JK akizungumza na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka kwenda Lusaka Zambia kwa ziara siku tatu ya kiserikali asubuhi hii, ambapo leo anatarajiwa kufunguwa maonesho ya kimataifa ya Biashara katika mji wa Ndola Lusaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2009

    MICHUZI BRO, HATA KAMA HUTATAKA, KAMA NI BABA MTEMBEZI, TANZANIA TUNAYE. AMEKUWA KAMA WAGANGA WAKUU WA WILAYA[DMOs] WALIOPACHIKWA JINA LA DAILY MISSING OFFICER. NDO RAIS WETU, HACHOKI NA MIDEGE HIYO. KAMA MNAAMINI UCHAWI HAKUNA HAYA!!!!! KUNA VIPAPAI VYA KUKIMBIA NYUMBA HAPA SIO BURE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2009

    Acha ujinga wewe Anon wa Jul.5 01:17pm. Lazima utofautishe majukumu ya rais na yako wewe baba au mama mwenye nyumba. Usiongee vitu hewa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2009

    Mdau wa 2:17, mwenzako huo ndo mtizamo wake ambao na mimi nauunga mkono.Mbona JKN original alikuwa sio mtembezi hivi..hapa kuna kitu kama sio kipapai hadi nyumbani unakuwa hutaki kukaa..
    Cha chandu- UK

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2009

    Rais wa nchi kusafiri safiri ni hatari pia,risk ni nyingi,ndege ni hatari hata kama mpya, nchi za wenzetu raisi kusafiri ni big ishu,mara chache sana na ni kama muhimu,sisi maskini ndio kila siku,kwa pesa ipi?safari yenyewe kwenda ndola hapo zambia kufungua sabasaba yao,si angemtuma hata mkuu wa wilaya ya tunduma avuke boda hapo kwenda kufungua.?!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2009

    Jamani hii tabia ya Rais akisafiri basi serikali nzima imsindikize airport na akirudi serikali yake yote isimame airport inamsubiri hamoni imepitwa na wakati waheshimiwa ? Si atafute muda mwingine wa kukabidhi nchi kwa hiyo cabinet yake sio en route to the airport ? coz hii ni kupoteza muda wetu kwa safari za airport ambapo mngekuwa mnafanya jambo lingine la maendeleo na hivi anasafiri kila kukicha am sure hata wasindikizaji wameshachoka sema tuu ndio hizo protocol hawana jinsi. HEBU tuliangalie hili ki undani jamani ...... !

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2009

    duh!! naona hizi safari sasa zimekuwa kichekesho. hata wenyewe wakubwa wameliona hilo. angalia wanavyovunjika mbavu hapo !!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 05, 2009

    nami nakuunga mkono,wanatuwekea foleni tu barabarani.

    Manake JK,wakati anaamka kitandani wanakuwa wameshafunga barabara,sasa fikiria,kama Primier,na Makamu wa rais,na wote wanakaa sehemu tofauti tofauti...kwa namna hiyo wanatuchewelesha sisi wengine kazini.
    Ukiangalia hapa America,rais akisafiri,makamu wa rais anafichwa,haonekani kabisa,na hawasafiri mara kwa mara.
    Sasa kwa nini Kikwete asiwe na maenvoy,ambao watakuwa na kazi hizo za kumwakilisha yeye.Kwani mabalozi wetu wanafanya nini.
    Saa moja ya Dreamline,ndege hiyo ya rais kuwa hewani inatumia dola 7000.Na hapo hujawalipa marubani na wafanyakazi wa ndani,walinzi wa rais...safari ni hasara tupu,ingawa safari ya rais wa america huwa huku hatuidisckcuss lakini inasemekana,kila kitu inatumia kwenye dola1000000 ukiweka walinzi hotel,kama rais ataishi hotelini na usafirishaji wa magari yao.
    Mdau kutoka Boeing.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2009

    Utwana si kitu chema. Mabwana wanacheka watwana wamenuna!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2009

    MIMI MSAFIRI BADO NIKO NJIANI......SIJUI LINI NITAFIKAAA EEHHHH.......

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2009

    Nimelipenda sana hilo pozi la Dr, maana inaonyesha ni jinsi gani anavyoheshimu mkubwa wake.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 05, 2009

    Mie hata sitii neno maana kaka tupi ananibania sana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2009

    Duh! kweli hata mimi nashangaa kwa hela gani tulioyonayo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2009

    Maonyesho yetu ya Sabasaba raisi gani anakuja kutufungulia

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2009

    Wewe anon wa pili kuanzia mwanzo nafikiri akili yako haina akili....So you think Kikwete kila siku mguu nje ni poa tu...You need to re-think before you open big mouth....
    Haiwezikani rahisi kila siku yuko nje, basi urahisi ampe mwingine akae nje moja kwa moja. Kwahiyo muhimu ni nje au ndani??

    Mdau

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2009

    urahisi ni kiingereza au kiswahili?

    ReplyDelete
  16. Hamisi, Galloway, OHIOJuly 06, 2009

    Jamani, Mwalimu Nyerere alikuwa hasafiri kila mara kwa sababu alikuwa hajui namna ya kuiendeleza nchi yake mbali na kusisitiza Azimio la Arusha na akisafiri nje ya nchi ujue ni UNO au OAU. Ndiyo maana hata ukiwa na redio zaidi ya bendi 3 lazima upate kibali kutoka Ikulu au kwa Mthuya.
    Siku hizi ma-deal ya mikopo, misaada na takrima ni mingi hivyo lazima ujue namna ya kuifuatilia, na ukichelewa wenzio wanaichukua.
    Mwacheni huyu jamaa afuatilie mwenyewe la sivyo tutarudi kulekule tulikotoka.

    ReplyDelete
  17. NIFIKISHIE SALAMU KWA WAKWE MZEE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...