Baadhi ya wajasiliamali wadogo wakigombea kununua samaki kutoka kwa wavuvi wa Bwawa la Mindu, lililipo Manispaa ya Morogoro wakiwa wamejitosa majini ili kuwawahi kabla ya kufikishwa nchi kavu, hali hiyo inatokana na uhaba wa upatikanaji wa samaki kwa kipindi hiki kutokana na mwanga wa mwezi nyakati za usiku. Baadhi yao wanatoka maneo ya nje ya Manispaa hiyo ikiwemo Tarafa ya Mlali, iliyopo zadi kilometa 25 kutoka mjini Morogoro.
Vijana hawa wanatunga samaki wadogo kwenye kamba baada ya kuvuliwa kutoka Bwawa la Mindu la Mjini hapa, jana tayari kwa kwenda kuwauza sokoni. Hivi sasa samaki katika Bwawa hilo ni adimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kipindi cha mwana wa mwezi. Picha na mdau wa mji kasoro bahari, John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    Umenikumbusha home mkuu
    Hapo walkipo ni karibu na Iringa rd.
    Kule kwenye minazi ni usawa wa mzinga jeshini wakate kulia kwake ni kijiji cha Tangeni na chuo cha IDM Mzumbe
    Mwelekeo wa kushoto kwa hiyo minazi ni chuo cha SUA
    Hiyo milima ndio iliyowahi kuimbwa na Mbaraka "maji ya tililika usiku na mchana"
    I love the Morogoro
    Its ma home

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    duh mtalaam unaijuajua moro kimtindo. lakini kwangu huoni ndani mi mji kasoro bahari ni kama chupi na uume!!

    ReplyDelete
  3. Hawa vijana naona wanautani na Magufuli,atawashukia kama Kunguru kaona kifaranga.Mkwara wa kwanza ni kukatakata hiyo ndoana,kisha kuwaambia walale chini awatandike fimbo akumbushie enzi zake za ualimu pale Sengerema sekondari,kisha awaambie wakimbie Shule maana wametoroka shule hao.Hapo atakuwa amewahurumia sana badala ya kuwapeleka polisi kuwafungulia mashitaka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2009

    Picha na habari hii inaonyesha ni jinsi gani tanzania msoto ni wa kutisha.kweli ni the poorest country in the world.

    Serikali,pls,pls

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...