mwenyekiti wa muda wa tawi la mashabiki wa manchester united bernard mbwana (pili kulia) akiwa na katibu wake wa muda mh. ngallo (kulia) mratibu wa tawi dennis ssebo (pili shoto) na kaka ray mmiliki wa regency hotel ya msasani kwa mwalimu ambako sherehe hii ilifanyika usiku huu. bahati mbaya tawi limefungiliwa kwa kipigo cha 2-0 dhidi ya barca. poleni
balozi wa uingereza nchini mh. diane corner akizindua rasmi tawi la manchester united dar usiku huu katika hoteli ya regency msasani kwa mwalimu. shoto ni mwenyekiti wa muda wa tawi bernard mbwana na kulia ni mratibu wa tawi dennis ssebo
mashabiki kibao wa manchester united walijitokeza kuzindua tawi na kuangalia gemu usiku huu hoteli ya regency
viongozi wa tawi la mashabiki wa manchester united wakiwa na wageni waalikwa kwenye sherehe hizo ambazo ziliingia dosari usiku huu kwa man yu kupigwa bao 2-0 na barca
mashabiki wakiwa katika hafla hiyo
mashabiki wakisubiri gemu baada ya uzinduzi wa tawi









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 48 mpaka sasa

  1. kwa majonzi au? barca oyeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2009

    watanzania mmekosa kazi na kupenda madaraka naona mtu anaona raha kuitwa "mwenyekiti" wa Manu ni upuuzi kwelikweli na kwa vile wameloose waambie wajiite "Looser umoja"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2009

    Nadhani ulikua mwanzo wa Tawi na Mwisho utakua usiku wa leo,Nani anabisha TUPINGE.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2009

    MICHUZI UNAMWOGOPA MWANAKIJIJI? MBONA UMERUDISHA MAMBO YA WORD VERIFICATION?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2009

    wewe hapo juu,sio looser ni LOSER

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2009

    Duh! hakika meno thelathini na nje yote mbili!Yaani!
    Mitaa sasa itatulia tutafanya kazi kwa raha maana kelele zilikua nyingi sana ooh sie mabingwa wa nini ,ooh sie hatujawahi kuingia fainali tukakosa kombe..nyieee!
    Shukrani kwa Sir Alex Fergason for poor substitution! Yaani alipomtoa Anderson na Park shughuli ikawa rahisi katikati. Ila sio siri huyu Pep Guadiola atasumbua sana miaka ijayo maana alivyoisumbua Man leo, wote walijua Messi atakabiziwa Evra lakini kocha alivyo mjanja kamtumbukiza ndani awe anadrive kuwafuata mabeki huku kina Et'oo na Kichogo wakifungua pembeni na kuwachanganya kabisa kina Vidic na Rio,Shukrani kwa Edwin maana leo wangepigwa ile kiJuma Nature!(3-0).

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2009

    Messi with the heaaadeeeeer! Yeeeeees!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2009

    Ondoa hiyo comment moderator mkubwa inazingua

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2009

    Kamongo natinga kama kawaida.

    Hawa jamaa wamekososa kazi kweli kweli.

    Nikisema sisi tuna akili za kitumwa ninaambiwa nabwata bila misingi. Jamani kama si utumwa mambo leo ni nini?? Usiniambie wanachangishana kukuza tawi. wadau mnisaidie nisije kosea.

    Sasa kuna tofauti gani na hoja aliotoa Kikwete juu ya uraia wa nchi mbili.?? Sisi hatuezi endelea mpaka turekebishe mienendo kifikira na vitendo. Huku anasisitizia wekesheni kwenu huku bakini hukohuko maana hamuezi kula sehemu mbili. Ni upuuzi mtupu. Mbona kuna viongozi wako madarakani na huku wana biashara zao je huko si kula sehemu mbili??

    Ndio haya ya tawi la Man bongo. Yakwetu simba na yanga yanatushinda ndio tutayaweza ya watu.??? Ni utumwa wa kifikira tu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2009

    Tawi lina mkosi sana kwani limefunguliwa wakati wa majonzi 2-0.Nimajonzi na kombe kulikosa pamoja na kufuatilia historia ya kuvaa uuzi wa ushindi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2009

    hizo bia lazma zilawakwama kooni baada ya kipigo walichopata roma leo...hahaaa

    ReplyDelete
  12. Sorry guys, you should have picked another day, may be last week or so to open up this. It will last for rest of your life, it is history people been made. Barcá 2-Manuers-0!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2009

    nyie wanyaturu na wandengeleko ni wajinga au nini?upuuzi gani huo jamani ati tawi la timu ya huko ukoloniland yanawahusu nini nyie wamatumbi wenzangu? na kweli huo upumbavu na ujinga kweli umetuzidi sisi wazaramo na wahaya bila haya yeyote ile!!!labda tuanzishe tawi la kufuta ujinga na upumbavu namie nitajiunga!!!Mungu tusaidie sisi wajinga ila utupatie busara angalau chembe nusu!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 28, 2009

    hongereni kwa kufungwa, sipindi kuwa nie ni wanazi wa ManU ila Watanzania wenzangu mambo mengine tuwe tunaona aibu!!! Mh ati tawi la ManU bongo, jamani mbona hatusikii matawi ya team zetu huko nchi za watu, hata hivyo ndio ushabiki, hongereni maana wengi naowajua mlioko hapo mpira na nyie mbona hamna kabisa!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 28, 2009

    12 facts I know about u MICHUZI
    1. Your reading my comment
    2. Now your saying/thinking thats a stupid fact.
    4. You didnt notice that i skipped 3.
    5. Your checking it now.
    6. Your smiling.
    7. Your still reading my comment.
    8. You know all you have read is true.
    10. You didnt notice that i skipped 9.
    11. Your checking it now.
    12. You didnt notice there are only 10 facts
    Copy and paste to 1 video, tomorrow will be your best day ever! no matter what HAPPENED IN ROME LAST NIGHT. WE ARE GOOD LOOSER NOT YOU TROPHILESS

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 28, 2009

    Watanzania hatuendelei sio kwamba tumelogwa bali tumezidi upumbavu. Tuendeleze timu zetu.

    Kila nchi wana mambo yao, sijaona matawi ya Manchester USA au Canada ambako wana utamaduni unaoendeana na Uingereza. Wao (USA/Canada) wanapenda football, baseball, hockey, basketball. Tupende Simba na Yanga.

    Huu ni Utumwa wa kimawazo

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 28, 2009

    Kama watoto vile.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 28, 2009

    inatia moyo!!!sasa tunaomba musherehekee kufunguliwa kwa tawi then tell what happened about the match!!!chabikia yanga na simba wewe unaweza ukafaidika wakiwa juu sio MU...............

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 28, 2009

    UFUNGUZI UMEINGIA NYONGOOOO! TEH TEH TEH TEH. MNGEFUNGUA SIKU NYINGINE SASA MTAFURAHIA UFUNGUZI KWA HALI YA 2-0?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 28, 2009

    Watanzania tunaitaji maombi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 28, 2009

    ......siyo tunahitaji maombi tu,tunahitaji maombi ya haraka sana,mungu tusaidie na nchi hii ya wadanganyika!!!

    ReplyDelete
  22. HAWA BARCA WAMEWEZA KWELI KUZIBA MIDOMO YA WATU MAANA TUSINGEKUNYWA MAJI.
    liverpool daima

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 28, 2009

    ukereketwa mwingine ovyo kweli!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 28, 2009

    Anon wa 2:59 a.m umeniacha hoi mpaka nikasahau matokeo kwa sekunde. tehe tehe...

    Hatya

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 28, 2009

    tatizo mani wana confo kishenzi

    ReplyDelete
  26. let me give them good advice how they can support team.buy share,attend on the match or u can buy scarf ,t-shirt.......hama kweli kipara si akili nimeamini leo

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 28, 2009

    mambo ya pwani bwana yananichanganyachanganya vitu flani wanavyofanya@
    zee zima lavishwa shanga, guu la kushoto la Fergie lavishwa shanga... wanaita kikuku.. hii ni hatari... sasa nyie washabiki wa manU mnaanzisha hilo genge huku m'mevaa shanga sa mnamaanisha nini?
    tehe tehe tehe! hii kali Fergie alianganya Big-G na Karanga halafu akawa anatafuna kwa pamoja... anamtoa midfielder anamwingiza forward.... haha ha ha ha ha!!!!!
    nikawa najiuliza hivi christina ronardo yumo uwanjani kweli haa kumbe alikuwa mbagala kusaidia kuokota mabomu yaliosalia...
    eti ni kweli kuna wakati uwanja mzima ulitulia tuliiii ni baada ya Fergie KUJAMBA alafu akawa anavunga kama anawaelekeza wachezaji kumbe kachafua hewa? ni kweli jamani? alafu wengine wanasema alikuwa anaviachia kulingana na kelele za mashabiki ili wasimshtukie, ni kweli jama?


    Nondo

    ReplyDelete
  28. SipendiukolonimamboleoMay 28, 2009

    Upuuzi mtupu, tawi tawi!! tawi bongo? Nani anawajua nyinyi huku manchesta? acheni kuendekeza utumwa!
    Wabongo tuna vichwa vimejaa kamasi wakati mwingine, haya sherekeeni tawi lenu!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 28, 2009

    NAMUONA MTOTO RESTITUTA BURA KWA MBALI NA KAPTURA YAKE.. MAMAA UKO JUUU..
    MDAU REGENCY

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 28, 2009

    ok jamani hili mimi limenishinda, kwa hiyo nitauliza. luanzishwa kwa hili ninhii litawasaidiaje hawa ndugu zetu katika maisha yao ya kila siku? kuna faida gani watakayoipata ambayo hawakuwa wakiipata walipokuwa hawajaanzisha hili ninhii? kulikuwa na haja gani kumualika balozi wa uk? mwisho kabisa je hili ninhii litakuwa likitambulika rasmi na man utd club kama moja ya branch za supporter zao abroad?

    watanzania tafuteni la maana na la kuwasaidia katika maisha yenu.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 28, 2009

    Mdau 2:56 ukiwa unadesa, jaribu ku-edit kidogo:
    SIYO Your reading my comment... NI YOU ARE READING......

    2. SIYO Now your saying/....NI NOW YOU ARE.....
    Inaendelea huko 5,6,7...

    HALAFU JANA MAN U HAKUWA GOOD LOSER, ACTUALLY AMEKUWA THE WORST LOSER (he didn't fight). AC MILAN ALIKUWA GOOD LOSER KWA LIVERPOOL..(if you know what I mean)

    chiggs, Deslam

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 28, 2009

    Anony 2:59Am
    Tumia lugha ya mama yaani kiswahili, tofautisha you are/your

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 28, 2009

    Mkuu wa wilaya ya nanihii
    Jina la pili la M'kiti wa Man U ni Mbwambo.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 28, 2009

    Hawa wote hawajawahi kuishi na wazungu wakajua tabia zao. Wakisikia upuuzi huu watatucheka kuwa tunajipendekeza kwao na hatuna vitu vyetu.Hawatujali hata leo ukiwauliza hao MAn U kuna baadhi hata hawajui kama kuna nchi inaitwa Tanzania leo sembuse tawi, mmeishiwa mawazo bongo zimejaa kinyesi, upuuzi mtupu !!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 28, 2009

    hapa naona sura za kina kin..na gosha... zilikuwa bado hazijasagika na kupaganyika,duh kwa kweli hii kali duh na tawi likafunguliwa kabla ya shughuli yenyewe!!!Poleni jamani,haswa Sebbo!!!!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 28, 2009

    yep wakati wazungu tele hapa hata ahawajui ilipo tanzania? watanzania na mbumbu zao wanafungwa matawi ya klabu za ulaya. wengine huko kenya wanajiua kwa sababu arsenal wamefungwa na united na jana tu mnageria ameua wenzake wanne kwa sababu united kufungwa. upuuzi mtupu, kupenda timu sio kosa lakini ukizidi namna hii ni ujinga na utumwa wa kisaikolojia. hebu jiulizeni nini mtakachonufaika na kufungua hilo tawi zaidi ya kuibiana pesa?

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 28, 2009

    Siyo mbaya sana, manaake hata CCM wamekuwa wakianzisha matawi London na miji mingine ya England.....nadhani nimeeleweka vizuri.

    ReplyDelete
  38. nadhani hatujalogwa tu,balio tumelaaniwa kwa kufanya mambo yasiokua na maana kama mdau alivyosema hapo juu

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 28, 2009

    Nadhani watanzania tunahitaji kuchapana viboko ili vichwa viamke,huu ni ukosefu wa kazi au tuitaje?Tumekaa kushadadia timu za watu wakati timu zetu kibao zimejaa hapo ambazo zinahitaji msaada.Hebu waulizeni hao waingereza kama wanajua timu yeyote ya bongo.Tuacheni upuuzi na tufanye kazi kwa bidii na kuthamini utu wetu na vitu vyetu wenyewe....mnaniudhi sana!!

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 29, 2009

    Wengi mnaoponda hapo juu mko nje ya nchi na mna stress zenu za kuishi kama second citizen....Huko Ulaya watu wameishi na wakaamua kurudi nyumbani, msiulize kwamba eti hatujawahi kuishi na wazungu!

    Ubora wa soka ndicho kivutio kikubwa kinachofanya dunia nzima ipende soka la Ulaya!

    Tawi limesajiliwa kisheria na litakuwa na shughuli nyingi za kuendeleza soka hasa la vijana. Hao Simba na Yanga tulishawachoka. Hawabebeki....kuna wazee walibeba matofali miaka ya 70 mpkaka leo wanazuia maendeleo ya klabu hizo.

    Wote walio katika klabu hii ya mashabiki wa Man United wa kazi zao au biashara za kuwaingizia kipato...Kwa hiyo msisema eti tumekosa kazi ya kufanya!

    MKIONA MAISHA YAMEWASHINDA HUKO NJE RUDINI NYUMBANI.....AMA LA BASI ACHENI KUMALIZIA HASIRA ZENU ZA KUBEBA MABOKISI KWA KUPONDA KILA KITU KINACHOFANYIKA BONGO.....!!!!

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 29, 2009

    Acheni ushamba nyie wabeba maboksi, tumewazoea kwa kuponda kila kitu kinachofanywa bongo.Hivi kuna kosa gani mtu kuwa mpenzi wa man u? au kufungua tawi lao? mbona nanihii kila siku tunamuona yupo bongo na fulana za bwawa la maini hamumsemi? tumeona simba na yanga marekani zimeanzishwa na wanacheza mechi tena zenye ushindani kwa hiyo na wao wanajipendekeza?kama alivyogusia mdau wa 8:49PM kila kukicha matawi ya CCM ulaya na marekani! maana yake nini ni ushamba au kujipendekeza au mapenzi kwa chama?acheni wivu wa kijinga, kama mmekosa vikombe jiandaeni kwa msim ujao sio kuwaponde wenzenu.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 29, 2009

    Embu ngoja kwanza..!Ufunguzi wa tawi la ManU??

    Mimi ni mshabiki wa ManU,lakini nilipokuwa Tz nilikuwa ninashabikia SIMBA zaidi kuliko ManU,infact hata sasa ingawa sio kama zamani.

    Watanzania,tufungue matawi ya SIMBA,YANGA na timu nyingine.Tunahitaji vijana wetu kucheza mpira duniani.
    Kazi kwenu...!!!

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 29, 2009

    Ok Watanzania wa Tanzania,na wabeba Mabox wote nafikiri mna jambo lamaana la kuongea zaidi ya kutupiana madongo.

    Embu tuongee mechi ya jana,Ukweli ni huu.Mechi ya jana haitupi mtazamo uliyo clear.Messi na Ronaldo nani mchezaji bora?Nafikiri ni bora kusema Xavi and eniesta labda.Mechi moja kushindwa ndio sio temu nzuri?nafikiri Man united overall more decorated.

    Manunited,ina big squad and is going to come back next CL.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 30, 2009

    hahahahahahaa kwi kwi kwi

    tih tih tih

    aisee mbavu zangu

    aya mabwana i hope hamkuvunja vyupa apo,,dah!!

    mbelekozzzzz iligoma bwana

    mwanaume atajulikana tu,na siye anajulikana tu

    mzazi utamjua tu

    hahahahahaaaa

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 30, 2009

    mdau Nondo apo juu

    kwi kwi kwi
    ahahahaha ha ha ha ha ha ha

    nihurumie izi mbavu basiii!!!

    dah u made my day

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 30, 2009

    mjichangishe izo pesa zinazowawasha
    then pelekeni MAKETE mkasaidie unpreveledge families kule

    mnachamba au???

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 30, 2009

    afu utakuta hili ni wazo la SABBO

    hahahahahahaaaaa
    waganda bwana?kama wakenya tu

    maji ya uganda kisiwa cha kenya

    hahahahaaaa

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 31, 2009

    anon wa 9:15 umenifanyia kazi rahisi sana. mimi nafanya kazi na jamaa baadhi wametoka college uk, usa na canada. hata kazi zenyewe hawawezi kufanya wana ma-frastration kutoka huko basi kila kitu wanaona hakifai wakati wao wanachohitaji ni kusahau kule walikotoka na kuanza kuconcetrate na life yaani reality. mmoja alijifnya ooh mimi siwezi kufanya kazi kwa mshahara huu akawa hatokei kzn siku 2 au 3 bila taarifa. wakampa barua yake BYE! amelia kama mtoto mgogo tukashangaa; huyu ndio analilia hii kazi? ukishabikia man u wanakuuliza inakusaidia nini. kuishi abroad himaanishi kuwa na busara sana. sisi tutashabikia man u na tutanunua viwanja tutajenga na wao waendelee kubeba maboksi na kututukana hivyo hivyo hatujali. kwanza waanzie kwa huyu mwenye blogu ambaye ni shabiki mkubwa wa bwawa la maini tena nakumbuka kuna nembo ilichorwa vizuri ilikuwa imechanganaya bendera ya tanzaia na takataka za liverpool. mbona walimsifia yule jamaa kwamba wanafurahia kuona hata mtanzania anaweza kucheza na photoshop kiasi hiki. yaani hawa jamaa wabeba maboksi ndio wanaohitaji msaada wa kisaikolojia kuliko wengine kwasababu mimi nimewaona mifano halisi ninayo mmoja amefukuzwa kazi na mwingine yupo under scrutiny ya nguvu. huko asia kuna washabiki wa man u kuliko bara lolote lile lkn je asia iko nyuma kimaendeleo? kama unafikiri kushabikia timu za ulaya ni utumwa kawaulize etoo, drogba, adebayor, essien na wengineo wengi tu halafu tuone maoni yao juu yako. kama huyo jamaa wa 9:15 ndiye sebbo basi anajua anachokisema huko uganda rio ferdinand ana kituo cah kuendeleza soka la vijana kwa gharama yake na ameshakwenda pale mara 2.
    haya. messi na ronaldo. bado ronaldo ana edge kwa messi kwasababu workrate yake iko juu kuliko messi isipokuwa messi atachukua uchezaji bora bila ubishi dunia inataka hivyo na ana idadi nzuri ya magoli ktk ecl na ubingwa. ronardo siwezi kumsahau kwa lile goli la porto though.

    glory glory man u we'll come back stronger you can be sure of that.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...