bosi wa masokon wa TBL David Minja akikabidhi magari kwa mwenyekiti wa Yanga Imani Madega
mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali akikabidhiwa magari na David Minja
basi la Yanga
basi la Simba
Kampuni ya bia (TBL) imekabidhi magari aina ya Toyota Coaster na Toyota Hiace (pichani) kwa klabu za Yanga na Simba ambapo mabasi madogo ni kwa ajili ya viongozi kutumia kwa shughuli ndogo ndogo za klabu, na makubwa kwa ajili ya kuwabeba wachezaji kwa safari za ndani na nje ya jiji la Dar katika michezo yao na mashindano na mazoezi katika hafla ya aina yake iliyofanyika katika viwanja vya leaders club, dar.
Ahsante Sana TBL kwa hili ila nauliza kitu kimoja,
ReplyDeleteHawa watani zetu Ssc watapaki wapi mabasi yao?!
kama vp tuwatoe mapene walete Jangwani pale yalaleee. ha haaaa
Hii ndiyo inachangia kuua soka Bongo. Sidhani kama Simba na Yanga wanahitaji misaada kuliko timu zingine za ligi kuu. Ingawa ni nzuri kwa TBL kibiashara lakini inapunguza ushindani.
ReplyDeleteKwani Manji hawezi kuwanunulia basi au Simba hawana wafadhili wa kuweza kuwanunulia basi?
Kaaazi kweli kweli!!!!!
JAMANI???!!!
ReplyDeleteKAZI IPO HIZI HARAMU,NDO MANA WAZENJI NAWAPENDA KWA MISIMAMO YAO YA VITU KM IVI.misaada mingine bwana
aya
mimi naona TBL wako juu sana kuliko serengeti kwani wanadhamini secta kibao sasa simba kazi kwenu kuwaonyesha TBL kuwa hawajakosea kuwadhamini kama kawa fanyeni mambo CAF(SHILIKISHO)KWANI NI KAWAIDA YENU KTK INTERNATIONAL NYINYI NI VITUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUZZZ
ReplyDeleteYANGA NA SIMBA BADO WANATUMIA VIPANYA NA VI DCM?
ReplyDeleteNILIFIKIRI WAMESHA MOVE ON...
Kwanini Simba na Yanga tu? nadhani ingekuwa vizuri kwa TBL kudhamini usafiri wa ndani kwa vilabu vyote vya Ligi kuu, hapa nina maana ya kulipia usafiri, kwani kuwapa haya mabasi ni rahisi, ila kuyatunza na kuyahudumia ipasavyo itakuwa mzigo mkubwa sana kwa hivi vilabu. kumbuka hata FAT iliwahi kuwa na basi, likaishia kuwa mradi wa kubeba abiria mikoani.
ReplyDeleteTBL wanatangaza biashara. Hizo timu nyingine zinapofanya mazoezi huwa zinajigawa Simba na Yanga. Ndio maana mwenye nacho anaongezewa.
ReplyDeleteHaya ndo tuliyoambiwa kwamba ni mabasi ya kifahari? Azam bado wamewapiga bao, na hayo magari yape mwaka tu juu ya mawe au yanauzwa!!!
ReplyDeleteWizzzzz Mtupppppu!!!
wadhamini wanapoteza mda kwa yanga na simba na wanazidi kukandamiza soka la tanzania.timu zinazo hitaji misaada hazipewi timu ambazo zinajigamba zina hela ndio zinasaidiwa zaidi.
ReplyDeleteRock on Dave......
ReplyDeleteTBL wamechemka kuweka "Kilimanjaro Premium Lager" on both teams.
ReplyDeleteMaadam hawa ni mahasimu wa jadi mngempa kila mtu brand yake - mmoja Kilimanjaro mwingine labda Miller Draft Beer.
Basi alilotoa marehemu gulamali lilikuw zuri kuliko haya mabasi. www.tanzaniasports.com laba tu ufahamu TBL wanafana biashara hawatoi huduma a bure.
ReplyDeleteHii biashara mnataka wakajitangazie mji mpwapwa! Nyie vipi!! Umeshawahi kuona samsung au IAG wanafadhiri WESTBROM au MIDOSBROUGH!Usifikiri wanatoa msadaa hapo wanatangaza biashara kupitia timu zenye majina makubwa!
ReplyDeletekatoe msaada kwenye mashule na hospitalini. sio unapoteza muda kuwapa magari yanga na simba ambao mpaka sasa hatujawahi kuwaona wakicheza mpira unaoeleweka duniani.watoto wako wanahitaji msaada wa komputer pale shuleni na umeme hakuna
ReplyDeleteNAKUBALIANA NA MMOJA HAPO JUU KILA SIKU YANGA NA SIMBA TU TIMU ZINGINE HAZIPATI MISAADA KAMA HII, HAYA NI MANI YANGU TU JUU YA CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILTY, LAKINI KWA UPANDE WA MARKETING HAWALAZIMISHWA KUMSAIDI MTU AMBAYE HATOWEZA KUWA-MARKET, NDO MAANA MAKAMPUNI MENGI DUNIANI UTAONA WANAWATAKA AKINA DAVID BECKHAM KUWATANGAZIA BIASHARA ZAO KWA VILE NI TAYARI WAO NI MARKETING TOOLS, KILA MTU HAPA DUNIANI ANGEPENDA KUNUNUA KITU KILICHOKUWA ASSOCIATED NA BECKHAM, PIA WATU WENGI HUWA WANASOMA NA KUANGALIA HABARI ZA BECKHAM SO ANAPOVAA CAP YA PEPSI COLA NI WENGI WATAIONA NA KUJIHUSISHA NA KINYWAJI HICHO KWA NAMNA MOJA AU INGINE IKIWA NI PAMOJA NA KUKINUNUA, SO THE SAME KWA KAMPUNI ILIYOTOA HAYO MABASI INAJUWA FIKA SI TANZANIA TU BALI AFRIKA NA DUNIANI KOTE TIMU ZA SIMBA NA YNGA NDIZO ZIJULIKANAZO SO THEY ARE MARKETING TOOLS, WAKIWAPATIA MISAADA YENYE HABARI ZA BIDHAA ZAO NDO MARKETING YENYEWE HIYO. PENGINE TU KUWA NA MAKUSUDI MAZIMA YA KUSAIDIA TIMU ZINGINE, LAKINI KWA HAPO HII KAMPUNI INALENGA ZAIDI KUJITANGAZA YENYEWE SI MSAADA KWA TIMU HIZI MBILI.
ReplyDeleteKweli mwenye nacho anaongezewa,,,sasa hapa tunajenga soka au tunabomoa soka? kuna timu zinaitaji huo msaada hata ukiwaambia wakupigie magoti wapo tayari,,,pesa za usafiri zenyewe ni taabu tupu leo hii unakwenda kujaza maji baharini na kujisifu,,hivi kweli simba na yanga hawana uwezo wa kununua hizo gari? TBL inaelekea hakuna mshauri mzuri pale hata kama bihashara sio kiivyo hapo ni kudidimiza soka la Tanzania
ReplyDeleteNaomba kuwakilisha maoni yangu
Michu, let me join hands with others in letting out what's in my head. I mught have numskulls buty maybe brainy is doing overtime.
ReplyDeleteSIMBA NA YANGA, why hizo timu tu? kweli hapo TBL nao watajigamba kuwa nia yao ni kukuza soka Tanzania? Kwa hizo pesa kwanini wasingetangaza kuwa wanatafuta 5 bora ya msimu ili wawadhamini in the next season? hapo ungeshangaa ile race ya 2nd position inavyokuwa hot.
Secondly, hivi hizo coaster na hiace zinaweza kwenda safari ya mbali kama MZA? AU KAGERA? TBL walivyojigamba kuwa wanatoa mabasi nikategemea kuwa watatoa basi kwa maana ya basi, lakini sio town commuter. I expected kuona basi kama la AZAM, jilo ndio unaita basi, not just daladala unaita basi na unalitoa kwa mbweeembwe. I feel sorry for the Brand manager mr shelukindo who proudly announce that tuinatoa MABASI. Oh hell
Tatizo la kushabikia man.u na liverpool ndio maana wengi wanashangaa kwa simba na yanga kupewa mabasi na TBL. ligi yote wadhamini wakuu ni vodacom, tbl wanawadhamini simba na yanga kwa mkataba maalum. hivyo kama mna taka kila timu iwe na basi lake hiyo ni kazi ya vodacom ambao ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu ya tanzania.
ReplyDeleteTuelewe kwanza kabla ya kulalamikia kila jambo.