dogo yuko juu, si mchezo. mapromota ughaibuni mpo???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2009

    Kijana yuko juu! wimbo umetulia, thanks kaka Michuz kwa kuturushia kibao! Keep it up Marlaw.

    ReplyDelete
  2. Nami nakubaliana na maoni yako. Kijana ni mwimbaji mzuri. Juzi niliupiga huo wimbo wa "Pii pii" kwenye mkusanyiko wa TZ niliowaalika nyumbani kwangu hapa kijijini, wengi ilikuwa ni mara ya kwanza kuusikia lakini waliupenda sana.
    Kwa maoni yangu Marlow ana uwezo sana kama alivyo Ali Kiba, ila hajabahatika kupata promota mzuri.
    Natumai hali hiyo itabadilika hivi karibuni.
    Kazi nzuri Marlow!
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2009

    Marlaw upo juu sana. Kila la kheri katika kazi yako ya mziki, ninaamina mafanikio makubwa utayapata muda si mrefu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2009

    marlow anatisha kuliko kiba... hata kwenye maconcert ya kimataifa dogo anakubalika Yaani kwA kifupi HABAATISHI,,,,,!

    MALAYSIA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2009

    wimbo mzuri sana marlaw...
    umejitahidi kwa kweli..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 23, 2009

    naona mnamtafutia soko la shoo za nje kwa nguvu zoote!!! si kazi baadhi ya anonis hapa ni michuzi mwenyewe na nyingine ni zake mwenyewe! teh teh teh!!! dogo ngoja nikakuuze leo kwa promota mmoja hapa ujerumani

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 23, 2009

    Kaka Michuzi shukrani sana kwa kutuwekea kibao MURUA cha Marlaw, kwa kweli kijana Marlaw yuko juu sana, yeye si mbanaji pua kama vijana wengine wanaopenda kuwa marekani au ulaya kila kukicha, Marlaw unamuona kama anaimba na sauti yake natural.

    Keep it up Marlaw!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2009

    Muziki mzuri sana. It really made my day haswa ukiwa mbali na nyumbani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2009

    safi sanaaaaa
    keep it up dogo!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2009

    Wimbo mzuri sana, una melody nzuri, maneno mazuri ya mapenzi. Video nzuri pia inatukumbusha nyumbani sisi tulio mbali, barabara za Dar, daladala, traffic lights, bajaj lakini zaidi ni lile kawa na maneno yake. Umefanya vizuri kwa wimbo na video pia. Keep it up!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 23, 2009

    nice tune,
    shame that the same cannot be said about the video

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 23, 2009

    Ndiyo, kijana anajiweza sana hususani katika sauti yake duuh!
    Mashairi yanaimbika na wimbo unachezeka inategemea audience yake huwa inaguswa na kipi,BUT mashairi sometimes yanajikanganya so ni hilo tu otherwise hes guuuud

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 23, 2009

    Mnyalu mwenzangu uko juu sana mtu wangu kuliko Kiba..maringo tu kama demu ..........Marlow juuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 23, 2009

    EXCELLENT SONG! Nimeupenda sana.

    Kwa huyo aliyom-compare na Ali Kiba, shame on you! Kila artist ana style yake and they are both good in their own way.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 23, 2009

    Nashukuru Bro. Michuzi kwa kutuma hewani huu wimbo na video yake! Kijana huyu ametulia na mziki wake ni mzuri sana ana sauti ya GOLD I can see a lot of pontentials in this guy!! Nimekuwa nikisikiliza wimbo huu na nimekuwa nimeurudia mara kwa mara mpaka track inakwaruza. Nilikuwa ninafikiria kumiliki huyu bwana na atafanya biashara nzuri sana. Kwa huku marekani ninamfananisha na waimbaji kama Akon, na John Legend. Nitamshukia bongo huyu kijana na kuzungumza naye business.
    Katika wanamuziki wanaoimba nyimbo za kusisimua na zenye mantiki huyu ni mmoja wao.
    Keep it up!
    Mdau USA

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 23, 2009

    naah, no way

    ReplyDelete
  17. Kwa Ujumla Marlaw yupo juu zaidi ya Ali kiba, Umesikia wimbo wake wa Bembeleza, ukitaka kupata tungo zilizopangiliwa sikiliza Marlaw. Asante kwa kutuweka sawa leo kija, kaza Buti gemu bado ni gumu

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 23, 2009

    du dogo yuko juu kibao chake kimenibamba kweli kweli

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 23, 2009

    Nyote niutoto unawasumbua mkikuwa mtaacha

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 23, 2009

    Dogo yupo juu kuliko maelezo.Ila kuna kitu kimoja tu ambacho lazima niseme.
    Wimbo ni mzuri mnoooooo,lakini video haijanifurahisha,hakuna creativity,nilitegemea kuona video inayoreflect ubora wa wimbo.Nina maana jinsi wimbo ulivyo mzuri,basi video nayo haikuwa na budi kuwa nzuri vilevile.
    Jamani hii ni constructive criticism yenye nia ya kumjenga huyu bwana mdogo.

    Mdau

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 24, 2009

    Nyimbo kali kinoma lkn video bado...Shooting bado bado naona, we need improvements in that area.

    pia wasanii wangeanza kucheza, ktk hiyo video naona wanacheza style ya mwaka 2002 ambayo iliingia bongo kutoka Jamaica.

    Tukitaka kushindana kitaifa inabidi tuongeze nguvu. Waganda wenzetu wamejaribu...Mfano mzuri Obsession girls.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 24, 2009

    Yangu macho tuu katika jamii hii ambayo imeshasalimu amri katika kitu chochote kinachohitaji kutumia akili.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 24, 2009

    hivi huu wimbo ni wa kiswahili au kiingereza?

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 24, 2009

    jamani mi laptop yangu ni aje????!!! nikipiga nyimbo hii sisikii sauti, naona kale kamshale kanakwenda mble freshi lakini sisikii chochote!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 24, 2009

    MARLAW YUKO JUU ZAIDI YA ALI KIBA
    SIKILIZA
    BEMBELEZA, RITA, PIPI NA NYINGINE NYINGI TU.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 24, 2009

    nISIPOSEMA NENO NITAKUWA MCHOYO WA FADHILA. KWA KWELI kijana yuko juuu sana. wimbo huu ukipigwa wanangu wananiambia mama wimbo wako unapigwa njoo usiklize. basi kwa mapenzi hayo wakaurecord nikirudi tu nyumbani baada ya salaam dogo ananiwekea, nikamuuliza ina maana hii nyumba kila nikiingia huu wimbo ndio uko hewani? wakasema hapana tumekuwekea kwenye laptop yako dada anasema atakuburnia cd.

    SO U CAN IMAGINE HOW JUU THE BOY IS TAKING SOME of US WENYE MATUSI KAZI KWENU.KUCHANGANYA LUGHA na letters SIO ISSUE. issue ni burudani.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 24, 2009

    wal'ai unaweza acha mumeo utoke na uyu mtoto

    aisee kijana,unawaweza mashoga mami??

    me nimekupenda nataka nikutunze baby boyyy

    yan huu wimbo uwa nacheka tu,jinsi unavonikuna

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 24, 2009

    majina yake kwa urefu plizzz

    bela u wa kuboma?mwagito wewe?

    u mwa nani?

    mithupu usibane hii acha wanyalukolo wanijibu

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 24, 2009

    habari mkubwa?
    me namtaka kijana nimfanyie mpango aje uku ughaibuni kwa tour, vp ninaweza kumpataje? kama una mobile no yake au email nidondoshee mkuu, my email is jibaba@hotmail.co.uk

    Thanks in advance

    Mdau No 1

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 25, 2009

    We annoni wa June 24, 2009 7:08AM nenda kwenye device manager kisha update drivers za sauti lazima utakuta zina alama ya kuuliza yenye rangi ya njano, jaribu ku update ukiwa online,ukishindwa tafuta drivers za aina ya computer yako. mfano kama computer yako ni dell latitude D600 hakikisha unatumia driver cd ya computer aina hiyohiyo vinginevyo waweza crush computer yako.
    Marlaw na Ally Kiba wote jamii moja na wote wanajitahidi. Hongera kwa kila mmoja wenu

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 25, 2009

    Asante bro michuzi kwa kutuwekea hii videoz ya marlaw
    kifupi dogo anajitahdi bt watu wanaocomment hawazingatii kilichowekwa na kuchangia wanachokiona ulichoweka Michuzi ni blah blah tu nyingi kwa walio wengi,nauliza y most of the comment alikiba na marlaw?
    kwani michuzi anashindanisha hapa? si ni vid ya marlaw?
    Wabongo tuache malumbano km marlaw yupo juu zaidi na anahitajika ughaibuni km mwenzake ali then tym yake itafika na matangazo tutayaona kwa bro michuzi,so nachoshauri tuwe na cha kuongea na sio blah blah,tukumbuke hatuna wanamuziki wengi toka Tz wanakwenda ughaibuni km wenzetu wakenya so tujitahdi kuwasaidia wasanii wetu wa Tz kwa promo ktk media zetu na tununue kazi zao ndio tutafanikiwa haraka haraka kuwa na wasanii wengi watakaoenda fanya show nje,marlaw umejaaliwa kipaji lakini ongeza juhudi uwe na nyimbo nyingi za kuweza piga show ya masaa mawili au moja na nusu,navyojua una album lakini track zinazojulikana ni 3 tu,so jitahdi mdogo wangu ili nawewe ututoe wabongo kimuziki,video yako sikulewa vizuri y umeamua kufanya story sehemu mbili au ni kulitafuta soko la kenya na tz?
    Navyowajua wabongo wataongea sasa hivi kama ilivyo alikiba au hussein machozi......big up kwako
    Mungu ibaririki Tanzania Mungu ibariki Bongo fleva
    MDAU WASHNGTN DC
    Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...