
Habari zilizoifikia Globu ya Jamii zinasema Chuo hicho, ambacho inasemekana kimemdhamani Grace katika masomo yake, kimegomea kushiriki kwa mrembo huyo ambaye kama atashiriki ni kwa mara ya kwanza kwa mlemavu wa aina yoyote ile kushiriki katika historia ya mashindano hayo toka yaanze mwaka 1994.
Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Flora Entertaiment,Flora Lauwo, amekataa kusema lolote juu ya hilo ila redio mbao zinasema wadau wengi wa Mwanza wameshindwa kukielewa chuo hicho kwa hatua hiyo.
Wengine wamekiunga mkono chuo hicho kwa kumzuia Grace kushiriki kwenye Miss Mwanza, baadhi wakisema hana nafasi ya kushinda na wengine wakisema kwamba hata akishinda hatofika mbali.
Redio mbao zimesema kwamba kambi ya Miss Mwanza imeingia simanzi kutokana na kupigwa stop Grace kushiriki na kuna minong'ono kwamba walitishia kususa kambi endapo kama ataendelea kufanyiwa kauzibe.
Juhudi za kuupata uongozi wa hicho chuo pamoja na Grace mwenyewe kuweka mambo hadharani zinaendelea.
mithupu naomba nikusahihishe, si mara ya kwanza kwa mlemavu wa aina yeyote kushiriki mashindano ya urembo. Kumbuka Miss Kinondoni last year walikuwa na kiziwi. Hayo tu for now.
ReplyDeleteDemu yuko bomba, ana sifa za kushiriki.
ReplyDeleteMsiingize siasa kwenye mashindano, fikirini namna ya kuwafurahisha hawa wenzetu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kushindanishwa wenyewe kwa wenyewe i.e FAIRNESS. Tofauti na hapo mtakuwa hamjawatendea haki washiriki wote watakaoshiriki hapo.Tusingependa kuona upendeleo ukifanywa kwa sababu ya ulemavu au vinginevyo. Naamini wakishindanishwa watu wenye hali sawa, atapatikana mshindi tu. Jambo halihitaji mpaka Rais aseme liko wazi. Hivyo, naupongeza uongozi wa chuo kwa kuliona hilo. Kama hawa waandaji wanakuwa na kigugumizi ktk hili watakuwa WANAFIKI. Msikwepe majukumu ktk jamii na kutaka sifa za kijinga kuwa mliwashirikisha badala ya kuwashindanisha, wapeni nafasi walemavu wajitanafasi wao kwa wao.
ReplyDeleteJamani kwani binadam wote si sawa kwani kuwa alibino ni kilema kwani nae hana haki za binadam kwa kweli inatia uchungu. Je wewe unayemkataza angekuwa mwanao ungefanyaje pia kumbuka inaweza tokea kwa familia yako mwacheni nae ajisikie binadam kama wengine ukichangia na wanavyouwawa pia tena muwabague hivyo huo sio ungwana jamani kaka mithupu je unalionaje hilo mie roho imeniuma sana kweli huko bongo kuna haki za binadam kweli. Mungu akubariki sana dada Grace uingie kwa mashindano na mungu atakuongoza ushinde pia nashukuru sana kuwa na moyo wakujitolea kushiriki fani kama hiyo ubarikiwe sana dadangu mpendwa
ReplyDeleteMimi nafikiri ni jambo la busara kumuomba mrembo huyu mwenye ulemavu asishiriki. Sababu ya kwanza ninayoweza kuitoa ni stereotype(sijui kiswahili chake) ambazo watu wanazo kila mara. Akitolewa kutokana na kutofikia viwango fulani, basi wengine wanaweza kusema ni kwa sababu ya ulemavu wake.
ReplyDeletePili kisaikologia inaweza kumuadhili na asiwe na ujasili wa kutosha wa kujielezea kutokana na self esteem aliyokuwa nayo. Ni ngumu kama hauko katika mtizamo wake kuelewa kinachomsibu ndani!
Kama anaona kuwa ana confidence ya kutosha basi apiganie haki yake ya kushiriki bila kubaguliwa kutokana na hali yake ya ulemavu.
God Speed!!
huyu demu albino anaonekana yuko bomba mbaya,unywele na mguu huo utakuwa na matunzo yenye tija.kudadadadeki nitajaribu kurusha ndoana yangu.
ReplyDeleteHEKO CHUO,haya mambo ya urembo hayana mpango
ReplyDeleteMIMI NINGEPENDA SANA GRACE ASHIRIKI, NA SIONI KAMA YEYE NI MLEMAVU NA KAMA NGOZI NI ULEMAVU BASI HATA SISI NI WALEMAVU MACHONI KWA WAZUNGU ILE NI RANGI TU.
ReplyDeleteWATU ACHENI USHAMBA WAMUACHIE MTOTO WA WATU ASHIRIKI HII NDIYO NAFASI YAKE YA KUJULIKANA HUENDA AKAPATA WADHAMINI MUACHINI TU
MSIMBAGUE KWANI MACHONI KWA MWENYEZI MUNGU SISI WOTE TUKO SAWA
DADA GRACE I REAL WISH YOU ALL THE BEST AND MAY GOD BLESS YOU.
BRO MISUPU,I DIDN'T LIKE THE FACT YOU DIDN'T DISCLOSE THE SCHOOL. THERE IS NO BIG DEAL WITH THAT, KAMA TUNATAKA KUJADILI MAADA NA KUWA WAWAZI NA WAKWELI NI LAZIMA KILA SOURCE YA HABARI IWEKWE WAZI,HATA KAMA SCHOOL HAS NOTHING TO DO WITH MY CONTRIBUTION. I'M NO GONNA CONTRIBUTE ANYTHING IF WE ARE NOT OPEN AND HONEST. THIS IS OPEN, HONEST AND TRUST ERA. PLS BRO MISUPU, USITUPE ANY MORE NEWS AMBAYO UNA ENCLOSE SOME INFO.
ReplyDeleteCHALLENGE:KAMA WEWE NI KWAAJILI YA JAMII DISCLOSE THE NAME. I KNOW IS NOT A BIG DEAL BUT IS A CHALLENGE. PLS USIBANE HII MSG NA KUWA MUWAZI TOA JINA.
IT IS WHAT IT IS.
Jamani msiwaite zeruzeru vilema. Huo sio ukilema ni ukosefu wa pigment tu kwenye ngozi. Sio vilema. Kilema ni ukosefu/kupungukiwa na kiungo/viuongo.
ReplyDeletewewe jamaa watatu hapo juu una akili fupi sana, kwa nini hao walemavu washindane uzuri wao kwa wao kwani wao sio sehemu ya jamii
ReplyDeletekama wewe unawaona watu wa ajabu na unataka watengwe mimi siwaoni
wacha mawazo mgando
Mambo ya uzuri hayana mpango,kila mtu mzuri kivyakevyake.
ReplyDeleteGRACE usimtake ubaya mfadhili,wenzio wanalilia hizo nafasi!
Hivi huo udhamini (pesa) wa hicho chuo kwa nini unamyang'anya huyu bint haki yake ya kuwa huru katika kujiamulia mambo yake?
ReplyDeleteJamani hata kama ndiyo mnamdhamini na kumlipia gharama zingine, lakini ikumbukwe huyo ni binadamu, mwacheni ashiriki katika sanaa na michezo ambayo ana kipaji, msitumie mabavu kuzima kipaji chake
anasoma kozi gani na chuo gani?
ReplyDeletehuyu binti anasoma st. augustine mwanza mwaka wa kwanza ila alipohojiwa alisema kuwa anaona muda mwingi anaupoteza kwenye mazoezi, yaani wanatumia siku nzima kufanya mazoezi anakosa muda wa kujisomea, hivyo akaomba ajitoe kwa kuwa mitihani yake ni this june.
ReplyDeleteHii inanikumbusha ile stori inayouliza je albino akikuibia simu yao utamkimbiza? au utaogopa kuambiwa unataka kumchuna ngozi?
ReplyDeleteMaoni yangu ni kuwa, huyu mdada kakosea. Kama ana sponsorship ni lazima angewauliza kwanza wanaomlipia chuo kama wako radhi ajishirikishe na mambo tofauti. Kumbuka anaweza kushinda na kuhitajika kuenda Dar es salaam, je ataendelea kutumia hela ya chuo akiwa Dar? Je asitishe sponsorship kwanza?
hili si swala la self esteem wala siasa, wala kujali vilema (japo mimi siafiki kama ni vilema) ni swala la matumizi muafaka ya fedha za chuo.
Amalize mkataba wake ndio ajirushe dunia nzima.
Huyo binti wa watu aende shule akasome msimchanganye bureee,huko kwenye u-miss hana nafasi zaidi ya kutumiwa kuwanufaisha wachache.Nyie wote mnaomtetea eti ashiriki mnaona karibu.
ReplyDeleteWewe unayemponda anon wa tatu, una matatizo ya Problem, hutaki kuambiwa ukweli. Kumbuka ktk mashindano haya kuna vigezo kibao vya kuzingatiwa. Na ndio maana hata Mratibu wa mashindano haya alipohojiwa hakutaka ku-comment maana angeweza kuwakwaza watu wenye mtazamo kama wewe. UKWELI UTABAKI KUWA UKWELI DAIMA. NI MIPANGO YA MUNGU, DON'T COMPLAIN.
ReplyDeleteHivi inakuwaje mtu anaandika maherufi makubwa makubwa, kero hii!
ReplyDeleteKama maadili ya hicho chuo yanakataza kushiriki mashindano ya urembo nadhani hata kama Grace asingekuwa albino angekatazwa kushiriki na mwanafunzi yeyote wa chuo hicho haruhusiwi kushiriki...ni kama Zanzibar walivyokataa mashindano haya!! Hapa hakuna issue ya kuendelea na huu mjadala!! Kama ni sababu nyingine tuelezeni basi ...lakini nadhani ni maadili mazuri ya hicho chuo tu!!
ReplyDeletemdhamini kumkataza ni sawa,hii ni kutokana na policy/maadili ya mdhamini wake kimasomo. mfano kama anasomeshwa na BAKWATA,kanisa au msikiti jua mashindano haya yanaenda kinyume na maadili yao,pia sponsor ni mzazi/mlezi wako wa pili.
ReplyDeleteUnapoomba Ufadhili kwa mtu au taasisi, basi jua unakubali kupoteza uhuru wako kwa namna moja au nyingine.
ReplyDeleteInavyoonekana, huyu dada anasoma ktk chuo kinachoendeshwa na taasisi ya Dini na ndicho kinachomfadhili.
Kwangu mimi, maamuzi ya chuo (Kama ni kweli) ni sahihi na ni vyema huyu dada (achia mbali hali yake) aamue kuchagua moja, Kuendelea na masomo (chini ya ufadhili wa chuo) au kuingia ktk urembo.
Kwa mtizamo wangu, huyu dada aendelee na Masomo. kwani hata ktk jamii ya maalbino wapo ambao wanalilia hiyo nafasi ya kuendelezwa kimasomo. Asijiingize ktk mgogoro
Mdadisi
Mbona tayari wamesham-bagua? kwa nini yeye kavaa nyekundu tofauti na wengine woote? hii ni kuonyesha yeye hayuko sawa na wengine ama?
ReplyDelete