Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican nchini Italia yamemnyang’anya Jimbo, Askofu wa Same, Jacob Koda, baada ya kubainika kukiuka mafundisho ya imani ya kanisa hilo.

Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Joseph Chennoth alithibitisha Dar es Salaam jana kuwa Askofu Koda ametakiwa na kanisa kuacha utume huo mara moja na kupumzika ama kufanya shughuli binafsi za mafunzo.
Hata hivyo, Balozi huyo wa Papa hakufafanua zaidi kiini cha kuondolewa kwa Askofu Koda na ni mafundisho gani ya kanisa aliyokiuka, ingawa taarifa kutoka Same zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa amejiingiza katika mafundisho yaliyo kinyume cha imani ya Kikristo na ya Kanisa Katoliki.
Habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2009

    Mimi binafsi ni mkatoliki, lakini kuna maadili mengi ya kanisa la katoliki huwa sikubaliani nayo.

    Inabidi watueleze ni kitu gani kibaya askofu ametenda mpaka akanyang'anywa madaraka. Ili na sisi tuweze kutoa mawazo yetu.

    Je inakuwaje kauli ya kumsamehe aliyekosa?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2009

    Kama ni Mkatoliki ungejua ni nini maana ya "kuvuliwa madaraka", Askofu huyu alipokea misaada mingi sana ya Devil Warship akidhani kuwa itasaidia kuendeleza Jimbo lake na baadae akaanza kuudhulia vikao vyao. Kwa hali hiyo, ameenda kinyume na mafundisho ya Kanisa ukizingatia dhehebu la Devil linapingwa na Makanisa mengi hata dini zingine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2009

    Mtuambie ukweli, alikuwa kihubiri kitu gani kanisani??Kanisa linapoteza mwelekeo.Ataibuka mwingine ila huyu atanyimwa uhuru wa kuongea na kuzibwa mdomo asielezee ukweli kama ilivyokuwa kwa Sister yule wa Iringa!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2009

    Sasa wewe anony wa kwanza, sasa kama hukubaliani na maadili mengi unafanya nini kwenye kanisa hilo? Wewe basi ni mwendaazimu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2009

    Mbona wapo maaskofu wengine ambao wamo kwenye devil worship na majina yao tunayafahamu. Afadhali kanisa lianze kujishafisha. longolongo nyingi sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2009

    As of December 31st 2005, there were 557, persons having the Vatican citizenship, of which 58 Cardinals, 293 of the Clergy having status as members of the Pontifical Representations, 62 other members of the Clergy, 101 members of the Pontifical Swiss Guard and 43 other lay persons.

    The persons authorized to reside in the Vatican City maintaining their original citizenship were 246, of the aforementioned numbers.

    The persons residing in buildings outside of the Vatican City in buildings exempt from expropriation and taxation were 3,100 on the above mentioned date.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2009

    What next?? kulikuwa na Orthodox then Catholics then lutheran then walokele then "Multiple of church/denomination??? then mwisho =Tatol Collapse

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2009

    Audhubillah mina sheitan rajim
    The devil is a manifest enemy of man, he has made no secret that he will mislead man so that he may not even remember to thank his own Creator
    Aduwin mubin au manifest enemy thats what he is
    O Children of Adam...you should not worship sheitan, Verily he is a plain enemy to you..36.60
    That is clear to me and the rest is up to you
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2009

    May be he never went to the devil worship but was considering THE ISLAM.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2009

    ni nyakati za mwisho

    dini ni wewe na Yesu basi,aya mengine ni misimamo tu yao binafsi na jinsi alivoamka asubuhi

    inaboa saaaana,unaweza salia home kwako tu ukifikilia jinsi watu wanavofanya vituko ktk izo majengo
    laaa sali zako tia timu achana kufatilia life za ao watu,yani utakuwa mpagani-usiwe na imani yoyote

    kero sana

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 08, 2009

    pole mtumishi wa watu

    ndo ivo,survival of the fitest

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2009

    Kanisa imara katoliki lenye misingi na sheria zake. halitayumba kwa maneno ama uamuzi wa mtu mmoja.
    Just get out of here-Kaanze kakobe yako ama msikiti ama chochote.
    Stable church will never shake na wewe msomaji kama mkatoliki unaona gozigozi anza.
    Tuache na utaratibu wetu
    Yep-Utawala wa sheria
    Zilikuwapo toka enzi za adamu na hawa

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2009

    Mdau wa kwanza hapo juu-
    Mkatoliki usiyependa maadili ya kikatoliki ni kama mwanaume unayependa mambo ya kike. Multiple personality.
    Ukiona katoliki wana maadili mabovu anza
    Sisis tupo yadi yesu ashushe mikono kwenye sanamu ya mbele ya kanisa
    We wahi tu
    Inawezekana wewe ndio huna maadili mazuri unalisingizia kanisa katoliki ama kutoelewa kwako.
    Pia we are not sure kama hayo maadili unayoyasema yametoka kwa mungu ama kwa shetani
    Wahini tu mtuache katoliki

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2009

    For us who knows him, he did so many good things on his Jimbo, hayo mambo eti kafundisha mafundisho yaliyo nje ni unaa tu, mtu akieleza ukweli eti katoka nje ya mafundisho kwa hiyo kuficha ukweli ndio yupo ndani ya mafundisho? please they should give people break. Koda endelea na maisha yako usiwe na noma wala nini, wewe peta tu mbele kwa mbele, the life just start enjoy it, i guess you been missing a lot so now ur free, fly like a bird!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2009

    wewe anonymous 6.45am usichanganye mambo, koda ametenda mazuri na mabaya, hakuna aliyesema kuwa hama mema. sasa kama yeye aliwaambia kuwa hakosei ndo mseme hayo. kwani kabla hajawa askofu si kulikuwa na maaskofu wengine, ?? pia si kuna mapadre ambao hawajawa maaskofu?? yeye bado ni askofu., hakuumbwa kwaajili ya jimbo la same tu, atakwenda kutumikia mahali pengine, aache atakayepewa jimbo afanye kazi si kumwaga fitina.siyo anapiga kelele hoo nataka kuondoa umasikini wa watu wa upareni, nani kamwambia sisi wanafiki kiivyo???. kama si hao wakatoliki kumleta same angejua lini hilo>>???. kama kweli sisi tu katika shida kwanini anaumia sisi kupewa mwingine wa kutusaidia ???. koda ni mnafiki anajikaanga kwa mafuta yake. sijawai kuona askofu anazunguka kwenye vyombo vya habari kutafuta suluhu na mwajiri wake. kama kweli hajatendewa haki, ajue hataweza kutafuta haki kwa kuongea ovyo- koda ameingia seminary akiwa mdogo, anajua utaratibu wa wakatoliki, na anajua hata akionge a huko nje haitasaidia, njia sahihi anayo ila anakwepa kuitumia,, anaogopa nini???. basi na afunge na kuomba ili epo huyo wa fitina na chuki aliye waingia wakubwa wake na ashindwe,,, kuliko yeye kuongezea pepo wa malumbano juu yake.
    nafsi yake inajua ilichofanya
    tuhubiri upendo na si chuki.. ikumbukwe yusfeli alimwasi mungu kwakuwa alitafuta kuonekana malaika aliye bora kuliko wenzake. koda kimsingi ni padre, tena askofu, akubali mwingine kupangiwa jimbo la same. yeye kusema anataka kuendelea kubaki same kuwaendeleza wana same ni kama kung'ang'ania madaraka- asije akafananishwa na yusfeli......tena mbaya zaidi anajua yeye aina ya kiapo alikula wakati anakabidhiwa uchungaji, sisi hatujui, wala magazeti hayajui, kamwe kelele za watu hazitamsaidia koba, ni mungu peke yake ndiyo anajua hatma ya kiumbe wake jakob koda. jakob koda kuwa karibu na mungu na sio waandishi wa habari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...