbo Uliobeba jina la "SALAM ZENU" wimbo ambao unachezeka katika kila hali.

Lakini kama kawaida yao wanapofyatua vitu vipya! mtunzi wa nyimbo hizo Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu akuacha tabia yake ya kutoa hoja kwa Jamii kwa kupitia wimbo mpya uliobeba jina "Furaha ya maisha iko wapi?" pia akusita kuomba asamehewe kwa aliyoyakosa kwa kupitia wimbo wa "Unisamehe" kitu ambacho kinatakiwa kufanywa na kila mwanadamu anapojiona kuwa kuna kosa la aina yoyote lazima amombe msamaha!

Nyimbo hizo mpya utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Ras makunja ameimba kwa kushirikiana na mpiga solo Christian Bakotessa aka Chris-B.

Nyimbo hizo mpya ni baadhi tu ya nyimbo zikazokuwamo katika Album yao mpya ambayo itafyatuliwa wakati wowote kuanzia sasa.

Tafadhali usikose kusikiliza kwa kubonyeza hapa.
www.myspace.com/thengomaafrica

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    huyu ras makunja utafikiri hana hakili nzuri? nimezisikiliza !lakini bado madongo aau mawe yapo pale pale hawezi kuacha tabia yake!
    tena naona safari hii kapoza kidogo kwa hilo song la salam zenu,
    lakini naona vijembe vipo pale pale any way naweza kumtaja ni mtunzi mkolofi mwenye uzito wa nguvu ya hoja

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    kaka bro! ras makunja kulikoni?hapa unaomba usamehewe lakini mbona madongo na mawe bado unarusha?sasa msamaha gani huu wa kupiga masaji kwa mgongo wa chupa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2009

    unajua kaka ras makunja,mara nyingi kama si mchokozi basi wewe ni mkorofi katika tungo zako!!
    si unaona wewe mwenyewe jinsi kwa upande moja unawasalimia wakubwa kwa SALAM Zenu! lakini hapo pia unatupa dongo kwa kupambana na Baba yako wa kambo,sasa kama huo sio uchokozi nini ?basi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2009

    Ngoma Afrika,kamanda wenu anawaponza kwa kuwachombeza mgombane na baba wa kambo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2009

    Mkuu kaka ras makunja,hili song la furaha ya maisha iko wapi? mpini na mdundo wake unatisha,tena umesindikiza mawe yako bila uruma
    Big Up

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2009

    te!te te wazee wa kazi moto wenu mkubwa teba babkubwa nyimbo zenu nimezipenda kwa kuwa kila nyimbo ina beat yake
    kazeni buti

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2009

    vipi? FFU hapa naona mnawatishia nyau wenzenu,ongereni sana sana kazi nzuri

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    baba kubwa, vichaa wetu mnatisha huu mziki wenu mkubwa kuliko nyinyi wenyewe,hapa kweli nakubali nyinyi ni mzuka wa dansi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2009

    Mdau ras makunja bin madongo,hapa kidogo unatuziba midomo !hizi beat!zimekaaje? mziki unasikika kuwa ni wa kitaalamu na unaleta changamoto fulani ya kulirudisha dansi la bongo katika enzi zake?
    Sasa ndio tuseme umedhamiria kuwaziba kuwasha vijana wenzio au??

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2009

    Kila penye nia pana njia
    ffu hapa mmewasha moto mwingine.Sijasikia bado kesi ya paka aliyewakwapulia mishkaki au hana hatia? maana nyie kila kitu ni song tu sasa hii ya Paka mwizi vipi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2009

    wazee wa kazi mie nauliza hivi?mnalala saa ngapi??
    unajua hizi mnazopakua zinatuunguza vinywa nakubaki bumbu wazi

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2009

    vichaa naona mnacheza mchezo mchafu kwa kuwabipu wakongwe,hili song la furaha ya maisha iko wapi? mpini wake umetulia tena unatisha.
    pia mjiwe mikubwa mikubwa inatia uchungu kweli moyoni,wengine hapa bongo wanazo na wengine wanalala njaa! sijui mzee wa vijisenti kausikia ujumbe wenu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2009

    nasikia uzushi kuwa wimbo wa furaha ya maisha iko wapi? umetungwa wakati wafanyibiashara wawili hapa bongo wanachuana? na nyinyi vichaa ndipo mnapopata nafasi ya kutuma madongo yenu?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2009

    hello machizi wetu,mnakubalika kweli nyie wazee wa kukaanga mbuyu,
    Baaaaab K

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 14, 2009

    kaka bro ras makunja,hivi utaombaje usamehewe na wakati bado unaendelea kurusha madongo tena kwa manati? huu wimbo wako UNISAMEHE umetulia,tena ndani naona umeyataja majina ya wazee la baraza,kina mjengwa ,michuzi n.k,lakini msamaha ni mgumu kwa kuwa libeneke la madongo bado unaliendeleza

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 14, 2009

    wimbo wa furaha ya maisha iki wapi?
    nimeupenda sana sana,mtunzi kanigusa moyoni.
    Mdau wa Uswid

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...