HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI KUTOKA BIHARAMULO ZIKISEMA KWAMBA CCM IMESHINDA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA BIHARAMULO MAGHARIBI, IKIWA NI ZOEZI LA KUJAZA NAFASI ILIYOACHWA WAZI JIMBONI HAPO NA MAREHEMU PHARES KABUYE ALIYEFARIKI MAPEMA MWAKA HUU.
KWA MUJIBU WA HABARI HIZO, MGOMBEA UBUNGE WA CCM KATIKA JIMBO HILO, MH. OSCAR MUKASA, AMETANGAZWA MSHINDI BAADA YA KUIBUKA NA ELFU 17, 561 (SAWA NA ASILIMIA 51) NA MGOMBEA KWA TIKETI YA CHADEMA KAPATA KURA 16, 670 (SAWA NA ASILIMIA 48.4) WAKATI MH. MPEKA BUHANGAZA WA TLP KAPATA KURA 198.
TAKRIBAN WAPIGA KURA 87,000 WALIJIANDIKISHA
NA 34,000 NDIO WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2009

    NI VIPI ALIYEPATA ASILIMIA 51.2 ASHINDWE NA APEWE ALIYEPATA ASILIMIA 48, POLENI VIONGOZI WA CHADEMA MLIOPATA AJALI YA GARI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2009

    najua wewe michuzi umefurahi sana ndio maana umeandika breaking news hizi baada ya hapa kwani awali hukuwa tayari kuziandika hata habari za matokeo ya awali yaliyokuwa yakionyesha kuwa mgombea mwingine asiye wa fisiemu alikuwa anaongoza. twali: kwa nini wamekuwa wakiongoza wangine kwa tofauti kubwa ya kura lkn baadaye mshindi anakuwa mwingine?? haya, tuendelee tu kwa kuwa bado tunaishi. alamsiki.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2009

    NIKAWAIDA YETU

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2009

    umefurahi sana bwana michuzi naona ulikuwa unasubiria kwa hamu ccm ishinde,kama kawaida yao kuiba kura

    ReplyDelete
  5. mzee wa ze fulanaz acha kuwa biased bwana....jinsi ulivyoandika tu hii post inaonyesha moja kwa moja kwamba na wewe ni wale wale...unamtaja mshindi wa kwanza humtaji wa pili unarukia kumtaja wa tatu....acha unazi mkuu wa wilaya kwa sababu hii ni blog ya jamii ati na inatembelewa na watu wa kada tofauti....mbona husemi huyo alipewa huo ushindi wa pili kapata kura ngapi!!!!!?
    sasa naomba niwape hali halisi wadau....
    MPAKA NUSU SAA KABLA HUYO MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HAJATANGAZA MATOKEO CHADEMA WALIKUWA WANAONGOZA KWA KURA 631, WAKIFUATIWA NA CCM, THEN TLP KWA MBALI.....
    hivi watanzania tunaelekea wapi na haya mambo...yani hawa wenzetu hawaoni aibu...kwani waliandikiwa kutawala milele!!!
    kaka mkuu wa wilaya naomba iweke hii post please!!!

    ReplyDelete
  6. mpenda demokarasiaJuly 06, 2009

    Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA inaelekea wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.

    Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.

    Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde

    Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:

    CHADEMA: 17,313

    CCM: 16,682

    TLP: 187

    Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)

    then mwisho wa siku!!!!


    Tume ya Uchaguzi imemtangaza mgombea wa CCM kama mshindi kwa kura zinazoonyeshwa kwenye Update ya awali ingawa CHADEMA wameyakataa matokeo ya vituo 9 kati ya vituo 237 vya uchaguzi!


    WHERE IS DEMOCRACY??????????????

    ReplyDelete
  7. haki daimaJuly 06, 2009

    Nafikiri sasa hivi kunahitajika vurugu tena vurugu hasa sio za kitoto. Wataua watu, 10, 20, 100, 1000 lakini Millioni 40 watapata haki ya kuwa na democrasia ya kweli. Nchi nyingi zenye viongozi dhalimu huwa hazitendi haki mpaka yatokee machafuko.

    Hii katiba ya nchi haifai, kuipa haki tume kuwa na kauli ya mwisho ni udikteta wa hali ya juu kwenye nchi yenye utawala wa sheria. Mahakama zilitakiwa kuwa na uwezo wa kuwithheld results zozote za uchaguzi mpaka ufumbuzi wa kisheria upatikane. Huu upuuzi wa CCM sasa hivi hauvumiliki tena. Watajifunza kutenda haki pale ambapo watakapoona maslahi yao yapo hatarini na ili kuweka maslahi yao hatarini ni vurugu tu na kuwafanya wasifurahie utawala. Si unaona Zanzibar baada ya kupelekeshwa na CUF wakajifanya muafaka na baada ya kuona CUF wametuliza steam, wakabadilisha kibao.

    Kwa nini wanakumbatia utamaduni ambao hawauwezi?, kwa nini tusiseme kuwa nchi yetu ni ya chama kimoja tu?. Haya mazingaombwe tunamfanyia nani? kama si kuendeleza chuki miongoni mwetu?. CCM hivi kiti Biharamuro kitawasaidia nini ninyi? zaidi ya kutugawa watanzania kiitikadi?. Mimi mzee wangu ni CCM pure na mimi sina chama ila kwa style hii inanifanya nianze kumchukia mzee bila sababu.

    Hivi CCM mnaijua gharama ya umoja wetu?, mnaijua gharama ya uishirikiano wetu?. naomba basi mfute mfumo wa vyama vingi ili kusiwe na chuki miongoni mwetu ambazo ninyi ni mbegu bora yenye afya ya chuki hizo.

    ReplyDelete
  8. mzanzibarJuly 06, 2009

    nimeenda kulala najua chadema wameshinda, nimeamka nikasema ngoja niangalie kuna nini kipya sherehe za hushindi n.k, mara naona kicha cha habari kingine kulikoni...

    nilivyoona jimbo la biharamulo magharibi nikazania jana kulikuwa na chaguzi mbili moja ya biharamulo na nyigine ya biharamulo magharibi kwa hiyo chadema wameshinda biharamulo na ccm biharamulo magharibi kumbe ni hilo jimbo moja, I am shocked

    kila nchi imemwaga damu ili kupata demokrasia na Tanganyika sio tofauti, ZNZ wameshamwaga damu tiyari angalau kura za pemba haziibiwi
    Tanganyika wakati wa kuamka ndio sasa, lakini kinachonishangaza kuna watu wengi ambao ni fukara na washabiki wa kubwa wa ccm je hawajiulizi ccm imewafanyia nini

    upinzani usikubali kuingia bungeni, ugomee kuingia bungeni...
    wabunge wa ccm hawawezi kukaa peke yao

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2009

    Jamani Rahaahhhhhhhh rahaaaaaaaaaaaaaaaaa. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE OYEEEEEEEEEEEEEEE CHAMA CHETU CHA MAPINDUZI CHA JENGA NCHI..... HONGERA NYINGI KWA MSHINDI NA CCM PAMOJA.

    ReplyDelete
  10. AAAH HAPO HAKUNA KITU ZAIDI YA DHURMA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2009

    MASIKINI JAMANI NA JUHUDI ZOTE ZA KULETA VIJANA TOKA TARIME. MMMH

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2009

    sasa ile chama ingine ijuu kuwa enyewe inayulikana saidi kule kanda ya kasikasini na tarime tu

    ReplyDelete
  13. UJUE CCM WANATUMIA PESA KUHONGA MAWAKALA ILIWAFANIKIWE KATIKA UCHAGUZI HUU. NA WAMEFANIKIWA WALICHO KITAKA ! YAANI INGETENDEKA HAKI BIN SAWIA YAANI CCM ANGESHIKILIA MKIA KATIKA UCHAGUZI HUU MDOGO WA WABUNGE!!!!!!!!!!!!1

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2009

    Wataendelea kushinda tu sio siri lakini swali ni je `NI KWELI WANAKUBALIKA KIHIVYO AU NI WASIWASI WA WANANCHI KWA HAYOWANAYOWATISHIA NAYO?
    Tumetembelea vijijini, wazee wetu wanaishia kutuulizia `hivi kweli ni hivyo tunavyoambiwa kuwa vyama vya upinzani vikichaguliwa kutakuwa na vurugu?'
    Demokrasia ya kweli Tanzania ni bado kabisa, nafikiri ni kweli walivyosema kuwa asilimia kubwa ya Watanzania hawajaelimika kuhusu swala zima la vyama vingi. Na sijui wakulaumiwa hapani nani?
    M3

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2009

    Ninakubaliana na mdau aliyempa ukweli ndugu Michuzi. hii ni blogu ya jamii na wewe kama mratibu wa blogu jaribu kufunikafunika hisia zako za kikereketwa na wafurukutwa wapeane vidonge bila ya kufikiria wanakupa wewe!!!

    NI MASIKITIKO MAKUBWA SANA kuwa jimbo hili "limokombolewa" na sisiemu. Hii ni 'mock' ya 2010 na matumaini ya kupanua kambi ya upinzani ndio yanazidi kuyoyoma, na hivyo tunapiga hatua nyingine moja kurejea karne ya 20!! Jamani tufanye nini kuikomboa nchi yetu????

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 06, 2009

    acheni hizo mkishindwa mnadai kura zimeibiwa! ukweli ni kwamba hamna mikakati inayoeleweka na watanzania,mnaifikiria ikulu tu,CCM oyeeee

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 06, 2009

    Kwa utaratibu wa uchaguzi ulivyo na muundo wa tume ya uchaguzi ni ndoto CCM kushindwa labda watake wenyewe au waogope kwa sehemu ambazo wananchi wake hawana uoga. Kwa kuwa ni CCM yenyewe inayosimamia na kutangaza inayotaka yatangazwe kwa kutumia wasimamizi ambao kinadharia ni huru na kiutendaji ni CCM.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 06, 2009

    Tunajifunza kwa watani wa jadi.Eti kutangulia si kufika

    ReplyDelete
  19. Mbona kura za Chadema umeshindwa kuziandika hapo bwana Michuzi? mpaka tuanze kutafuta calculator!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 06, 2009

    Longolongo ziachwe,kama kweli wapinzani wanataka kuongeza viti bungeni vya ubunge,kwa nini wasikubaliane waungane?Hizi siasa nazo sometimes ni kudanganyana tu,watu wana uchu wa madaraka.Hakuna upinzani wa kweli TZ bado.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 06, 2009

    Kuna mtu amesema "kama kweli wapinzani wanataka kuongeza viti bungeni..., kwa nini wasikubaliane waungane". unaweza kuamaini kuwa sheria haiwaruhusu hata kuunganisha vyama vyao?!!

    ReplyDelete
  22. The moon moves slowly, but it crosses the town.July 06, 2009

    Wewe Michuzi una matatizo makubwa na wanaokushabikia...ni bora UJIVUE NGOZI YA UNAFIKI ULIYONAYO.....tangu mwanzo ulipojua CHADEMA wameshinda ulikaa kimya ukisubiria mkakati wa KUIBA MATOKEO ufanikishwe maana i believe you knew this....baada ya hapo ndio unapost thread yako...NOTHING BREAKING....breaking is that THE RESULTS HAVE BEEN ALTERED....pia wewe anonynm wa mwisho kuchangia....WEWE NI FISADI...badala ya kushangaa ..unakuja na hoja ya kuungana...UNATAKA CCM waungane na nani? Kwani wao sio wapinzani....UPINZANI hujui maana yake?

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 07, 2009

    KADA MICHUZI UNA HAKI YA KUSHEREHEKEA.....

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 07, 2009

    Wanajiamini wameshika jeshi, wana dola na wana kila kitu . Hata viwanja vya mpira tulivyojenga kwa nguvu zetu wananchi wamevinyang'anya na kuvifanya vyao, ole wao maana ipo siku wanapotaka tufike tutafika, nasikitika maana pengine itakua ni zaidi ya yaliyotokea Rwanda. Tumeona IRAN kinachotokea sasa ipo siku na si mbali sana. Eee Mola ingilia kati Taifa lako hili ambalo Hayati Muasisi alilikabidhi kwako na kulitungia wimbo wa Taifa ambao kila uimbwapo jina lako linatukuzwa lakini kikatokea Chama kimoja kwa makusudi kabisa kimeamua kudhulumu haki ya Watoto wako na kuwakabithi wachache wenye itikadi na zao na fedha za kuwadhamini wao. Tuokoe kabla watoto wako hawa hawajafikia ukomo wa uvumilivu wao pindi waonapo haki zao zinaporwa waziwazi.
    Tazama North Mara watoto wako wanaangamia serikali yako inashikwa na kigugumizi kusema wakati hali halisi ipo wazi.
    Tazama watoto wako leo hii wanafariki bila kupewa haki zao kutoka kwa mashirika waliyoyatumikia zaidi ya robo tatu ya maisha yao hapa duniani,leo hii wamekabidhiwa eti "wawekezaji"
    Tazama,Tazama, wanaohoji maslahi ya nchi na wananchi wa Taifa hili lako ambalo muasisi alilikabidhi kwako siku lilipopata UHURU, wanatishiwa kila kona ili wazibe midomo yao, je kwa faida ya nani?
    Ingilia kati wewe uliye muweza wa yote, amua juu yetu kama ulivyoingilia kati kesi ya yule aliyeuwawa kwa risasi akiwa kwenye DCM pale njia panda ya kawe, na kutoa hukumu iliyomfikia akiwa katikati ya lindi la starehe. Tunajua unaweza, na tunaamini utasikia kilio chetu ili nasi tunaokuamini tusije tukaishiwa nguvu na imani tukaangukia kwenye mitego yao
    .....amen....

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 07, 2009

    Waliojiandiakisha ni 87000. Waliopiga kula ni 34000. Wasiopiga kula ni 53000. Wasiopiga kula ni Asilimia 60 (60%). Tanzania kuna TUME HURU YA UCHAGUZI?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 07, 2009

    wewe msemaji wa mwisho jifunze kuandika kiswahili fasaha "kula" ndio nini wakati watu wanaongelea "kura" unatia aibu kutoijua lugha ya taifa, hao fisiemu hawajashinda bwana ila ni umugabenisation umepita. kama kawaida yao wanachukua wanaweka mambo yanakua waaa, ila siku moja ushindi wa kizushi utawatokea puani umma wa watanzania wakiamua.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 07, 2009

    Vitabu vya dini vinaelezea jinsi siku za mwisho kutakavyokuwa na dhuluma ndani ya mioyo ya watu, hii ndo mifano.
    Dunia haina faraja ila kwa hakika pepo si ya Wadhulumati. Kila ajiingizaye kwenye DHULUMA, kiama ni kuchungu kwake kama MUUAJI!

    Gloria BUHIYE

    ReplyDelete
  28. Dont hate crocodile before crossing the river!July 07, 2009

    Mtoa maoni wa mwisho saa 12:44:00 nadhani wewe ndio hujui ulipo...anonym inayemshambulia kwa kutojua lugha ya taifa ni ulimbukeni...the discussion here is not kura....ni kula...maana CCM hawajua kura maana wangeziheshimu..wanachotafuta wao maybe including you.....angalia matumbo ya CCM yalivyo nje nje,.....ni shauri ya kula sio kura!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 07, 2009

    mie sina chama chochote ila tunataka kujua vyama vyote apo!!

    Bwana Mungu uturehemu...

    sijui ccm inataka kupeleka watu wapi..ao viongozi

    lazima siku yawafike tena nyie tu na familia zenu sio roho zisizo na hatia

    afu unabandika matokeo ya chama fisadi wee balozi,kwani vyama vingine havikuwepo??ovyooo hii blogu sio ya chama fulani

    nyambaf

    bana hii sasa

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 08, 2009

    CCM aijashinda popote katika chaguzi zote tatu zilizopita, ni wizi mtupu!!. Busanda walipotakiwa kurudia kuhesabu kura ccm walikataa pamoja na tume yake. lakini biharamulo baada ya kuona kuwa wameshindwa wakalazimisha kurudiwa kuhesabu kura na hapo ndipo wakapata nafasi ya kutumbukiza kura zao bandia.
    Nyie endeleeni kuiba lakini mwisho wenu ukalibu sana.nyinyi mnaoshabikia wizi pamoja na bwana michuzi, ipo siku mtabaki midomo wazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...