Yesu akiwa chini ya ulinzi huku picha ndogo ikionyesha mmoja wa majeruhi akipandishwa kwenye ambulansi.


Jamaa mmoja wa Marekani anayejiita Yesu Kristo amewaua watu wawili na kujeruhi watu saba wakati alipovurumusha risasi kwenye chumba cha wanawake wanaosubiria kutoa mimba zao huku akisema 'Ingekuwaje kama bikira maria angeamua kuitoa mimba yangu.
Jamaa huyo anayejiita Yesu Kristu au Massiah akiwa amevalia kama Yesu, aliingia kwenye kliniki ya utoaji mimba ya Huntsville na kuanza kupiga risasi hovyo kwenye chumba cha mapumziko ambacho wanawake wajawazito hukaa humo wakati wakisubiria kutoa mimba zao.
Walinzi katika kliniki hiyo walifanikiwa kumwahi Yesu Massiah kabla hajaikoki tena bunduki yake Glock 9mm aliyoinunua kihalali kwenye duka moja nchini humo.

"Kutoa mimba ni dhambi" alisema Yesu wakati alipokuwa akipelekwa kituo cha polisi baada ya kukamatwa akiwa amefungwa pingu na kuongeza "Ni kitu ambacho siwezi nikakifumbia macho".
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba jamaa huyo aliibuka ghafla na kuanza mashambulizi yake ambayo yalipoteza maisha ya Dr. Nelson Woodring, 51, na nesi Danielle Costa, 29.

"Alikuja kwenye meza ya maulizo na kuuliza kama anaweza kumuona Dr. Woodring," alisema mhudumu kwenye meza ya maulizo na kuongeza "Kilichofuatia baada ya hapo alikuwa akisoma mistari ya biblia huku akipiga risasi kwa kila kitu alichokiona".

"Hali ilikuwa inatisha sana" alisema nesi mmoja ambaye alipigwa risasi ya mkononi na tumboni na hivi sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.

"Alimfata Dr. Woodring na kuweka mikono yake kichwani mwake na kumwambia "Nimekusamehe madhambi yako" halafu akampiga risasi kwenye paji la uso".

Maafisa polisi wa Huntsville hawajapata jibu Yesu huyo aliingiaje na silaha kwenye kliniki hiyo pamoja na kwamba kuna ulinzi mkali getini na kukiwa na kamera za ulinzi kila kona.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye selo yake Yesu alisema kwamba hajutii hata kidogo kwa mauaji aliyofanya.

"Kama nilivyosema kwenye John 16:21, maisha ya kila kitu ni ya thamani sana, sio tu kwa wale ambao wameishazaliwa, baba yangu, Mungu anafikiria kama ninavyofikiria".

Yesu aliendelea kusema: " Ingekuwaje kama bikira Maria angeamua kuitoa mimba yangu, ningezaliwa?, inawezekana alifikiria kama hivyo lakini aliamua kutoitoa mimba yake na kunizaa, alifanya jambo sahihi kabisa, kukaa na mimba yake hadi mwisho na kuipatia dunia mkombozi, ni mwanamke aliyebarikiwa sana"

Kwa mujibu wa wataalamu wa sheria, Yesu anaweza akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.

"Kwa jaji sahihi na waendesha mashtaka wazuri Yesu atauliwa tena kwa mara nyingine" alisema profesa wa sheria wa chuo kikuu cha Michigan Profesa Arthur Lipscomb.

Yesu kwa upande wake amesema kuwa haogopi adhabu ya kifo na kusema "Niko tayari kufa kwaajili ya dhambi za wengine".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2009

    duh kazi kweli kweli haya mambo ya imani za kidini mara nyingu huwa yanakuwa ni magumu tu, sasa wale watu masikini walikuwa wanasubiri kutoa hizo mimba yaani kuua viumbe halafu akaja huyo jamaa na kuona isiwe tabu badala ya wao kutoa mimba na kuua ngoja awaonyeshe au kuwaua ili ngoma iwe draw imekuwa balaa.Ya Mwenyezi Mungu tumpe Mungu na ya kaisari tumpe kaisari!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2009

    mie nampongeza sana huyo Yesu kwa uamuzi wake wa maana...piga wote risasi yesu,na pia wamwachie huru

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2009

    Yesu Kristo? amerudi lini na kuanza kuhukumu watu kwa risasi? ama kweli kuishi kwingi kuona mengi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2009

    haya shime jamani tufanyeni zambi yesu kashajitolea huyo!
    kudadadeki!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2009

    duh. kumbe yesu tupo nae? eeeh wewe yesu mbona unamuacha shetani akitawala dunia hii?? kwa nini badala ya kufanya mema na kuhubiri mema kwa njia ya amani wewe yesu umeamua kuhubiri kwa njia ya risasi?? hivyo ndivyo ulivyotumwa na baba yako aliye mbinguni???
    duh!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2009

    Yesu wangu mbona umetuacha watanzania tukiteseka? eeh yesu wamngu tunafahamu ulisema kuwa utarudi, mbona sasa hujatuambia kuwa umesharudi na kwamba upo marekani kwa sasa??
    eeh yesu baada ya kuwatungua hao wauwaji wa vichanga, tunaomba basi eeh bwana uje Tanzania utusaidie kuwatungua kwa risasi vichwani wale mafisadi wafanyao wanao wateseke. Eeeh Bwana yesu sihitaji kuwataja hao mafisadi hapa michuzi blog kwa maana kaka Issa Michuzi ana tatizo woga, na kubania maoni makali makali kwa hiyo eeh bwana yesu nikiwataja hapa basi kaka michuzi hatairusha hii comment hewani kama ilivyo kawaida yake mbaya. Lakini eeh bwana yesu kwa kuwa wewe waona sirini, waona hata yaliyo mioyoni mwetu unawafahamu mafisadi hawa wote kwa majina yao, wengi wa waharifu hawa ni viongozi wa nchi eeh yesu ambao hata huko marekani huja eeh bwana.
    eeh bwana yesu tunaomba baada ya operesheni hiyo ya marekani uje basi bwana na huku tanzania utusaidie, ukatuondolee kikombe hichi cha matatizo kwa kuwatungua vichwani wale mafisadi woote eeh baba. bila kumsahau yule muajemi aliyetokea mashariki ya kati na kuja kutuletea maumivu makali ndani ya nchi yetu eeh baba.
    mwisho kabisa eeh bwana yesu ninaomba baba aliye mbinguni akusaidie akawajaze busara wale majaji wote wa mahakama wakaweze kutenda haki katika maamuzi yao, wakuachie huru ili basi eeh bwana ukaweze basi kuja na huku tanzania kufanya hizo operation zako za kuua wauaji uje bwana utuondolee mafisadi wauaji wote.
    Amina.
    Elieza.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2009

    Ndio mesiah. ndio bwana mkombozi wa dunia. baada ya kuhubiri kwa njia ya amani, na kwa kutumia maandiko, dunia imeonekana kushindikana na kutofuata kabisa yale uliyoyanena. madhambi yamezidi, mauwaji ya kutisha yamezidi, chuki dhuluma na kila aina ya uovu vimezidi sana. baada ya binadamu kushindwa kufuata mafundisho yako bwana yesu hiyo njia uliyotoka nayo sasa hivi ya kuwapiga risasi waovu ndio njia sahihi bwana yesu. binadamu wamekuwa jeuri hawasikii na hiyo njia uliyotoka nayo ndio njia pekee ya kuadavisha wanawako bwana yesu. mahakama ikuache ili basi uwapige risasi waovu woote na wabaki wale wema tu ambao utaenda nao juu mbinguni kwa baba yako eeh yesu.
    Bwimbwi,NC.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2009

    Unajua tunapokuja kwenye suala la ugaidi tusiangalie wale wenye dini ya kiislamu tu hata wakristo wapo magaidi tena ni wabaya kuliko hata Taliban.

    Ukifuatilia hapa US, hivi sasa hawa conservatives ni sawa kabisa na Taliban maana wao mtu ukiwa haumini kama wanavyotaka basi wewe ni adui yao na wako tayari kukufanyia kama huyu Yesu alivyowafanyia wenzake. Huu ni ugaidi period na si kingine.

    Huwezi lazimisha watu wafuate imani yako kwa nguvu hapo ndipo tunaporudi kwa taliban na conservatives wa marekani hawa wote wanaingia kwenye kapu moja la "extremists".

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2009

    Utoaji wa mimba ni zaidi ya imani ya dini. Ni uuaji na hakuna mjadala hapo. Namshangaa sana Obama ambaye anajiita mkrito wakati anaruhusu uuaji wa watu wasio na hatia.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2009

    Sasa ndio muda muafaka wa dini kuenezwa kwa upanga.Dini kwa upanga ngoma droo

    ReplyDelete
  11. Please dont call this Man YESU.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2009

    daaaa duniani kuna vituko vya kila sampuli


    duuu haya huyu nae kaamua kugiita yesu lakini YESU wa halali hakuwateka watu kwa upanga,vita n.k aliwaita kwa upole hivyo na huyu yesu feki asinge toa roho za watu

    ILA ALICHOFANYA SAWASAWA MANA ANATETEA ROHO ZA WATU

    KAMA HAWATAKI KUZAA KWANINI WASITUMIE KONDOMU?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2009

    SAFI BWANA YESU FUNDSHO KWA WAJINGA WENGINE HASWA BONGO kama utaki kuzaa kwa nini unachanua alafu unakwenda kuua hatari kweli kweli

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2009

    Jamani hii habari sio ya ukweli. Ni habari ya kutungwa tu inatoka kwenye jarida maarufu la story za kutunga linaloitwa The Onion.

    http://www.theonion.com/content/index?utm_source=nav

    Mnyepe

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2009

    we anoni wa 12:04 kondomu za nini tena? Kondomu hazina flavour. mungu alipotuumba hakutuvalisha kondomu ndio maana ukivaa kondomu libeneke hulipati live mwanawane. lile joto stahiki hulipati kabisa so fogeti abauti uzing'i kondomu.
    ushauri unaotakiwa kuutoa ni jinsi ya kucheza kwa stepu. waambie hasa wasichana waijue vizuri ile penati box yao ili basi wakishaingia ndani ya penati box yao wajichunge na uchezaji rafu usio na ulazima sababu utawasababishia penati na kujikuta wakipigwa bao la kizembe chini na uvimbe ukitokea juu na adhabu zake sasa ndo kama hivyo jesus anawashukia!!! jamani kina dada msifanyage makosa ndani ya kumi na nane la sivyo muwege tayari hata kulea watoto jamani. mkumbuke kuwa mama zetu hawakututoa ndo mana leo hii tunawaheshimu na kusema nani ka mama!!!
    Ahsenti
    Kamuzola

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 08, 2009

    Na wewe MNYEPE uwe unaandika kitu ulichokuwa na uhakika nacho. Hii habari imetangazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwani wewe huoni? OOOooooopppsssssssssss samahani kumbe gongola mboto hampati habari za kwa OBAMA pole weeee kalagabaho.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 08, 2009

    Kama hiyo story ni yakutungwa sawa huyo ametuweza kweli kweli. Ila kama ni ya kweli ni hatari. Ila tuwe makini kwa lolote wakati wowote na ningependa kusema hivi:-

    Wakati mwingine binadamu tusipuzee hii hali ya kawaida eti ukamuona binadamu wenzako ukadhani kuwa hata Yesu / Nabii Issa atakuja wa maajabu labda kila mtu ambaye utamshangaa labda atakuwa tofauti. NOOO. Tujue kuwa Nabii atakuja kama mtu wa kawaida kama mimi na wewe. Na pia malaika wkt wote kama ilivyo katika Masahafu na Biblia huwa haendi kwa mtu kama malaika wkt mwingine anaenda kama binadamu.

    Mfano wa kisa kimoja cha Tajiri na maskini ktka hadithi za mitume kwa ufupi naeleza kinasema hivi:

    Maskini alikwenda nyumbani kwa tajiri akiwa mchafu saana alipofika akamkuta tajiri na kuanza kuomba msaada wa chakula. Tajiri yule bila kujua alimfukuza masikini yule km mbwa kwa kuwa alikuwa ni mchafu na anachafua nyumba yake iweje walinzi wamruhusu kuingia. Aliwaamuru wafanyakazi wake wamtoe nje yule masikini. Baada ya yule tajiri kufanya vile muda ulipopita Mw.Mungu akamfanya akawa yeye ndio maskini, akamuondolea rizki na yule Maskini akawa tajiri yeye ndio akaenda kwa yule aliyekuwa maskini kuomba msaada. Maskini yule akamwadithia kisa kile.

    Huu ni mfano wa malaika kugeuka kuwa watu. Hivyo tusione pia baadhi ya watu wanaokemea maovu tukawapinga. Ni watu lakini roho huwezi jua km ni Mungu amemwagiza. Tujiulize; Je Mw. Mungu alipoangamiza vizazi vilivyopita kwa dhambi je yeye alikosea kuuwa watu? Tujiepushe na dhambi hatujui wkt gani Kiama na wakati gani Nabii Issa / Yesu atarudi.

    Tunaambiwa Massiydajal atakuja atajifanya yeye ndio Mungu na wale wenye dhambi watamuamini wasio na dhambi watampinga na kuuliwa. Sasa wewe kwanini uunge mkono dhambi hizi? Jifikirie, fikiria maandiko ya Biblia/Masahafu. Fikiria hadithi / visa vya manabii upate taswira ya leo nini kinatokea.

    Mtazamo wangu wasije kumtesa sana mtu huyu. Wamtumie mtu huyu kumchunguza. Waende taratibu Wafikirie pande mbili.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 08, 2009

    Tatizo binadamu tumezidi dhambi hivyo hakuna atakaye support hilo hata mmoja. Hivi nyinyi mnataarifa kuwa Yesu yupo karibu kurudi? Je wewe binadamu unahakika Yesu akirudi atakujulisha kwa kukupigia simu? Je unahakika kuwa utamjua? Tuweni makini jamani. Tusiende pupa

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 08, 2009

    Duh! Ahsante kaka Michuzi kwa kutuletea hiyo habari. Iwe ni kweli iwe ni uongo story hiyo. Ila ni kuwa pia tumekumbushwa kuwa binadamu wamezidi dhambi. Tuacheni jamani hatujui mwisho lini. Hatujui Mweshimiwa atakuja lini. Yani hii ni hatari kweli kweli Hospitali kbsa maalumu kwa utoaji mimba????? inatisha. Tunakoenda kubaya.

    Haya kwa wale wanaounga mikono mambo ya kidhungu ungeni mikono.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 08, 2009

    watu mna MAPEPO SANA umu blogun

    na uyo feki yesu
    ila utoaji mimba ni UUAJI,na obama wenu ndo yuko ktk mstari mmoja wa kutoa ruksa,akaishi arabuni

    ReplyDelete
  21. Maoni yangu kama Mkristo:

    Huyo mtu aulizwe jina lake halisi, maana marekani si ndio wanaojifanya kuwa ni mabingwa wa ku-keep records?

    Hasiukumiwe kama YESU KRISTO, la sivyo marekani mtamjua mungu ni nani, mtalipa dhambi hii. ya kumdharirisha mwana wa Adam

    Fanyeni utani na vitu vyote sio hii ya kumuita muuaji ni Yesu Kristo?

    Simo kwenye dhambi hii mimi na kizazi changu na mungu wangu ni shahidi

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 08, 2009

    hivi yesu (issa) anajua kutumia bastola au bunduki? kali kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...