Na Mwandishi Maalumu
KANISA Katoliki limeishukuru Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushirikiano ambao Serikali hiyo imekuwa inatoa katika kuendeleza shughuli za huduma na miradi ya Kanisa hilo.
Kanisa hilo pia limesema kuwa halina tatizo lolote na Serikali na limeisifia uhusiano mzuri ulioko kati ya Kanisa hilo na Serikali, likisisitiza kuwa litaendelea kushirikiana na uongozi wa Rais Kikwete katika kutoa huduma mbalimbali kwa Watanzania.
Shukurani hizo zilitolewa Ikulu, Dar es Salaam, jana, Alhamisi, Julai 23, 2009, na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea, Askofu Nobert Mtega wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete.
Askofu Mkuu Mtega alikuwa sehemu ya ujumbe wa Shule ya Chekechea ya Mtakatifu Scholastica iliyoko Ukonga, Dar es Salaam, na uongozi wa Shirika la Watawa la Benedictine la Masista wa Mt. Agnes Chipole wa Songea, ambao ulikutana kwa mazungumzo na chakula cha mchana na Rais Kikwete kumshukuru kwa mchango wake katika kuendeleza shule hiyo.
Pamoja na kwamba iko Ukonga, shule hiyo ya Mt. Scholastica inaendeshwa na Shirika la Watawa la Benedictine la Masista wa Mt. Agnes Chipole lililoko chini ya Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea ambalo kiongozi wake ni Askofu Mkuu Mtega.
Ujumbe huo wa shule hiyo ulimshukuru Rais Kikwete kwa mambo mawili makubwa ambayo kiongozi huyo ameifanyia shule hiyo ambayo pia ni mlezi wake.
Rais Kikwete aliahidi mwaka 2002 na tayari amefanikisha kuipatia shule hiyo viti 100, na eneo la ujenzi wa ujenzi wa shule za msingi na sekondari na zahanati la ekari 16 (sawa na hekta sita).
Eneo hilo ambalo awali lilikuwa mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), pia litatumika kujenga nyumba ya watawa wa shirika hilo, iliyobomolewa katika eneo la Ukonga kupisha ujenzi wa bomba la mafuta la TAZAMA.
“Mheshimiwa Rais, mimi nimekuja mwenyewe. Baada ya kusikia Mama Mkuu wa Watawa wa Mt. Agnes Chipole wanataka kuja kukuona na kukushukuru na mimi nikaona nije kwa nia ya kukushukuru, kwa niaba ya Kanisa katika Jimbo la Songea na pia kwa niaba ya Kanisa katika Jimbo la Ukonga, ambako pia tunaendesha shughuli zetu,” alisema Askofu Mkuu Mtega.
Alisisitiza Askofu Mkuu Mtega: “Aidha, napenda kushukuru na kupongeza ushirikiano mzuri kati wa wananchi wa Ukonga na shule yetu ile ya chekechea na pia kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Mbunge wa Ukonga, Mhe. Makongoro Mahanga.” Mbunge huyo aliandamana na ujumbe huo kwa ajili ya mkutano huo na Rais Kikwete.
Wakati wa mkutano huo, Rais Kikwete pia alionyeshwa michoro ya ujenzi wa shule za msingi, sekondari, zahanati na nyumba za masista katika eneo hilo la ekari 16. Ujenzi huo uliopangwa kuanza mwakani, umekadiriwa kugharimu shilingi bilioni nne utakapokamilika.
Naye Rais Kikwete alimweleza Askofu Mkuu Mtenga na ujumbe wake kuwa alikuwa amefurahi kusikia kuwa Jeshi la Wananchi lilikuwa limekubali kutoa eneo hilo na kuwa tayari hati miliki ya kiwanja hicho, Ploti Nambari 351, imetolewa kwa Watawa wa Benedictine wa Mt. Agnes Chipole.
“Nawashukuru sana kwa kuja. Sote tulishukuru Jeshi kwa kusaidia kupata eneo hili. Nafurahi pia kusikia kuwa mmefikia hatua hii, mipango yenu ni mikubwa kweli kweli…mimi kama mlezi tutaendelea kusaidiana kwa chochote…mipango yenu mikubwa lakini hakuna kubwa lisilowezekana.”
sasa ngojeni wachonga midomo
ReplyDeletehongereni sana asa kwa kutaka kuanza toa elimu ya uraia na siasa kwa wanainchi ambao wengi hatuna elimu iyo kwa uwazi zaidi
angalizo:kazi mnayoifanya kanisa katoliki kweli ni ya baraka sana kwa raia,mnatoa huduma bora sana kuanzia mashule,vyuo,hospital nk
Kwa mara nyingine namuona Askofu aliye nipa kipaimara wakati akiwa Askofu wa jimbo la IRINGA mwaka 1992 nikiwa darasa la tano! Mungu akubariki sana Muhashamu Baba Askofu na awape nguvu katika kuwajenga Watanzania kielemu bila kujali dini wala kabila!Tuna ushahidi kuwa shule kama St. francis ya kule Mbeya, Marian girls ya Pwani na hata Loyola Dar ni za kikatoliki lakini zinazomesha umma wa watoto wa kike wa kitanzania bila kujali dini zao! Nani ambaye analipinga hili?
ReplyDeleteHuyo askofu anaitwa Norbert Mtega na sio Mtenga
ReplyDeletenisingependelea kuona vyombo vya dini vikijiingiza kwenye mambo ya siasa.SIO DALILI NZURI KABISA HIYO.
ReplyDeleteMAMA YANGU WEEEE, LEO MAGOMENI HAPATAKALIKA.
ReplyDeleteAlisisitiza Askofu Mkuu Mtega: “Aidha, napenda kushukuru na kupongeza ushirikiano mzuri kati wa wananchi wa Ukonga na shule yetu ile ya chekechea na pia kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Mbunge wa Ukonga, Mhe. Makongoro Mahanga.”
ReplyDeletehawajajiingiza kwenya mambo ya siasa, kumtembela rais na kuongea nae si siasa! kusaidia jamii katika maendeleo si siasa! it is just doing good to the community, it is a social responsibilty, it is not politics as one said above
ReplyDeleteHuu sio udini kabisaa.
ReplyDeleteWanajitahidi kufundisha wafuasi ni kiongozi gani ni bora mbele kwa Mungu au chaguo la Mungu ili wamchague.
Anon wa mwanzo kumbe unajuwa wangekuwa hawa ni wa bakwata hii peji ingejaa komenti 200.
ReplyDeleteof kozi bakwata hawawezi kufika ikulu labda kufuturu wakikaribishwa.
Ukurasa huu kuwa tupu kunaonyesha watu wa dini fulani wana staha, hawakuchonga.
ReplyDeleteNaona huu ndio mwanzo wa kampeni za udini. Baada ya waraka sasa wanaingizwa ikulu, je hii tuiite ni siasa za kampeni au tuite kitu gani? Jamani tutaamka lini na hivi viini macho vya wana siasa? Inabidi tujihadhari sana na hii itikadi.
ReplyDeleteCertainly, this was a political trip of this Archbishop to State house, as the Kingunge saga is now prevailing
ReplyDelete