Tamasha la fasihi na
maadhimisho ya mwaka mmoja wa Soma.
Soma Mkahawa wa Vitabu unawakaribisha kujumuika nasi katika tamasha la tatu la fasihi litakalofanyika sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja wa Soma kuanzia leo Ijumaa, Jumamosi hadi Jumapili.
Soma Mkahawa wa Vitabu unawakaribisha kujumuika nasi katika tamasha la tatu la fasihi litakalofanyika sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja wa Soma kuanzia leo Ijumaa, Jumamosi hadi Jumapili.
Shughuli na maonyesho mbalimbali yatafanyika ikiwa pamoja na maonyesho ya kazi mbalimbali za usomaji na uandishi wa fasihi, kazi za ubunifu, mijadala ya kirika na masuala ya kijamii, simulizi za hadithi, tambo za kishairi, maonyesho ya vipaji kwa watoto na vijana, filamu fupifupi.
Kutakuwa pia maonyesho lukuki kutoka kwa wasanii na wanafasihi maarufu kama MRISHO MPOTO, VITALIS MAEMBE, ROGERS LUCAS na wengineo wengi watajumuika pamoja na kutumbuiza pamoja na wasanii wachanga katika siku zote hizo tatu za tamasha.
Unakaribishwa kuja na tungo, mashairi na kazi zinginezo za kifasihi na kisanii ambazo ungependa kuzionyesha na/ama kuzijadili pamoja na wadau wa jamii ya usomaji, ubunifu na utamaduni.
Jumamosi tarehe 11 Julai 2009, Saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni
Jumapili tarehe 12 Julai 2009, Saa 9 jioni hadi saa 2 usiku.
“Karibu Soma ujenge maarifa,

ufurahie utamaduni
na uburudike katika mandhari murua”
ni kweli
ReplyDeletemana tulio wengi kiswahili hatujui kabisa,sasa ndo usiseme vijana wa kizazi kipya sasa ndo zero kabisaaa
yan ilimradi mtu naunganisha tu sentensi na unaelewa basi
kazi ipo adi tufike!!!