Ushiriki wa Grace Wabani mrembo mwenye ulemavu wa ngozi (albino) katika Miss Vodacom Mwanza kumeingia kwikwi baada ya Chuo anachosoma (jina kapuni kwa sasa) kumtaka asishiriki kwenye mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika kesho uwanja wa CCM Kirumba.
Habari zilizoifikia Globu ya Jamii zinasema Chuo hicho, ambacho inasemekana kimemdhamani Grace katika masomo yake, kimegomea kushiriki kwa mrembo huyo ambaye kama atashiriki ni kwa mara ya kwanza kwa mlemavu wa aina yoyote ile kushiriki katika historia ya mashindano hayo toka yaanze mwaka 1994.
Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Flora Entertaiment,Flora Lauwo, amekataa kusema lolote juu ya hilo ila redio mbao zinasema wadau wengi wa Mwanza wameshindwa kukielewa chuo hicho kwa hatua hiyo.
Wengine wamekiunga mkono chuo hicho kwa kumzuia Grace kushiriki kwenye Miss Mwanza, baadhi wakisema hana nafasi ya kushinda na wengine wakisema kwamba hata akishinda hatofika mbali.
Redio mbao zimesema kwamba kambi ya Miss Mwanza imeingia simanzi kutokana na kupigwa stop Grace kushiriki na kuna minong'ono kwamba walitishia kususa kambi endapo kama ataendelea kufanyiwa kauzibe.
Juhudi za kuupata uongozi wa hicho chuo pamoja na Grace mwenyewe kuweka mambo hadharani zinaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2009

    mithupu naomba nikusahihishe, si mara ya kwanza kwa mlemavu wa aina yeyote kushiriki mashindano ya urembo. Kumbuka Miss Kinondoni last year walikuwa na kiziwi. Hayo tu for now.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2009

    Demu yuko bomba, ana sifa za kushiriki.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2009

    Msiingize siasa kwenye mashindano, fikirini namna ya kuwafurahisha hawa wenzetu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kushindanishwa wenyewe kwa wenyewe i.e FAIRNESS. Tofauti na hapo mtakuwa hamjawatendea haki washiriki wote watakaoshiriki hapo.Tusingependa kuona upendeleo ukifanywa kwa sababu ya ulemavu au vinginevyo. Naamini wakishindanishwa watu wenye hali sawa, atapatikana mshindi tu. Jambo halihitaji mpaka Rais aseme liko wazi. Hivyo, naupongeza uongozi wa chuo kwa kuliona hilo. Kama hawa waandaji wanakuwa na kigugumizi ktk hili watakuwa WANAFIKI. Msikwepe majukumu ktk jamii na kutaka sifa za kijinga kuwa mliwashirikisha badala ya kuwashindanisha, wapeni nafasi walemavu wajitanafasi wao kwa wao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    Jamani kwani binadam wote si sawa kwani kuwa alibino ni kilema kwani nae hana haki za binadam kwa kweli inatia uchungu. Je wewe unayemkataza angekuwa mwanao ungefanyaje pia kumbuka inaweza tokea kwa familia yako mwacheni nae ajisikie binadam kama wengine ukichangia na wanavyouwawa pia tena muwabague hivyo huo sio ungwana jamani kaka mithupu je unalionaje hilo mie roho imeniuma sana kweli huko bongo kuna haki za binadam kweli. Mungu akubariki sana dada Grace uingie kwa mashindano na mungu atakuongoza ushinde pia nashukuru sana kuwa na moyo wakujitolea kushiriki fani kama hiyo ubarikiwe sana dadangu mpendwa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2009

    Mimi nafikiri ni jambo la busara kumuomba mrembo huyu mwenye ulemavu asishiriki. Sababu ya kwanza ninayoweza kuitoa ni stereotype(sijui kiswahili chake) ambazo watu wanazo kila mara. Akitolewa kutokana na kutofikia viwango fulani, basi wengine wanaweza kusema ni kwa sababu ya ulemavu wake.
    Pili kisaikologia inaweza kumuadhili na asiwe na ujasili wa kutosha wa kujielezea kutokana na self esteem aliyokuwa nayo. Ni ngumu kama hauko katika mtizamo wake kuelewa kinachomsibu ndani!
    Kama anaona kuwa ana confidence ya kutosha basi apiganie haki yake ya kushiriki bila kubaguliwa kutokana na hali yake ya ulemavu.

    God Speed!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    huyu demu albino anaonekana yuko bomba mbaya,unywele na mguu huo utakuwa na matunzo yenye tija.kudadadadeki nitajaribu kurusha ndoana yangu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    HEKO CHUO,haya mambo ya urembo hayana mpango

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    MIMI NINGEPENDA SANA GRACE ASHIRIKI, NA SIONI KAMA YEYE NI MLEMAVU NA KAMA NGOZI NI ULEMAVU BASI HATA SISI NI WALEMAVU MACHONI KWA WAZUNGU ILE NI RANGI TU.

    WATU ACHENI USHAMBA WAMUACHIE MTOTO WA WATU ASHIRIKI HII NDIYO NAFASI YAKE YA KUJULIKANA HUENDA AKAPATA WADHAMINI MUACHINI TU

    MSIMBAGUE KWANI MACHONI KWA MWENYEZI MUNGU SISI WOTE TUKO SAWA

    DADA GRACE I REAL WISH YOU ALL THE BEST AND MAY GOD BLESS YOU.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    BRO MISUPU,I DIDN'T LIKE THE FACT YOU DIDN'T DISCLOSE THE SCHOOL. THERE IS NO BIG DEAL WITH THAT, KAMA TUNATAKA KUJADILI MAADA NA KUWA WAWAZI NA WAKWELI NI LAZIMA KILA SOURCE YA HABARI IWEKWE WAZI,HATA KAMA SCHOOL HAS NOTHING TO DO WITH MY CONTRIBUTION. I'M NO GONNA CONTRIBUTE ANYTHING IF WE ARE NOT OPEN AND HONEST. THIS IS OPEN, HONEST AND TRUST ERA. PLS BRO MISUPU, USITUPE ANY MORE NEWS AMBAYO UNA ENCLOSE SOME INFO.

    CHALLENGE:KAMA WEWE NI KWAAJILI YA JAMII DISCLOSE THE NAME. I KNOW IS NOT A BIG DEAL BUT IS A CHALLENGE. PLS USIBANE HII MSG NA KUWA MUWAZI TOA JINA.

    IT IS WHAT IT IS.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    Jamani msiwaite zeruzeru vilema. Huo sio ukilema ni ukosefu wa pigment tu kwenye ngozi. Sio vilema. Kilema ni ukosefu/kupungukiwa na kiungo/viuongo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    wewe jamaa watatu hapo juu una akili fupi sana, kwa nini hao walemavu washindane uzuri wao kwa wao kwani wao sio sehemu ya jamii
    kama wewe unawaona watu wa ajabu na unataka watengwe mimi siwaoni
    wacha mawazo mgando

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2009

    Mambo ya uzuri hayana mpango,kila mtu mzuri kivyakevyake.
    GRACE usimtake ubaya mfadhili,wenzio wanalilia hizo nafasi!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2009

    Hivi huo udhamini (pesa) wa hicho chuo kwa nini unamyang'anya huyu bint haki yake ya kuwa huru katika kujiamulia mambo yake?
    Jamani hata kama ndiyo mnamdhamini na kumlipia gharama zingine, lakini ikumbukwe huyo ni binadamu, mwacheni ashiriki katika sanaa na michezo ambayo ana kipaji, msitumie mabavu kuzima kipaji chake

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2009

    anasoma kozi gani na chuo gani?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2009

    huyu binti anasoma st. augustine mwanza mwaka wa kwanza ila alipohojiwa alisema kuwa anaona muda mwingi anaupoteza kwenye mazoezi, yaani wanatumia siku nzima kufanya mazoezi anakosa muda wa kujisomea, hivyo akaomba ajitoe kwa kuwa mitihani yake ni this june.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2009

    Hii inanikumbusha ile stori inayouliza je albino akikuibia simu yao utamkimbiza? au utaogopa kuambiwa unataka kumchuna ngozi?

    Maoni yangu ni kuwa, huyu mdada kakosea. Kama ana sponsorship ni lazima angewauliza kwanza wanaomlipia chuo kama wako radhi ajishirikishe na mambo tofauti. Kumbuka anaweza kushinda na kuhitajika kuenda Dar es salaam, je ataendelea kutumia hela ya chuo akiwa Dar? Je asitishe sponsorship kwanza?
    hili si swala la self esteem wala siasa, wala kujali vilema (japo mimi siafiki kama ni vilema) ni swala la matumizi muafaka ya fedha za chuo.
    Amalize mkataba wake ndio ajirushe dunia nzima.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2009

    Huyo binti wa watu aende shule akasome msimchanganye bureee,huko kwenye u-miss hana nafasi zaidi ya kutumiwa kuwanufaisha wachache.Nyie wote mnaomtetea eti ashiriki mnaona karibu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2009

    Wewe unayemponda anon wa tatu, una matatizo ya Problem, hutaki kuambiwa ukweli. Kumbuka ktk mashindano haya kuna vigezo kibao vya kuzingatiwa. Na ndio maana hata Mratibu wa mashindano haya alipohojiwa hakutaka ku-comment maana angeweza kuwakwaza watu wenye mtazamo kama wewe. UKWELI UTABAKI KUWA UKWELI DAIMA. NI MIPANGO YA MUNGU, DON'T COMPLAIN.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2009

    Hivi inakuwaje mtu anaandika maherufi makubwa makubwa, kero hii!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2009

    Kama maadili ya hicho chuo yanakataza kushiriki mashindano ya urembo nadhani hata kama Grace asingekuwa albino angekatazwa kushiriki na mwanafunzi yeyote wa chuo hicho haruhusiwi kushiriki...ni kama Zanzibar walivyokataa mashindano haya!! Hapa hakuna issue ya kuendelea na huu mjadala!! Kama ni sababu nyingine tuelezeni basi ...lakini nadhani ni maadili mazuri ya hicho chuo tu!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2009

    mdhamini kumkataza ni sawa,hii ni kutokana na policy/maadili ya mdhamini wake kimasomo. mfano kama anasomeshwa na BAKWATA,kanisa au msikiti jua mashindano haya yanaenda kinyume na maadili yao,pia sponsor ni mzazi/mlezi wako wa pili.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2009

    Unapoomba Ufadhili kwa mtu au taasisi, basi jua unakubali kupoteza uhuru wako kwa namna moja au nyingine.
    Inavyoonekana, huyu dada anasoma ktk chuo kinachoendeshwa na taasisi ya Dini na ndicho kinachomfadhili.

    Kwangu mimi, maamuzi ya chuo (Kama ni kweli) ni sahihi na ni vyema huyu dada (achia mbali hali yake) aamue kuchagua moja, Kuendelea na masomo (chini ya ufadhili wa chuo) au kuingia ktk urembo.

    Kwa mtizamo wangu, huyu dada aendelee na Masomo. kwani hata ktk jamii ya maalbino wapo ambao wanalilia hiyo nafasi ya kuendelezwa kimasomo. Asijiingize ktk mgogoro

    Mdadisi

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 05, 2009

    Mbona tayari wamesham-bagua? kwa nini yeye kavaa nyekundu tofauti na wengine woote? hii ni kuonyesha yeye hayuko sawa na wengine ama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...