Bro Michu!!
Habari za masiku. Ulikuwa RSA na nilitumai kabisa kwamba sasa ingekuwa nafasi nzuri wewe kupitia huku niliko, lakini bahati mbaya tiketi ya bei poa toka Jozi mpaka Zenjibari ilikufanya usahau kama nipo huku. Yote heri yakhe, iko siku najua utatia timu huku pia.
Habari za masiku. Ulikuwa RSA na nilitumai kabisa kwamba sasa ingekuwa nafasi nzuri wewe kupitia huku niliko, lakini bahati mbaya tiketi ya bei poa toka Jozi mpaka Zenjibari ilikufanya usahau kama nipo huku. Yote heri yakhe, iko siku najua utatia timu huku pia.
Nimetumiwa email kibao yenye picha na maelezo ya kupatikana kwa Nanihii na nimestushwa sana. Nina hakika kwa maelezo hayo huyu ndiye aliyekuwa mmilika wa hiyo Nanihii iliyokuwa ikinanihii sana wadau kile pembe ya dunia.
All in all bado ngoma nzito maana sheria za nchi hasa kuhusu hii teknologia bado haijawa sawa sawa sana, na si kwetu tu bali nchi nyingi bado hazijawa makini kisheria na mambo haya ya utandawazi. Nafurahi kusikia JK kaliona hilo na kaamuru lifanyiwe kazi mara moja katika ujio wa mkonga wa mawasiliano (fibre optic) ambao nasikia karibu utaanza kazi hapo Bongo.
Naona swala la Nanihii limefikia pahala ambapo sasa wanasheria wataamka na kuona kwamba kuna haja ya kufahamu kiufundi zaidi mambo haya ya habari huria kupitia Internet.
Mimi nimefanya kazi nyingi tu hapa nilipo za Information Forensic kwenye kitengo cha Police Special Crime Squad. Nina mengi ya kusema kuhusu swala kama hili na namna ya kulifuatilia ili sheria ichukue mkondo wake.
Kwa utashi wangu mimi ningependa sana Tume Ya Sayansi (COSTECH) wangesimama kidete na kuwa na kitengo cha research cha mambo kama haya ili kiisaidie serikali. Yaani iwe inafanya kazi za technology reserach kama vile wanavyofanya CIA ama FBI. Najua hilo lnawezekana ila nashangaa kwa nini hakuna kinachoendelea. Inatia uchungu.
Nasema tena, hili linawezekana sana Tanzania ila bado hatujawa na uzalendo tosha kuingia katika mambo kama haya na pia tumelele fofofo, japo wapo wengi wanaodaiwa kuwa ni wataalamu wa mambo haya. (ninaomba mnikosoe ila msinielewe vibaya, hii ni katika kuita kijiko kuwa kijiko, na sio sepetu).
Hakika bado tuna mengi ya kujifunza na hivi sasa ndiyo imekuwa zaidi maana kwa Tanzania sasa tumevamiwa na Technology lakini bado hatujaona pa kukimbilia bali kufumbatia Technology yenyewe. Yaani sijui ni lini tutaamka na kuanza kuchakarika kama wenzetu wa Rwanda, Kenya na kwengineko.
Pamoja na ukweli kwamba wapo Polisi hapo Tanzania ambao wamehudhuria warsha nyingi tu za FBI kuhusu maswala ya Information Forensic, lakini bado wanahitaji msasa mkubwa kwenye kazi hiyo na siyo kwenda kuishia kwenye warsha na kuongelea ama kumsifia mtoa maada kwenye warsha kuwa ni mjuzi ama vinginevyo na kumpigia makofi tele. Kuna mengi ya kufanyka kivitendo.
Sipendi sana kuchangia hadharani mambo kama haya lakini ipo siku nikipata scenario best for this kind of talks, nitajitahidi kuelimisha. Na bado ninasubiri kupata a good link kwa wahusika na nina hakika I will drive a good point interms of Information management on the technology side. Siyo kwamba wahusika hawana washauri ila kila mshauri ana namna yake ya kufikisha ujumbe na nia yake ya ujumbe kufika.
Tumuombee Mungu huyo Nanihii maana kesi iliyo mbeleni kwake ni nzito.
Salaam wote
Mdau Nanihii
Ile email ni hoax. Nanii yupo mtaani anadunda tu.
ReplyDeletesi mseme tu ze utamu kadakwa?
ReplyDeleteserikali itam-charge na nn?wtss the charges??
ReplyDeleteMdau, mimi sikufahamu vizuri, ila kwa mambo ya research na kupata watu wa kufanya nao kazi yenye mtizamo wa kuwasaidia watanzania, mtafute mtaalamu mmoja yuko london, amebobea kwa mambo ya utafiti. Anaitwa Dr. Shayo. Endapo hujapata kumzikia, basi jitahidi uwasiliane naye kwani jamaaa aliwahi kutoa dodoso, kuhusu uboreshaji na ufundishaji wa kikosi chetu cha polisi siku za nyuma. Ninaamini kamisa jamaa huyo uzoefu wake wa utafiti Africa na ulaya mtasaidiana katika kubadilishana mawazo.
ReplyDeleteNi kweli hii sekta ya sheria na mambo ya mtandao bado ni kitendawili, hata huyu mhusika wa "hiyo nanihii" ambaye kwa sasa anatuhumiwa itaiwia vigumu kwa kutumia sheria za sasa kumshitaki.
Ushauri, mtafute dr. shayo, si mchoyo wa ushauri na you will see the matunda ya mawazo yako.
Kwa wataalam washeria, tunajuwa kwamba huyu nanihii hana kesi kubwa (kama unavyodai), zaidi atapata usumbufu tu!
ReplyDeleteKwanza lazima uelewe kwamba hawezi kushtaki kwa sheria ya makosa ya jinai, coz haja jinai aliofanya, hivyo kama serkali haina uwezo wakumfungulia kesi! Anaweza kushtakiwa tu, kama kesi ya madai, na hii inabidi muhusika aliekashfiwa aende kufunguwa kesi hiyo ya madai. Kama watamshataki kwa kosa lakumkashifu mkuu wa nchi bado ni (madai) na huyu jamaa atashinda kwa kishindo cha ajabu (kwani katika post ile alikuwa makini sana, hakuna sehemu alotaja jina kwamba huyo ndo mkuu wa nchi hii). Kwa wale wahanga wengine, walowekwa picha zao, na majina yakaandikwa wanaweza kupiga kelele lakini pia kama wote walikuwa na umbri zaidi ya mika 18 basi pia wataanguka vibaya kwenye kesi hii! Kama ulivyosema hakuna sheria ya udhibiti wa technologia hii ya mtandao, bado hawana uwezo wa kumtia hatiani, kwani alifanikiwa kutekeleza sheria ya kuendesha mtandao wake ikiwa ni pamoja na kuweka onyo la aina ya mtandao anaoendesha na watu wanaoruhusiwa kuangalia...!
Kufupisha stori, kesi ya huyu jama ni ndogo sana, afadahli hata kesi ya mama ntilie wanaokamatwa na mgambo ni kubwa (coz kuna mahakama ya jiji) kuliko kesi ya huyu jamaa, ambayo hakuna kifungu cha sheria kinachoweza kumtia hatiani!
MWANASHERIA!
Swali kwa wanasheria
ReplyDeleteje?sheria za kimataifa za uhalif zinasemaje kuhusu sehemu anayostahili kushitakiwa huyu jamaa?
Je atashtakiwa Tanzania au Uingereza ulipo uraia wake?
Nakumbuka aliyempiga Rais wa marekani kwa kiatu.alishtakiwa pale plae kwao..iraq kama skosei.na akahukumiwa miaka mitatu na sio marekani alipo rais bush.
so mi naona hatoshtakiwa bongo kama wengi tunavyodhani.kama ni kushtakiwa itabidi iwe uingereza.
na je kwa kosa gani?
Ni swali tuu
Kwa Wale wanaosema Kilimanjaro haitangaziwi kama Tanzania tizameni hapo http://www.youtube.com/watch?v=uX-joc_O9X4 CNN NEWS Wanatangazia.
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=uX-joc_O9X4
ReplyDeletejamani hamumtaji huyu Male wa zeutamu mnaishia kusema nanihii nanihii kwani hamjui alivyowatesa watu na mtandao wake mchafu wa kichonganishi na usio na maadili, Michuzi kwanza ulitakiwa uitoe habari take kama ilivyo na picha yake maana hapa imeandikwa kimafumbo watu wengi hawatoiona.
ReplyDeletemale sio zeutamu hio email ni uzushi mtupu kwakuwa km kakamatwa na interpol iweje tunamuona anadunda tu ana kazi zake yupo very busy yeye mwenyewe kashangaa accusations na alieweka habari jamii forums ishatolewa kwakuwa ni uzushi mtupu na huko ndipo ilipoanzia sio vizuri kuharibiana majina nyie watu na aliemsingizia wana beef atajuta cha mtema kuni
ReplyDeleteSIKU ZOOTE UKISIKIA HABARI, FANYA UCHUNGUZI MWENYEWE, USIWE UNASIKILIZA WATU TU, KAMA ANGEKUWA AMEKAMATWA SI ANGALAU TUNGEPATA NA PICHA YAKE KIDOGO.
ReplyDeleteNdugu Mtaalam
ReplyDeleteKama wewe kweli ni mtaalam wa Digital Forensics, niko tayari kushirkiana nawe kwa lolote lile utakalotaka.
Niandikie: strategos@africaonline.co.tz