Jeneza kama hili ndilo litakalotumika
kwenye mazishi ya Michael Jackson
Mwanamuziki Michael Jackson ambaye alifariki juni 25 mwaka huu baada ya kukumbwa na shambulio la moyo atazikwa kwenye jeneza lenye thamani ya dola 25,000 kama lile alilozikwa nalo gwiji wa muziki wa Soul, James Brown.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Michael Jackson atazikwa kwenye makaburi ya Forest Lawn Memorial Park jijini Los Angeles akiwa kwenye jeneza lenye thamani ya dola 25,000 ( takribani Tsh. Milioni milioni 32.5).

Jeneza hilo linalojulikana kama "Promethean" lina kuta za nje za dhahabu ya karat 14 na kwa ndani lina foronya za aina yake za thamani za rangi ya bluu.
Jeneza kama hilo ndilo ambalo alizikwa nalo nguli wa muziki wa Soul, James Brown "The Godfather of Soul" aliyefariki siku ya krismasi mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 73.

Michael Jackson alihudhuria mazishi ya James Brown na inasemekana alitembelea kampuni iliyotengeneza jeneza hilo na kujionea majeneza ya aina mbali mbali.

Ili kuhakikisha vibaka hawaibi jeneza au mwili wa Michael Jackson baada ya kuzikwa, kaburi la Michael Jackson litafunikwa kwa zege.

Wakati huo huo takribani watu nusu bilioni wamejisajili kwenye bahati nasibu ya kuhudhuria sherehe za kuuaga mwili wa Michael Jackson zitakazofanyika kwenye ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles siku ya jumanne asubuhi kwa saa za Marekani( Kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Tanzania).

Mpaka wakati wanafunga utaratibu wa kujiandikisha ni takribani watu Milioni 1.6 waliojiandikisha kwa ajili ya tiketi hizo.
Yasemekana watu nusu bilioni watafuatilia kwenye luninga na internet. Na tiketi hizo zitatolewa kwa watu hao 8,750 kwa kuwa kila jina litapata tiketi mbili. Kwa hiyo jumla ya tiketi 17,500 zitatolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. jamani ndugu zangu michel jackson si muislamu? sijui kama kuna sheria ya kuzikwa na jeneza katika dini hii lakini all in all keshakufa tu kama hukumu iko palepale hata ukizikwa vipi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2009

    Ukisikia ufisadi wa mazishi ndio huo. Haingii akilini kuwa wakati watoto na familia nyingi zinaishi katika lindi la umaskini ufujaji wa pesa kwa kiwango hicho unapewa umuhimu. Hapo Marekani kwenyewe wapo walala hoi kibao- haina maana kutumia gharama kubwa namna hiyo kwa mazishi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2009

    katika mtu ambaye namuheshimu ambaye alifariki na kuzikwa na sanduku la kawaida kabisa ni pope john paul hii tabia ya kuzikwa kifahari na utumiaji wa pesa nyingi wakati aliyefariki ameacha watoto kwanini hizo pesa wazitumie kwa watoto wa MJ.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2009

    jeneza cheap walitakiwa wazike carats cazaa za almus, atleast 1Milion jeneza ingekuwa poa huyo ni king 25,000 ni uzushi kabisa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2009

    Kaka wa Wacko jacko ndio muislamu.
    Lakini Maiko alikuwa mkristo wa mashahidi wa yehova.
    Alipoanza kupungukiwa ngawila ndio alitaka asilimu ili apewe sapoti toka kwa mtoto wa Mfalme..hii ni kutoka taarifa za redio mbao:
    http://news.yahoo.com/s/eonline/20090702/en_top_eo/132450

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2009

    Si kila mtu anaivalue saaana hiyo 25000$ kama wewe kaka.Usitake kushare umasikini na watu wengine...huo ni wako tafuta njia za kujikwamua kaka.
    Mbije,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2009

    Kama alikuwa dini gani hiyokwasasa haijalishi kwani anaenda kukutana na Mwenyezi. Tunachotakiwa sisi bila kujali hilo kumuombea Mungu amsamehe makosa yake. Na hata kama atazikwa na dhahabu hizo ni starehe za kujifurahisha nafsi zetu tu.
    M3

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 06, 2009

    Hizo pesa zinakwenda kwa muuza jeneza ambaye atazitumia kupata huduma nyingine kama vile kununua mahitaji ya nyumbani au kulipa karo ya mtoto, nk hatimaye hapo katikakati kuna watu lukuku (maskini na matajiri) watanufaika na ununuzi wa bidhaa hiyo. huo ndio mzunguko wa pesa za mfumo wa kibepari, na kwa hiyo ni sehemu ya mpango wa Baraka obama wa stimulus package!!!! matajiri wasipo-spend uchumi unaganda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2009

    MICHAEL JACKSON ALIKUWA MUISLAMU. SIELEWI HILO JENEZA NI KWA MALENGO GANI. HALAFU KWANINI WAMECHELEWA KUMZIKA KINYUME NA TARATIBU ZA KIISLAMU?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2009

    WAOSHA VINYWA BWANA
    MWACHENI BWANA HATA AKIZIKWA NA LA POUND M10 NI YEYE TU HELA NI ZAKE KUKU NYIE
    JAMAA KASOTA SANA
    HA,AF SIO MUISLAM HIO KIISLAM NI DINI YA WAJITOA MUHANGA NA WAPENDA VITA TU NA MAMBO YA SIASA NA CUF NA USHIRIKINA MAANA DINI HIO KACHAA
    MICHAEL NI MKRISTO PYUAA
    NA MTAZIKWA NA SANDA TU

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2009

    MICHAEL JACKSON HAKUWA MUISLAMU ACHENI UZISHI WA KIDINI. KAKA YAKE NDO ALIINGIA UISLAMU KWA KUSHAWISHIWA NA RAFIKI YAKE MTOTO WA MFALAME WA BAHARAIN NA AKAPEWA MKEWA WA KIARABU, ALIINGIA MUDA SANA WAKATI HALI YAKE YA KIPESA ILIPOKUWA MBAYA NA ALIENDA KUISHI HUKO UARABUNI KWA HII FAMILIA YA KIFLUME, NA HUYU MTOTO WA MFALUME ALIKUWA MPENZI SANA WA JACSON 5 WALIPOKUWA NA MOTOWN RECORDS, NA HATA WALIPOHAMA NA KUJIITA THE JACKSONS. SO MIKE IS NOT AN ISLAM!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2009

    Go Michael! Go Michael! Go Michael! Go Michael! You deserve the Coffin! You worked hard in your lifetime ! Hata kama lingekuwa millioni moja I support and salute you 100%
    RIP Michael

    ReplyDelete
  13. Duh!! Jamani hebu tuheshimuni dini za watu. Awe ama asiwe muislamu wao wanajua kwanini wanafanya nini na ili kiwe nini. Na haijalishi kama atazikwa hivi ama vile, maana kama ni maisha yanayoweza kumpeleka kwema ama kubaya hayaji baada ya kufa na hayawezi kuamuliwa na mwanadamu kwa namna mtu alivyozikwa.
    Lazima pia kutambua kuwa hizi dini haziko standardized na mazingira yanaathiri hata namna ya kuabudu.
    Kwa hiyo kuweka mjadala wa dini kwa mtu aliyekufa sidhani kama ni jambo la busara na zaidi kuikashifu dini ya watu (hata kama mkashifuji hana dini kama wengi wetu)si jambo la busara.
    Ni vema kuheshimu ili kuheshimika.
    Blessings

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2009

    unaposema watu nusu bilioni una maana iuna hesabu wa le watahudhuria mazishi kwa njia ya television? Nusu bilioni ni watu milioni mia tano. Nadhani umekosea. Mchungaji mtikilia atakuambia ameshakuwa mzoga hata ukitumia shilini ngapi kwa marehemu bado atafukiwa tu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2009

    MICHAEL JACKSON NI MUISLAM, ALISLIM MWAKA JANA NOVEMBER,SIONI SABABU KWANINI ANAZIKWA NA JENEZA? WAKATI SHERIA YA DINI YA KIISLAM HAIRUHUSU. ALISLIM KWAJINA LA MIKAEEL. HABARI NDO HIYYO MKUBALI MKATAE MJ NI MUISLAM.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 07, 2009

    HE deserves it. HE IS THE KING, I LOVE MIKAELI SAY WAT U WANNA SAY MAIKO IS THE BEST....ALLL TIME BEST BEST BEST.......R.I.P MJ.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 07, 2009

    MIMI BADO SIJAAMINI KAMA KWELI MICHAEL JACKSON HATUNAYE HAPA DUNIANI, SISI BANADAMU TULIMPENDA SANA MICHAEL ILA MWEYEZI MUNGU KAMPENDA ZAIDI YETU TUTAKUKUTA MICHAEL KAWBURUDISHE NA WALIOTANGULIA

    TAYARI TUMESHAKUKUMBUKA VIBAYA MNO MICHAEL

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 07, 2009

    Kwakweli sijui inamaanisha nini kuforce na kumsemea marehemu kuwa ni dini hii ama ile hadi mwingine anaandika "mkubali mkatae..." Jamani dini pekee si zitakazo tupeleka mbinguni.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 07, 2009

    MIE NI MWISLAMU NINAYEPENDA KITIMOTO KWA SANA. NAOMBENI NIKIFA MNIZIKE NA JENEZA PLEASE. HABARI HII YA KUZIKWA NA SANDA SII-MIND

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 07, 2009

    JAMANI EE! MWACHENI MTU APEWE HESHIMA YAKE YA MWISHO...KWANZA NI HELA ZAKE...WEWE UNAONA $25,000 NI NYIIIINGI SANA LAKINI KWA WENGINE SIVYO!! SASA WEWE UNAPATA SHIDA GANI MTU NA PESA YAKE AKIZIKWA KWENYE JENEZA LA $25,000???!!! KAMA UMESOMA HABARI ZA MICHAEL JACKSON, BAADA YA KUTOA MADENI YOTE ANABAKIWA NA NET ASSETS YA $236M SASA SHIDA IKO WAPI? PESA YA KUTUNZA WATOTO IPO IMEBAKI NYINGI TU... NA ZINGINE BADO ZINAINGIA KWA WINGI KUPITIA MAUZO YA ALBUM ZAKE...ACHA WIVU

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 07, 2009

    mbinguni hakuingiliki na DINI yoyote!!wala jeneza wala mkeka,wala mipesa,wala ushabiki wa watu,wala supestaa,wala wapenzi,wala kutoa charity mabilioni nk

    mbinguni ni uhusiano wako na muumba je ulikuwaje ulipokua duniani,uliishi maisha ya kumpendeza muumba vile alivoagiza??kufeni muone

    kaaazi kweli

    na habari ndo iyo

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 07, 2009

    STOP all these NONSENSE!...ooh jeneza lake limecost 25000 dollars..so WHAT???....try to RESPECT his family WISHES...,may be to them he is that EXPENSIVE! besides,even if akizikwa kwenye mifuko ya rambo hio pesa ndio itamaliza TATIZO la watoto wote ulimwenguni wanaoishi under poverty??NO!!!..stop all this politiko korektiness eboh...kwanza MICHAEL in his LIFE,he gave to CHILDREN ,his house was children centre and now in his death you people you have guts to demand the money used to buy his coffin...?????kuweni na AIBU ala!
    mmeweka vizuri saaaana,even if he is burried in $25000 coffin,it doesnt erase the fact he is DEAD! na mie nawaambie even if akizikwa kny GUNIA it doeesnt erase the fact,he is DEAD either!!!!....let his family burry him the way they want....!!you shameless idiots..you can back OFF!


    i saw one of his quotation..and i felt SAD!....it says; if you enter this world knowing you are LOVED and you LEAVE this world knowing the SAME,then anything that hapened in between can be dealt with....!!!i dont know if there are people outhere who feel like me,that his final days were just SAD and LONELY!,,MICHAEL being severly malnourished/one meal a day and on 'painkillers'...you wonder..if he felt 'LOVED'... when he was going...???

    his financial worries..and the-then-busy-upcoming-tour...i only felt he couldnt take anymore!!... 'A MAN SHOULD BE FAITHFUL,AND WALK WHEN NOT ABLE!..but am only HUMAN...he said in one of his songs, REST IN PEACE MICHAEL!!!!!

    WE LOVE YOU!!..may be we didnt get a chance to say this when you are alive,,,but i know you are watching us.....yes,WE LOVE YOU MICHAEL!!!!!...we are only comforted,that you are in a better place...!!!!!!!((YES IS LIKE AM SEEING YOU NOW...IN A VERY BETTER PLACE!!!)

    fan-birmingham.
    BHAM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...