muvu ya goli la pili ilianzia kwa mrisho ngasa aliyeshusha majalo iliyomdondokea mussa hassan mgosi
mgosi akampiga tobo mlinzi wa new zealand na ngoma ikamkuta mwinyi kazimoto nje ya 18

kazimoto akamcheki kipa amekaaje akaachia nduki kali iliyokwenda nyavuni moja kwa moja
mgosi alikuwa wa kwanza kusherehekea baada ya ngoma kugonga nyavu na kurudi graundini
jamaa nusu walie....
shujaa kazimoto alihemewa...
kicheko kila kona. waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. george mkuchika na mbunge wa singida mjini mohamed dewji wakipongezana huku mkurugenzi wa ufundi wa tff sunday kayuni akiachia hadi jino la mwisho
mwenyekiti wa yanga imani madega (shoto) na mh. mohamed missanga (kulia) wakijiunga na mkuu wa mkoa wa kipolisi kanda ya dar selemani kova na afande mstaafu alfred tibaigana wakisherehekea. tibaigana ni mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya tff kwa sasa
kina dada nao walikuwepo kushangilia ushindi wa stars










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2009

    Mzee wa Libeneke nimezikubali taswira hizi hasa ya Mrisho Ngassa akiwafungisha tela Weupe Watupu wawili hapo chini, Dihile akikamata mpira na chuma kilivyotinga ndani ya kimia.
    Endeleza libeneke mwanangu.

    ReplyDelete
  2. Taswira zimetulia babake.Utadhani ni ndani ya emirates.Taifa starzz kaza buti kuleni vinyesi baada ya miaka miwili lazima tutie timu ndani ya Africa Cup of Nations.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2009

    broo michuzi pole kwa kazi !

    hongereni taifa star lakini ukweli hapa tunajidanganya newzeland wapi na wapi na kabubumbu hawa ni rugby cricket na sio football.

    hata ukiangalia fifa world rank utajua tumetwanga maji bora hata tujipime na burundi ama rwanda.

    sikandii lakini ukweli ni huo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    Wenzetu Nigeria ijumaa wamecheza na Ireland matokeo moja moja na jana wamecheza na france ikiwa full mkoko na kuilaza moja bila.sisi tunacheza na watu wa Rigby,hawa hawana tofauti na Vancouver ya Canada.
    mdau Kisiju.

    ReplyDelete
  5. Al MusomaJune 04, 2009

    Mimi tu au mwandishi hajatuambia ni magoli mangapi tumeshinda? Hata hivyo nashukuru kuona ushindi maana juzi niliota tuko sare na Afghanistan hadi dakika ya 89 alipopachika goli talibani mmoja mwenye kilemba cheusi. Japo ilikuwa ndoto tu iliniuma...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    Mzee wa kukandia hatujatwanga maji kwenye kinu. Nimeangalia fifa world rankings nikaona ziko hivi:
    Tanzania:
    31 kati ya 52 kwa Afrika
    ya 109 ulimwenguni kati ya zaidi ya 200.

    New Zealand:
    1 kati ya 11 kwa Oceania
    82 kati ya zaidi ya 200 ulimwenguni.

    Kwa hiyo tumempiga bao mtemi wa ukanda wa Oceania na FIFA wanaiona timu hiyo ni kali kuliko Zambia, Rwanda, Angola, Kenya, El Salvador na Liberia. Japo ushindi huo sio sawa na kuwafunga Ghana au England lakini walau utafanya mataifa yaliyo juu zaidi kisoka yakubali kucheza mechi na sisi, au pengine hata kuomba wao mechi. Tungepigwa tunapigwapigwa mabao basi hata kupata mechi za kirafiki na Djibouti ingekuwa tabu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    Mzee wa kukandia hatujatwanga maji kwenye kinu. Nimeangalia fifa world rankings nikaona ziko hivi:
    Tanzania:
    31 kati ya 52 kwa Afrika
    ya 109 ulimwenguni kati ya zaidi ya 200.

    New Zealand:
    1 kati ya 11 kwa Oceania
    82 kati ya zaidi ya 200 ulimwenguni.

    Kwa hiyo tumempiga bao mtemi wa ukanda wa Oceania na FIFA wanaiona timu hiyo ni kali kuliko Zambia, Rwanda, Angola, Kenya, El Salvador na Liberia. Japo ushindi huo sio sawa na kuwafunga Ghana au England lakini walau utafanya mataifa yaliyo juu zaidi kisoka yakubali kucheza mechi na sisi, au pengine hata kuomba wao mechi. Tungepigwa tunapigwapigwa mabao basi hata kupata mechi za kirafiki na Djibouti ingekuwa tabu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    MWAMBIE KOCHA AILETE INDIA SASA MAANA ND'O KIBOKO YA SOKA. HAO NEW ZEALAND WANATAMBA SANA KWA SOKA LA MABAVU LAKINI HAPO TUMEWAFUMA. MAXIMO LETE INDIA. CANADA TAYARI, NEW ZEALND NDO HIVYO TENA....BADO INDIA TU THEN INDONESIA, THAILAND, HADI WATUKOME. KUDADEKI

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    JUNE FIFA WORLD RANKINGS: NEW ZEALAND 82; TANZANIA 109.

    THIS IS CRAZY. HII NCHI HAIJULIKANI KABISA KATIKA WA SOKA ZAIDI YA RUGBY NA KRIKETI LAKINI IPO NAFASI YA 82.

    TANZANIA INAYOJULIKANA KWA KUCHEZA SOKA TU (RIADHA NA NGUMI KWISHNEHI) IPO NAFASI YA 109. HAYO MAENDELEO YA MAXIMO YAPO WAPI?

    TUJIULIZE WAJAMENI SIYO KUKENUA KENUA MENO TU KAMA NGIRI ALIYENUSURIKA KUNG'ATWA MATAKO NA SIMBA AU CHUI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    Mdau hapo juu kwa kukandia umejaliwa, yaani wewe hata huoni aibu....yaan ukweli pia hutaki kukubali haya bwana, kuna wengine ubishi ni jadi yenu bwana.

    ReplyDelete
  11. Massoud Jr.June 04, 2009

    Mzee wa libeneke, mh. DC wa Tegeta nakufagilia kwa taswira ulizotutumia wadau wako.
    Hiyo yaswira ya mwisho ya akina dada wanazi wa soka imenikuna sana kwa jinsi wanavyoonekana kuwa makini katika fani.
    Natamani niwe na mawasiliano na mmoja wao ili tubadilishane mawazo kila baada ya gemu kama hii.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    Watanzania wenzangu sijui mnataka mpewe nini zaidi.Mimi nimefurahi sana kwa sisi kuifunga New Zealand. Kwa kifupi,ni kuwa wana rank juu zaidi yetu katika fifa standings,kwahiyo taratibu, next time tutacheza na timu nyingine,na next time nyingine,hivyo hivyo hadi vijana wawe na experience ya kutosha. Nyie mnataka tuwafunge England,Italy,Brazil ndo mshangilie nchi yenu? Jifunzeni kwa wenzetu wa Bafana Bafana,wao siku zote wako na timu yao, hata kama ikiifunga Sudan,kwao ni ushindi mzuri na wanasherehekea. Nasikitishwa na wadau wanaona huu ushindi si muhimu.na huyo aliyeifananisha Tanzania na Nigeria, nadhani akili zake za kimpira bado ni changa sana.Nigeria wameenda world cup mara kibao,mabingwa wa afcon,wana rank juu duniani, kwahiyo wao kuifunga france,ni kitu cha kawaida coz huwezi fananisha wachezaji walio nao na sisi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    "WAJAMENI TWENDENI MBELE TURUDI NYUMA" MNALIONAJE HILI KWENDA MPIRANI NA SUTI JAMANI? HII IMEKAAJE?
    MPIRA ULIKUWA USIKU ,INA MAANA HAWAKUPATA MUDA KWENDA KUBADILISHA?UNASHANGILIAJE HUKU UMEVAA SUTI JAMANI , HAIJATULIA

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2009

    MAKISIMO afukuzwe anakula tu hela zetu, juzi tu tumefungwa na Congo halafu anatuletea timu ya Rugby icheze footbal? Tusimpe muda tena.
    Wabongo hapo tumeliwa..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 04, 2009

    USHINDI NI USHINDI TU HATA WA NUSU GOLI NA HAUJALISHI UNACHEZA NA NCHI GANI.

    KINACHOKERA NI WATU KUIKANDIA TIMU HATA KABLA YA MCHEZO HAUJAISHA. MMEABIKA.... KULENI MATAPISHI YENU. HONGERA STARS JK BOYS

    ReplyDelete
  16. nakerwanamashabikiJune 04, 2009

    Lini wabongo tutaacha upuuzi huu wa kuizomea timu yetu!! ni timu gani ambayo kila mechi inashinda! hata man u iliyo klab bingwa duniani hua inachapwa na vitimu kama fulham! Tuwe na uzalendo, kufungwa goli moja la penalti watu mnaanza kuzomea, si mngezomea hadi mpira unaisha basi! Upuuzi mtupu!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 04, 2009

    Watanzania tunatakiwa tuelimike. Kuwa wabishi kwa jambo linaloonekana wazi sinzuri kabisa. Kwa mtu yoyote anayejua mpira anaelewa timu yetu ilipofikia ni pazuri sana. Zamani tulikua tunaenda uwanjani kwa kuwa tunapenda mpira tufanyeje ila saizi kwa kweli tunafurahishwa na kiwango walichofikia wachezaji wetu. Kwa kifupi wale wanaosema New Zealand si timu nzuri basi hata wakisema waje Brazil au England na tukafanikiwa kuwafunga watasema waliokuja si wachezaji wenyewe. Naombeni tujiamini tuipe timu yetu sapoti ili tuzidi kusonga mbele. wacheni kuwa wagumu kuelimika jamani tusonge mbele. Tuipende timu yetu. Tuache chuki binafsi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 04, 2009

    Misoup hao uliotuwekea ni kina Dada au Kinamama.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 04, 2009

    Refa iliwaonea wazungu, goli la kusawazisha lilikuwa offside

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 04, 2009

    maoni ya coach wa newzealand ippmedia" Kocha wa New Zealand, Hurbeth Ricki ameisifia Stars na kueleza wachezaji wake wengi hawakuwa wa kikosi cha kwanza na aliwapa nafasi ya kucheza ili waweze kuelewana".

    link: http://ippmedia.com/Stars yawapa raha Watanzania

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 04, 2009

    Kwa mdau unayezungumzia kwenda mpirani na suti..Ni kwamba gemu ilipangwa kuanza saa moja kamili jioni na ni siku ya kazi..kwa hiyo kama unaijua Dar vizuri,hiyo ni mida ya foleni so kwenda home na kuchange ikawa ngumu for most of us..kwa hiyo tuwie radhi,tunajua nini cha kuvaa mpirani..hata hivyo sio issue kiivyo babu..Mzungumzie huyu anayejiita mkurugenzi wa ufundi wa TFF,ambae anafanya flops mbili kubwa within a week kwa kuitoa Tabora kwenye Taifa Cup kihuni na kumtangaza Chuji mfungaji bora na kumsahau mwingine waliyefunga mabao sawa.. Yaani kufanya tallying ya magoli ya mashindano ya wiki 2 tu huyu jamaa ameshindwa.Kayuni are you really serious?Inua game yako kaka,watu wanakuheshimu sana..

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 04, 2009

    Heee na huyu nae eti unashangaa mtu kwenda na THUTI mpirani we vipi? Ushishangae Tz shanga hata nchi za wenzetu ukiangalia mechi utawaona wazungu wamevaa suti na wako uwanjani. Hebu wacha upuuzi. Unakosoa watu pengine wewe hapo unaenda na bukta ofisini.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 04, 2009

    HEEEE KUMBE TULILUDISHA NA KUFUNGA ZAIDI MAGOLI???

    aiseee safi sana,

    mko juuuu vijana excellent Taifa stazzzz maxomo safiiii

    office chairs kama kawa uwanjani hahahaaa

    afi kila izi mechi zikiwepo me sipo,sijawai ingia ilo wanja natamani saaaana

    asante

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 04, 2009

    Kaka michuzi hao ni kina mama. Tofautisha kati ya kinadada na kinamama. Hao hawakosi umri juu ya 30 huoni sura zao?? Weshaondoka katika age ya udada. Tofautisha kati ya kina dada na kina mama kaka.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 04, 2009

    Hivi kweli watu wengine wanakosa yakuzungumza wanazungumzia mavazi kweli,huyo anaye zungumzia suti ni mpenziwa football na huwa anaangalia game za nje ikiwa makocha wana vaa suti uwanjani ita kuwa watazamaji,wabongo tuna kasumba yakudharau kila kinachofanywa na waliokua hom kisa tu mtu yupo ulaya ama america,matokeo yake hatuoni kile tunachozungumzia ni pumba kutokana tu na ushamba wa kua nje ujione mjuaji get life dawg

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 04, 2009

    jamani nimefurahi sana kumuona huyo dada wa chini aliyevaa miwani ni dada yangu Ronica mimi ni mdogo wa rafiki yako tulikua tunakaa sinza lkn sasa hivi nipo uk

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 04, 2009

    kazi nzuri, bongo teknohama inakua....

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 05, 2009

    mama,mama yako mzazi

    koma wee kijeba apo juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...