
Jamaa mmoja wa Marekani anayejiita Yesu Kristo amewaua watu wawili na kujeruhi watu saba wakati alipovurumusha risasi kwenye chumba cha wanawake wanaosubiria kutoa mimba zao huku akisema 'Ingekuwaje kama bikira maria angeamua kuitoa mimba yangu.
Jamaa huyo anayejiita Yesu Kristu au Massiah akiwa amevalia kama Yesu, aliingia kwenye kliniki ya utoaji mimba ya Huntsville na kuanza kupiga risasi hovyo kwenye chumba cha mapumziko ambacho wanawake wajawazito hukaa humo wakati wakisubiria kutoa mimba zao.
Walinzi katika kliniki hiyo walifanikiwa kumwahi Yesu Massiah kabla hajaikoki tena bunduki yake Glock 9mm aliyoinunua kihalali kwenye duka moja nchini humo.
Walinzi katika kliniki hiyo walifanikiwa kumwahi Yesu Massiah kabla hajaikoki tena bunduki yake Glock 9mm aliyoinunua kihalali kwenye duka moja nchini humo.
"Kutoa mimba ni dhambi" alisema Yesu wakati alipokuwa akipelekwa kituo cha polisi baada ya kukamatwa akiwa amefungwa pingu na kuongeza "Ni kitu ambacho siwezi nikakifumbia macho".
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba jamaa huyo aliibuka ghafla na kuanza mashambulizi yake ambayo yalipoteza maisha ya Dr. Nelson Woodring, 51, na nesi Danielle Costa, 29.
"Alikuja kwenye meza ya maulizo na kuuliza kama anaweza kumuona Dr. Woodring," alisema mhudumu kwenye meza ya maulizo na kuongeza "Kilichofuatia baada ya hapo alikuwa akisoma mistari ya biblia huku akipiga risasi kwa kila kitu alichokiona".
"Hali ilikuwa inatisha sana" alisema nesi mmoja ambaye alipigwa risasi ya mkononi na tumboni na hivi sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.
"Alimfata Dr. Woodring na kuweka mikono yake kichwani mwake na kumwambia "Nimekusamehe madhambi yako" halafu akampiga risasi kwenye paji la uso".
Maafisa polisi wa Huntsville hawajapata jibu Yesu huyo aliingiaje na silaha kwenye kliniki hiyo pamoja na kwamba kuna ulinzi mkali getini na kukiwa na kamera za ulinzi kila kona.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye selo yake Yesu alisema kwamba hajutii hata kidogo kwa mauaji aliyofanya.
"Kama nilivyosema kwenye John 16:21, maisha ya kila kitu ni ya thamani sana, sio tu kwa wale ambao wameishazaliwa, baba yangu, Mungu anafikiria kama ninavyofikiria".
Yesu aliendelea kusema: " Ingekuwaje kama bikira Maria angeamua kuitoa mimba yangu, ningezaliwa?, inawezekana alifikiria kama hivyo lakini aliamua kutoitoa mimba yake na kunizaa, alifanya jambo sahihi kabisa, kukaa na mimba yake hadi mwisho na kuipatia dunia mkombozi, ni mwanamke aliyebarikiwa sana"
Kwa mujibu wa wataalamu wa sheria, Yesu anaweza akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.
"Kwa jaji sahihi na waendesha mashtaka wazuri Yesu atauliwa tena kwa mara nyingine" alisema profesa wa sheria wa chuo kikuu cha Michigan Profesa Arthur Lipscomb.
Yesu kwa upande wake amesema kuwa haogopi adhabu ya kifo na kusema "Niko tayari kufa kwaajili ya dhambi za wengine".
duh kazi kweli kweli haya mambo ya imani za kidini mara nyingu huwa yanakuwa ni magumu tu, sasa wale watu masikini walikuwa wanasubiri kutoa hizo mimba yaani kuua viumbe halafu akaja huyo jamaa na kuona isiwe tabu badala ya wao kutoa mimba na kuua ngoja awaonyeshe au kuwaua ili ngoma iwe draw imekuwa balaa.Ya Mwenyezi Mungu tumpe Mungu na ya kaisari tumpe kaisari!
ReplyDeletemie nampongeza sana huyo Yesu kwa uamuzi wake wa maana...piga wote risasi yesu,na pia wamwachie huru
ReplyDeleteYesu Kristo? amerudi lini na kuanza kuhukumu watu kwa risasi? ama kweli kuishi kwingi kuona mengi!
ReplyDeletehaya shime jamani tufanyeni zambi yesu kashajitolea huyo!
ReplyDeletekudadadeki!
duh. kumbe yesu tupo nae? eeeh wewe yesu mbona unamuacha shetani akitawala dunia hii?? kwa nini badala ya kufanya mema na kuhubiri mema kwa njia ya amani wewe yesu umeamua kuhubiri kwa njia ya risasi?? hivyo ndivyo ulivyotumwa na baba yako aliye mbinguni???
ReplyDeleteduh!
Yesu wangu mbona umetuacha watanzania tukiteseka? eeh yesu wamngu tunafahamu ulisema kuwa utarudi, mbona sasa hujatuambia kuwa umesharudi na kwamba upo marekani kwa sasa??
ReplyDeleteeeh yesu baada ya kuwatungua hao wauwaji wa vichanga, tunaomba basi eeh bwana uje Tanzania utusaidie kuwatungua kwa risasi vichwani wale mafisadi wafanyao wanao wateseke. Eeeh Bwana yesu sihitaji kuwataja hao mafisadi hapa michuzi blog kwa maana kaka Issa Michuzi ana tatizo woga, na kubania maoni makali makali kwa hiyo eeh bwana yesu nikiwataja hapa basi kaka michuzi hatairusha hii comment hewani kama ilivyo kawaida yake mbaya. Lakini eeh bwana yesu kwa kuwa wewe waona sirini, waona hata yaliyo mioyoni mwetu unawafahamu mafisadi hawa wote kwa majina yao, wengi wa waharifu hawa ni viongozi wa nchi eeh yesu ambao hata huko marekani huja eeh bwana.
eeh bwana yesu tunaomba baada ya operesheni hiyo ya marekani uje basi bwana na huku tanzania utusaidie, ukatuondolee kikombe hichi cha matatizo kwa kuwatungua vichwani wale mafisadi woote eeh baba. bila kumsahau yule muajemi aliyetokea mashariki ya kati na kuja kutuletea maumivu makali ndani ya nchi yetu eeh baba.
mwisho kabisa eeh bwana yesu ninaomba baba aliye mbinguni akusaidie akawajaze busara wale majaji wote wa mahakama wakaweze kutenda haki katika maamuzi yao, wakuachie huru ili basi eeh bwana ukaweze basi kuja na huku tanzania kufanya hizo operation zako za kuua wauaji uje bwana utuondolee mafisadi wauaji wote.
Amina.
Elieza.
Ndio mesiah. ndio bwana mkombozi wa dunia. baada ya kuhubiri kwa njia ya amani, na kwa kutumia maandiko, dunia imeonekana kushindikana na kutofuata kabisa yale uliyoyanena. madhambi yamezidi, mauwaji ya kutisha yamezidi, chuki dhuluma na kila aina ya uovu vimezidi sana. baada ya binadamu kushindwa kufuata mafundisho yako bwana yesu hiyo njia uliyotoka nayo sasa hivi ya kuwapiga risasi waovu ndio njia sahihi bwana yesu. binadamu wamekuwa jeuri hawasikii na hiyo njia uliyotoka nayo ndio njia pekee ya kuadavisha wanawako bwana yesu. mahakama ikuache ili basi uwapige risasi waovu woote na wabaki wale wema tu ambao utaenda nao juu mbinguni kwa baba yako eeh yesu.
ReplyDeleteBwimbwi,NC.
Unajua tunapokuja kwenye suala la ugaidi tusiangalie wale wenye dini ya kiislamu tu hata wakristo wapo magaidi tena ni wabaya kuliko hata Taliban.
ReplyDeleteUkifuatilia hapa US, hivi sasa hawa conservatives ni sawa kabisa na Taliban maana wao mtu ukiwa haumini kama wanavyotaka basi wewe ni adui yao na wako tayari kukufanyia kama huyu Yesu alivyowafanyia wenzake. Huu ni ugaidi period na si kingine.
Huwezi lazimisha watu wafuate imani yako kwa nguvu hapo ndipo tunaporudi kwa taliban na conservatives wa marekani hawa wote wanaingia kwenye kapu moja la "extremists".
Utoaji wa mimba ni zaidi ya imani ya dini. Ni uuaji na hakuna mjadala hapo. Namshangaa sana Obama ambaye anajiita mkrito wakati anaruhusu uuaji wa watu wasio na hatia.
ReplyDeleteSasa ndio muda muafaka wa dini kuenezwa kwa upanga.Dini kwa upanga ngoma droo
ReplyDeletePlease dont call this Man YESU.
ReplyDeletedaaaa duniani kuna vituko vya kila sampuli
ReplyDeleteduuu haya huyu nae kaamua kugiita yesu lakini YESU wa halali hakuwateka watu kwa upanga,vita n.k aliwaita kwa upole hivyo na huyu yesu feki asinge toa roho za watu
ILA ALICHOFANYA SAWASAWA MANA ANATETEA ROHO ZA WATU
KAMA HAWATAKI KUZAA KWANINI WASITUMIE KONDOMU?
SAFI BWANA YESU FUNDSHO KWA WAJINGA WENGINE HASWA BONGO kama utaki kuzaa kwa nini unachanua alafu unakwenda kuua hatari kweli kweli
ReplyDeleteJamani hii habari sio ya ukweli. Ni habari ya kutungwa tu inatoka kwenye jarida maarufu la story za kutunga linaloitwa The Onion.
ReplyDeletehttp://www.theonion.com/content/index?utm_source=nav
Mnyepe
we anoni wa 12:04 kondomu za nini tena? Kondomu hazina flavour. mungu alipotuumba hakutuvalisha kondomu ndio maana ukivaa kondomu libeneke hulipati live mwanawane. lile joto stahiki hulipati kabisa so fogeti abauti uzing'i kondomu.
ReplyDeleteushauri unaotakiwa kuutoa ni jinsi ya kucheza kwa stepu. waambie hasa wasichana waijue vizuri ile penati box yao ili basi wakishaingia ndani ya penati box yao wajichunge na uchezaji rafu usio na ulazima sababu utawasababishia penati na kujikuta wakipigwa bao la kizembe chini na uvimbe ukitokea juu na adhabu zake sasa ndo kama hivyo jesus anawashukia!!! jamani kina dada msifanyage makosa ndani ya kumi na nane la sivyo muwege tayari hata kulea watoto jamani. mkumbuke kuwa mama zetu hawakututoa ndo mana leo hii tunawaheshimu na kusema nani ka mama!!!
Ahsenti
Kamuzola
Na wewe MNYEPE uwe unaandika kitu ulichokuwa na uhakika nacho. Hii habari imetangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwani wewe huoni? OOOooooopppsssssssssss samahani kumbe gongola mboto hampati habari za kwa OBAMA pole weeee kalagabaho.
ReplyDeleteKama hiyo story ni yakutungwa sawa huyo ametuweza kweli kweli. Ila kama ni ya kweli ni hatari. Ila tuwe makini kwa lolote wakati wowote na ningependa kusema hivi:-
ReplyDeleteWakati mwingine binadamu tusipuzee hii hali ya kawaida eti ukamuona binadamu wenzako ukadhani kuwa hata Yesu / Nabii Issa atakuja wa maajabu labda kila mtu ambaye utamshangaa labda atakuwa tofauti. NOOO. Tujue kuwa Nabii atakuja kama mtu wa kawaida kama mimi na wewe. Na pia malaika wkt wote kama ilivyo katika Masahafu na Biblia huwa haendi kwa mtu kama malaika wkt mwingine anaenda kama binadamu.
Mfano wa kisa kimoja cha Tajiri na maskini ktka hadithi za mitume kwa ufupi naeleza kinasema hivi:
Maskini alikwenda nyumbani kwa tajiri akiwa mchafu saana alipofika akamkuta tajiri na kuanza kuomba msaada wa chakula. Tajiri yule bila kujua alimfukuza masikini yule km mbwa kwa kuwa alikuwa ni mchafu na anachafua nyumba yake iweje walinzi wamruhusu kuingia. Aliwaamuru wafanyakazi wake wamtoe nje yule masikini. Baada ya yule tajiri kufanya vile muda ulipopita Mw.Mungu akamfanya akawa yeye ndio maskini, akamuondolea rizki na yule Maskini akawa tajiri yeye ndio akaenda kwa yule aliyekuwa maskini kuomba msaada. Maskini yule akamwadithia kisa kile.
Huu ni mfano wa malaika kugeuka kuwa watu. Hivyo tusione pia baadhi ya watu wanaokemea maovu tukawapinga. Ni watu lakini roho huwezi jua km ni Mungu amemwagiza. Tujiulize; Je Mw. Mungu alipoangamiza vizazi vilivyopita kwa dhambi je yeye alikosea kuuwa watu? Tujiepushe na dhambi hatujui wkt gani Kiama na wakati gani Nabii Issa / Yesu atarudi.
Tunaambiwa Massiydajal atakuja atajifanya yeye ndio Mungu na wale wenye dhambi watamuamini wasio na dhambi watampinga na kuuliwa. Sasa wewe kwanini uunge mkono dhambi hizi? Jifikirie, fikiria maandiko ya Biblia/Masahafu. Fikiria hadithi / visa vya manabii upate taswira ya leo nini kinatokea.
Mtazamo wangu wasije kumtesa sana mtu huyu. Wamtumie mtu huyu kumchunguza. Waende taratibu Wafikirie pande mbili.
Tatizo binadamu tumezidi dhambi hivyo hakuna atakaye support hilo hata mmoja. Hivi nyinyi mnataarifa kuwa Yesu yupo karibu kurudi? Je wewe binadamu unahakika Yesu akirudi atakujulisha kwa kukupigia simu? Je unahakika kuwa utamjua? Tuweni makini jamani. Tusiende pupa
ReplyDeleteDuh! Ahsante kaka Michuzi kwa kutuletea hiyo habari. Iwe ni kweli iwe ni uongo story hiyo. Ila ni kuwa pia tumekumbushwa kuwa binadamu wamezidi dhambi. Tuacheni jamani hatujui mwisho lini. Hatujui Mweshimiwa atakuja lini. Yani hii ni hatari kweli kweli Hospitali kbsa maalumu kwa utoaji mimba????? inatisha. Tunakoenda kubaya.
ReplyDeleteHaya kwa wale wanaounga mikono mambo ya kidhungu ungeni mikono.
watu mna MAPEPO SANA umu blogun
ReplyDeletena uyo feki yesu
ila utoaji mimba ni UUAJI,na obama wenu ndo yuko ktk mstari mmoja wa kutoa ruksa,akaishi arabuni
Maoni yangu kama Mkristo:
ReplyDeleteHuyo mtu aulizwe jina lake halisi, maana marekani si ndio wanaojifanya kuwa ni mabingwa wa ku-keep records?
Hasiukumiwe kama YESU KRISTO, la sivyo marekani mtamjua mungu ni nani, mtalipa dhambi hii. ya kumdharirisha mwana wa Adam
Fanyeni utani na vitu vyote sio hii ya kumuita muuaji ni Yesu Kristo?
Simo kwenye dhambi hii mimi na kizazi changu na mungu wangu ni shahidi
hivi yesu (issa) anajua kutumia bastola au bunduki? kali kweli
ReplyDelete